Kanga yazua kizaazaa.

kakuruvi

JF-Expert Member
Sep 2, 2009
770
256
Jamaa mmoja mkaazi wa Lamu amempa mkewe talaka baada ya kukasirishwa na maneno yaliyokuwa yameandikwa katika kanga aliyovaa mkewe.

Jamaa alikuwa amesafiri kwa muda wa miezi 3, alishtuka aliporudi na kukuta mkewe amevaa kanga iliyoandikwa: "KULIKO KIOZE, HERI NIMPE JIRANI"
 
Kinachooza si chakula pekee yake? Au jamaa alielewaje?!
 
Na angeiona hii "Hata kama usingerudi jirani anatunza vizuri"
 
hahahahah.....sasa yeye miezi mitatu mke hana hamu ya dushelele? ameyataka
 
Hahaha umenikumbusha maneno haya kwenye kanga nyingine nliiona kariakoo, "Sikutaka kiliwe na nyenyere.":nerd:
 
Mwanamke mwingine alinunua chupi imeandikwa UTAJIJU. Ilizua timbwili kubwa katika ndoa yao ijapokuwa hawakuachana.
 
Unajua kiuswazi, Kanga hufikisha jumbe mbalimbali
kwa mfano Uke wenza kujiamini

Nimeridhika na hali yangu,

Mimi ni kama bata nikikosa nchi kavu baharini ntapata,

Nikweli lakini hayakuhusu,

Sasa kama mwanaume anafuatilia mambo hayo lazima ahamaki, Utachukuaje khanga yenye maneno ambayo hayana mafundisho.
 
Haina SHOBO yeye angekula tu labda kaogopa kubambikiziwa mimba.
Talaka aliyompa sasa jamaa wataitifua kila kona isiyofikiwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom