Kaniomba nizae naye!!

(Usje sema sikukuambia) Hahaha. Nashkuru sana Mkuu
Ushuhuda:

Nimezaa na mwanamke ambaye ana maisha mazuri tu na yeye alinishawishi hivyo hivyo kuwa sitokusumbua kuhusu malezi ya mtoto nahitaji uniachie alama tu ya mbegu yako.

Kizaa zaa kilianza alipokuwa mjamzito Mara anapiga simu Saa sita za usiku uzuri simu nilikuwa sizimi naweza silent mode. Nikiamka asubuhi nakuta missed calls zake na SMS za kutosha tena lawama na matusi ya nguoni kwangu na mke wangu.

Ikanibidi niwe nazima simu ili kumkwepa yeye maana nilihofia ipo siku atapiga simu imkute make wangu yupo macho akiona ule mwanga wa simu anaweza kuipokea au kuniamsha niipokee ikawa gharika bure.

Alipojifungua akawa analazimisha niende kulala kwake angalau siku moja kwa mwezi nalo ikawa shida ugomvi mpaka sasa hivi mtoto ana miaka mitatu hatuna mawasiliano mazuri na maelewano yetu ni dhaifu sana.

Ninachoshukuru ni kuwa hapajui kwangu maana alishasema siku akipajua tu siku hiyo atakuja kujitambulisha kwa mke wangu ili ajue kuwa wapo wawili.

Ujumbe ninaotaka uupate hapa mkuu ni kuwa bora uachane na huyo mwanamke tu vinginevyo atakusumbua sana baadaye na ndoa utakuja kuiona chungu kwa tamaa ya muda mfupi tu.

Usije sema sijakuambia.

Take it from me
 
Nshatoa majibu ya kwamba Labda tuandikiane So kasma atanichek baadaye
You better negotiate on your own, think teice, think rationally and very critical about the future life of your kid,

Mda mwingine anaeza kukuomba hivyo kumbe naye kashapachikwa na mwingine, ila sasa kinachobaki ni ujichengetu akubambikizie ili apate wakulea naye hiyo mimba na mtoto.

Hebu jitambue nduguyangu, amka kifikra.
 
Ndoa yako Ina furaha, shetani anakunyemelea na utaangukia dhambini.
 
Usikubali, kauli za kusema nitalea mwenyewe zimewaponza wengi na ikitokea ukafariki ataisumbua sana familia yako. Kama upo tayari kuzaa nae na ukibari kumuoa kabisaaaaa ifahamike ni mke wa pili. Nimemaliza
Mtoa uzi chukua huu ushauri. kwa kuongezea
Hayupo mwanamke atakayesema atalea mtoto pekee yake ikiwa baba yupo na mna mahusiano mazuri. Hiyo ni gia ya kukiingia ila baada ya siku lazima uwajibike kama baba na atakusumbua sana na usipoangalia unaweza kuvunja ndoa yako. Angalia usije kuwa km baba yake na Mwana FA au Diamond. Kama utaamua kuzaa na huyo bibie toa matumizi kama baba. Ni ujinga wa hali ya juu kukubali mwanao aliyetoka kwenye kiuno chako kulelewa na mwanamke bila ya ww kugharamika. Itakucost na ukumbuke watoto wa siku hizi siyo km wale wa zamani.
Muda utaongea.
 
Baada ya kutembelea mji mmoja nilbahatika kukutana na Bint mwenye maisha/Biashara zake.

Baadaya muda tulianza mahusiano lakin nilimuambia ukwl kuwa nina mke na ni Baba wa mtoto mmoja,
tuldet naye mara mbil tu kwa miez miwl tofaut nilienda mwaka jana mwez 9 ndo mwez ambao mahsiano Yalianza na nikaenda mwz 10 baada ya hapo sjaenda tena maana nilcho kifata nilkamisha.

Cha ajabu mwez huu yaan Jana saa 2:45pm kanpigia sm ananiomba Tuzae me nikamwambia ukwl siwz tunza Nyumba mbil I mean kulisha hku na hku kasma kuhsu hlo nisjal atahdumia kila kitu labda akiugua tu ndo nawza lazmika Changia Napo kwa 25% tu.
Nimemwambia subr nilfkirie wana Jf Naomba mawazo yenu nikubal na Je wife akjua? Japo yupo mbal ila hii Dunia hamna sir ya watu wawl


Nb: Ndoa yangu ni moja kat ya Ndoa zenye furaha Dunian

Usithubutu kuzaa naye kwa kigezo cha yeye kumhudumia mtoto bila kukusumbua... Utajuta kama walivyojuta wengine wengi.
 
Baada ya kutembelea mji mmoja nilibahatika kukutana na Binti mwenye maisha/Biashara zake.

Baada ya muda tulianza mahusiano lakini nilimuambia ukweli kuwa nina mke na ni Baba wa mtoto mmoja.

Tuli-date mara mbii tu kwa miezi miwili tofauti nilienda mwaka jana mwezi 9 ndio mwezi ambao mahusiano yalianza na nikaenda mwezi wa 10 baada ya hapo sijaenda tena maana nilichokifuata nilikamilisha.

Cha ajabu mwezi huu yaani Jana saa 2:45pm kanpigia simu ananiomba tuzae mimi nikamwambia ukweli siwezi kutunza nyumba mbili I mean kulisha huku na huku, akasema kuhusu hilo nisijali atahudumia kila kitu labda akiugua tu ndo naweza lazimika kuchangia napo kwa 25% tu. Nimemuomba asubiro nilifkirie.

WanaJF naomba mawazo yenu nikubali?

Je, wife akojua Japo yupo mbali ila hii dunia hamna siri ya watu wawili.


Nb: Ndoa yangu ni moja kat ya Ndoa zenye furaha Dunian
Mkuu usijaribu hicho kitu kabisa we pambana na familia yako tuu. Hata mimi kuna ex wangu alishawahi kuniambia hivyo nikamtolea nje. Yaani kulikua hamna maelewano nikamuambia basi tuachane, akasema kama unataka tuachane nipe mimba basi nitalea mwenyewe. Nikamuambia mimi sitaki kuona mtoto wangu analelewa na baba mwingine, nikasepa. Kwa hiyo mkuu we achana nae atakuja kukusumbua huyo.
 
Back
Top Bottom