Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 158
- 175
Kanda ya ziwa sukari imeisha, msambazaji mkuu anyimwa mzigo
Hali ya upatikanaji wa sukari katika mikoa ya kanda ya ziwa ni tete, baada ya kiwanda cha Kagera kukataa kumuuzia Sukari msambazi mkuu kampuni ya V.H SHAH.
Inaelezwa Msambazi wa sukari kanda ya ziwa amenyimwa sukari na kiwanda hicho baada ya kushindwa kufikia gharama za manunuzi ya mzigo uliokuwa umeingia bandarani.
Siku tatu zilizopita Kagera Sugar iliingiza meli yenye shehena ya sukari katika bandari ya Mwanza kusini lakini baada ya kufikisha mzigo huo, alishindwa kuuza kwa gharama iliyozoeleka kwa msambazaji.
Baada ya mvutano wa gharama za kuuziana sukari, Kagera waliamua kuuza moja kwa moja kwa wafanyabiashara wakubwa jijini Mwanza ambao wamekiri kuuziwa sukari.
Bei ya jumla ambayo Kagera Sukari walitaka kuuza kwa msambazaji mkuu wa kanda ya ziwa kwa mfuko wa KG 25 ni shilingi elfu 70,000 huku mfuko wa KG 50 kwa shilingi 140,000.
Inaelezwa mfuko wa KG 25 Msambazi huuziwa na kagera sukari kwa shilingi elfu 62,000 wakati ule wa KG 50 akiununua kwa shilingi elfu 124,000 kitendo ambacho kimeibua mgogoro.
Kutokana na hali hiyo Msambazaji wa sukari kanda ya ziwa kwa sasa inaelezwa hana mzigo ambapo ofisi zake zimefungwa na kusababisha wananchi kukosa sukari toshelezi.
Mmoja wa wafanyabiashara jijini Mwanza (jina lake limehifadhiwa), amekiri kununua sukari moja kwa moja kutoka Kagera sukari licha ya kudai ununuaji wa sukari wa namna hiyo unaweza kusababisha baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kuficha sukari.
"Mfano mimi nilipata sukari kutoka kiwandani, Kagera walituuzia sisi moja kwa moja ila nahofia kuna siku nitakosa mzigo, unajuwa wenzetu sio waaminifu wanachukua mzigo wanaficha ili kutengeneza mazingira ya kuadimika," amesema mfanyabiashara huyo.
"Utaratibu mzuri ni ule wakununua kutoka kwa msambazaji maana huyo serikali inaweza kumbana kuliko kila mfanyabiashara kununua moja kwa moja kutoka kiwandani hiyo ni mbaya sana," ameeleza mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo kwa sasa hali ya upatikanaji sukari katika mikoa ya kanda ya ziwa ni mgumu na sababu kubwa inatajwa ni kiwanda cha Kagera sukari kushindwa kuuza mzigo kwa msambazaji mkuu.
NB: Waziri Bashe anasema sukari nchini ni ya kutosha, lakini cha kushangaza msambazi wa sukari kanda ya ziwa hana sukari hiyo sukari ya kutosha ipo wapi?