Kanisa Katoriki linaelekezwa wapi ikitokea Papa kapingana na maagizo ya maandiko

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,596
15,393
Kauli za Papa akiwa kwenye kiti chake cha mamlaka ni Extracathedral (hazipingiki wala kazigeuziki).
Hii ndio sababu unapaswa kuwa makini kujua kauli amezitoa akiwa wapi? Mfano kuna kipindi alitoa kauli tata akiwa anahojiwa kwenye ndege baadhi ya wananzuoni wa kidini wakatetea kusema hayo ni maoni yake sio extracathedral.

Nimeona ndugu zangu Wakatoriki wa JF wakikatishwa tamaa na mwenendo wa kauli zikitishi za maandishi na maagizo ya Papa kuhusu watu wa mapenzi ya jinsi moja.

Najiuliza kanuni zao za kidini zinawaelekeza waende wapi ikitokea Papa kwenye kiti cha enzi ananena kinyume na Aliye juu?

Sababu ya dukuduku langu ni dini ya kikatoriki wanaamini katika fundisho la Infallibility of pope ( Yaani Papa hakosei au haanguki). Pili wanaamini Maneno ya biblia yako sawa tu na kauli za Papa au maamuzi ya kikao cha kikanisa.

Dini hii inatoa mwongozo gani kwa wafuasi wake ikitokea kiongozi mkuu Papa ameingia chaka au ananena yaliyo juu?

Wajuvu mnisaidie. Ni kwa nia njema ili tujifunze sote na kama kuna kitu unaona hakiko sawa, ukikosoa kwa hoja zenye mashiko nitakukubalia.

Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom