Kanda maalum ya ushirikina

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,641
698,017
1473435033208.jpg
kila kinachotokea kwenye ulimwengu wa macho ya kawaida ni replica ya ulimwengu wa roho! (Ushirikina ni mkusanyiko wa juju uchawi ulozi chumaulete kuwanga nk)
Tunapozungumzia kanda maalum ya kitu maana yake ni kwamba eneo hilo lina uhitaji wa ziada wa huduma fulani
..mfano Dar kwa sasa ni kanda maalum ya kipolisi kutokana na matukio ya ujambazi kushamiri! Kariakoo kwa sasa ni kanda maalum ya kodi za mamlaka ya mapato Tanzania kutokana na uhitaji wake!
Eneo lote la pwani ya Dar nenda mpaka bagamoyo msata wami pangani mbwewe mkata mpaka tanga mjini ni kanda maalum ya ushirikina
Hapa ndio kuna vilinge vingi vya ushirikina kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania, hapa ndio kuna wachawi waganga na walozi(kwa ujumla wao washirikina wa kila aina)
Hapa ndo kuna kila aina ya matibabu kuanzia miti shamba tunguli kisomo mpaka uganga/uchawi wa kitabu
Unaweza kwenda mikoani na sehemu tofauti kama gambosh nk lakini ukashindwa kwa hakika kukutana na ushirikina halisi....huu ukanda hukosi
1473435815100.jpg

Kwanini ukanda huu lakini?
Mazingira na jiografia yanaruhusu, malighafi za baharini na nchi kavu vinapatikana kwa wepesi urahisi na kwa wingi! Taka viungo vya binadamu hupati shida! Taka makombe na mazao bahari mengine ni rahisi mno! Taka variaties ya mizizi miti magome na hata matunda na majani huku sio tatizo kabisa
Lakini kwanini isiwe ndani ya Dar na ni nje ya Dar na maeneo ya karibu au mbali kidogo?
Ushirikina ni mambo ya kiroho zaidi yasiyo na ithibati za kisayansi! Yanahitaji ukimya utulivu upweke usiri uchache wa watu na kitu chochote kilichoendelezwa na binadamu kwenye ulimwengu wa teknolojia..teknolojia na usasa ni sumu kubwa kwenye ushirikina
Unaposhuhudia misafara isiyokoma kwa waheshimiwa sana Unaposhuhudia ajali za kila siku! Unaposhuhudia upotevu wa watu wazima na watoto! Unaposhuhudia mambo ya ajabu ajabu usishangae sana bali jua kwamba uko karibu kabisa na ukanda maalum wa kishirikina
1473436726118.jpg
 
Vip sumbawanga?
Na je utatusahau vp watu wa morogoro-Malinyi zaman ikijulikana ulanga ambako kulikuwa na bibi aliekuwa anawatoa uchawi na kuacha kabisa na kuwa mtu mwema hata uwe mchawi wa wapi hapa tz.
Tena ukiuliza kwa bibi lazma ufikishwe kwake
Nawasilisha hoja
Ni sawa lakini huko hakujafikia viwango vya kanda maalum
 
View attachment 397114usafiri wa namna huu ni wa kiwango cha chini sana kuweza kuukuta kwenye kanda maalum..maendeleo kwenye ulimwengu wa kawaida huenda sambamba na maendeleo kwenye ulimwengu wa kiroho..hivi hapa Dar na maeneo ya jirani unaweza kweli kumkuta mtu anafuga fisi?
Kwa hiyo tunaweza kufananisha na vitz kwa huku kwetu sasa mwenye hammer au bugatti anakuwa na usafiri gani kwa mfano maana umeandika teknolojia na usasa upo pia huko
 
Dar ndo kitovu wakifanya kollabo na Tanga ni miji ambayo inaongoza kuwa na misukule wengi...kwa Dar misukule ni biashara hasa kariakoo bila kusahau tanga...kiongoz kanda hizo ulizozielezea zina mambo ya ajabu lakini watu wanaofanya mambo hayo ya ajabu huwezi amini
 
View attachment 397114usafiri wa namna huu ni wa kiwango cha chini sana kuweza kuukuta kwenye kanda maalum..maendeleo kwenye ulimwengu wa kawaida huenda sambamba na maendeleo kwenye ulimwengu wa kiroho..hivi hapa Dar na maeneo ya jirani unaweza kweli kumkuta mtu anafuga fisi?
Mkuu ina maana Pwani ina rasilimali za kutosha juu ya uchawi? Je wale wachawi wa kanda za mbali na pwani kama sumbawanga hufunga safari kuja pwani kufuata rasilimali?
 
Back
Top Bottom