Kanisa Katoliki LATOA MWONGOZO WA MAONI YA KATIBA

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=6]Kanisa Katoliki lahoji madaraka ya Rais

LATOA MWONGOZO WA MAONI YA KATIBA, LATAKA ASITEUE MAJAJI, WABUNGE WAKUU WA MIKOA, ASHTAKIWE

KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limetoa mwongozo kwa waumini wake, likiwataka kushiriki mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya, huku likihoji madaraka makubwa aliyonayo Rais katika mambo mbalimbali.[/h]
 
Kwa hiyo wakatoliki tutatoa maoni kama kundi baada ya kupata mwongozo toka kwa maaskofu? Vitu kama hivi ndivyo huleta chokochoko. Wenzetu wa upande wa pili nao wakitoa muongozo kwamba mahakama ya kadhi iingie kwenye katiba itakuwaje?

Najua maaskofu wameongelea tu hayo madaraka ya rais lakini hivi ni muhimu wao kutoa muongozo kwa waamini? Kwa nini tusiachiwe tutoe maoni yetu kama watu huru bila viongozi wetu wa kiroho kuingilia? Hayo yatakuwa ni maoni ya kanisa au maoni ya waamini?
 
Viongozi wa dini kutoa msimamo juu ya jambo fulani kwa waamini wao ni suala la kawaida maana labda watu watafsiri wanavyotaka. Mi nijuavyo kila tuendapo kwenye majumba ya kuabudia tunapewa misimamo ya mambo mbalimbali juu ya imani yetu.

Mojawapo ni kuacha dhambi...na hadi leo haishangazi kwa nini waamini bado wanatenda dhambi pamoja na viongozi wao wenyewe kutoa miongozo. Mi nadhani kutoa mwongozo ni msimamo wa pamoja halafu kila mmoja anautekeleza kadiri ya dhamiri yake na nafasi yake katika jamii.

Rais kwa mfano yeye mwenyewe atasita kutoa msimamo wake juu ya madaraka yake mwenyewe pamoja na kuwa viongozi wake wa dini wanaweza kuwa wametoa msimamo wao.
 
And its their judicial right, actually vikundi vyote vimepewa rai ya kutoa maoni

Na huu mchezo kuwa simtambui so and so bcoz I don't agree with them, won't fly,we might not agree with Kikwete but he's our president we might have not voted for him but he got the majority ...that's democracy...

Kuwa makini...uhuru wa kutoa maoni, ni ili usikilizwe lakini haina maana utakacho ndicho...

Ok..smile n wave guys
 
[h=6]Kanisa Katoliki lahoji
madaraka ya Rais

LATOA MWONGOZO WA MAONI YA KATIBA, LATAKA ASITEUE MAJAJI, WABUNGE WAKUU
WA MIKOA, ASHTAKIWE

KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limetoa mwongozo kwa waumini
wake, likiwataka kushiriki mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya, huku
likihoji madaraka makubwa aliyonayo Rais katika mambo
mbalimbali.[/h]

chombo pekee kilichopewa mamlaka ya kusikiliza na kuratibu maoni ya katiba ni Tume ya mabadiliko ya katiba na ipo kisheria na sio kanisa katoliki,hao maaskofu wanavunja sheria za nchi kwa kuwahawishi waumini kufuata mawazo ya kanisa! washtakiwe haraka!
 
Hongereni maaskofu! Haya... tusubiri miongozo ya viongozi wa Wasukuma, Waha, Freemansons, Salafi, nk. kwa wanachama wa jumuiya zao
 
Hongereni maaskofu! Haya... tusubiri miongozo ya viongozi wa Wasukuma, Waha, Freemansons, Salafi, nk. kwa wanachama wa jumuiya zao

Ndiko tunakoelekea huko! Natamani kusikia muongozo toka kwa wazee wa Kikurya huko Tarime. Nadhani wao watatoa muongozo kwamba musuba uhalalishwe ndani ya katiba na kuwa zao la biashara.

wasukuma watataka chagulaga iwe halali kikatiba.
 
Ndiko tunakoelekea huko! Natamani kusikia muongozo toka kwa wazee wa Kikurya huko Tarime. Nadhani wao watatoa muongozo kwamba musuba uhalalishwe ndani ya katiba na kuwa zao la biashara.

wasukuma watataka chagulaga iwe halali kikatiba.

KAbla ya sensa serikali ilihamasisha hata dini kuwaasa waamini wao wahesabiwe sasa linapokuja suala la Katiba kanisa kuwakumbusha waamini wao kuchangia maoni yao inakuwa taabu sana. Sooooote tunajua kuwa kabla ya kuwa na mchakato wa katiba mpya kulitakiwa kuwa na ueleweshaji wa katiba ya zamani ili unapochangia maoni juu ya katiba mpya uwe unaelewa nini kiwemo na nini kisiwemo. Hilo halikufanyika kwa makusudi ya kiburi cha watawala. Kanisa katoliki linachofanya ni hicho serikali ilichoamua kutokukifanya kwa makusudi!!
 
Sijasikia kuwa kanisa limetoa mwongozo, nadhani ni neno ambalo mwandishi ameamua kulitumia kwa matakwa yake. Kanisa limetoa maoni na wala siyo mwongozo, hawa ndiyo waandishi wapotoshaji. Ni lazima tufahamu kuwa katika mchakacho huu kuna maoni ya watu binafsi na maoni ya makundi ya kijamii na taasisi, na kufanya hivyo wala siyo kosa.

Kwa hiyo wakatoliki tutatoa maoni kama kundi baada ya kupata mwongozo toka kwa maaskofu? Vitu kama hivi ndivyo huleta chokochoko. Wenzetu wa upande wa pili nao wakitoa muongozo kwamba mahakama ya kadhi iingie kwenye katiba itakuwaje?

Najua maaskofu wameongelea tu hayo madaraka ya rais lakini hivi ni muhimu wao kutoa muongozo kwa waamini? Kwa nini tusiachiwe tutoe maoni yetu kama watu huru bila viongozi wetu wa kiroho kuingilia? Hayo yatakuwa ni maoni ya kanisa au maoni ya waamini?
 
Ndiko tunakoelekea huko! Natamani kusikia muongozo toka kwa wazee wa Kikurya huko Tarime. Nadhani wao watatoa muongozo kwamba musuba uhalalishwe ndani ya katiba na kuwa zao la biashara.

wasukuma watataka chagulaga iwe halali kikatiba.

Mapanga yagaiwe bure nchi nzima.
 
kweli nyani haoni kundule, kunya anye kuku akinya bata kaharisha, ndo sasa nazidi kuamini hii misemo. ki ukweli udini upo wazi wazi kwenye nchi hii ya tanzania, je? wangesema wale wa upande wa pili ingekuwa reactiona za watu kama si kusengenya na kejeli, na post ingewekwa humu jf ingekuwa ishashambuliwa sana mpaka sasa! nazidi kuamini mfumo wa dini fulani kuiongoza na kutoa maamuzi kati hii nchi kweli upo, na ingekuwa upande wapili wametoa yao, humu ungesikia jk dhaifu kaupandikiza mwenyewe udini, duuh, tunaelekea kubaya sana.
 
[h=6]Kanisa Katoliki lahoji madaraka ya Rais LATOA MWONGOZO WA MAONI YA KATIBA, LATAKA ASITEUE MAJAJI, WABUNGE WAKUU WA MIKOA, ASHTAKIWE KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limetoa mwongozo kwa waumini wake, likiwataka kushiriki mchakato wa kutoa maoni ya Katiba Mpya, huku likihoji madaraka makubwa aliyonayo Rais katika mambo mbalimbali.[/h]
Unamaanisha nini unaposema kanisa katoriki limetoa mwongozo?weka ushahidi tuone kama ni MWONGOZO au NIMAONI? weka nakara tusome wenyewe.
 
Kanisa lina wajibu wa ku-mobilise waumini wao katika mambo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na zaidi kiroho (inaitwa diaconia). Ni muhimu kuhamasisha wananchi kutafakari na kufanya maamuzi sahihi bila shuruti, kwani mwisho wa siku huwezi kuhubiri imani kwa kundi la waumini wasio wasomi, wagonjwa na maskini wa kutupwa. Ndio maana kila kundi la dini linajitahidi kuongeza nguvu kwenye afya, elimu na uchumi.
Nilisali kwenye kanisa la kilutheri pia miezi kadhaa iliyopita mkoa fulani, na ilitangazwa kuwa waumini wanawajibika kuandika maoni yao na kuyafikisha kwa kiongozi wao. Yatakuwa compiled na kuwakilishwa. Sikuona tatizo kwa sababu ni wengi hatujui hata ratiba ya tume kufika vijijini kwetu, na huenda tukawa safari.
Kutotangaza waumini wapeleke maoni yao ya katiba katoliki haitawazuia waislamu kutaka mahakama ya kadhi. By the way sio waislamu wote wanaotaka mahakama ya kadhi, kama ambayo pia kuna wakristo wanao-support mahakama ya kadhi.
 
Mkuu King'asti huoni shida hapo ambapo maoni yanapelekwa kwa kiongozi wa kanisa na kuwa compiled? Kama kuna muamini ambaye anataka utoaji mimba uhalalishwe atakuwa huru kweli kusema hilo kupitia kwa kasisi? Mimi kwa mfano nataka pombe iwe inauzwa masaa 24 lakini nasali kanisani (Mfano Lutheran) nitaweza kusema hivyo kwenye maoni yanayopitia kwa mchungaji? Kwa nini wasingepeleka kwa viongozi wa kiserikali mfano mtendaji/mwenyekiti wa kijiji? Naona hapo kuna udikteta wa kidini katika kubaka uhuru wa maoni ya waamini. Maoni yakihusishwa na imani lazima yatakuwa biased. Makanisa yangewahamasisha wananchi/waamini kwenda kutoa maoni yao sehemu husika bila kutoa miongozo. Mkuu unajua kitu imani ni hatari sana.
 
Last edited by a moderator:
Mi mwenyewe na rafiki zangu tunaandaa mwongozo! napendekeza JF tutoe mwongozo wetu tuukabidhi kwenye tume ya katiba!!
 
Back
Top Bottom