A
Anonymous
Guest
Mimi ni miongoni mwa wafanyakazi (150+) wa M-gas Cooking Limited. Hatujalipwa mshahara wa mwezi wa pili bila taarifa yoyote zaidi ya hapo tulipokea taarifa kwa njia ya email kwamba kampuni imeshindwa kutulipa mshahara kutokana na matatizo yao ya kibenki na masuala yote ya kampuni tumuone Andron Mendes ambae alikuwa mkurugenzi wa kampuni kabla ya kutangaziwa mkurugenzi mpya, ila kilichotushtua zaidi ni kuondolewa kwenye mifumo ya mawasiliano ya ofisi na ofisi za kampuni kufungwa mwanzoni mwa mwezi wa tatu.
Maboss waliokua wakitusimamia wamefungua kampuni mpya M-gas Resources na kuhamishia shughuri zote za kampuni huko huku sisi tukiterekezwa bila kulipwa mishahara na bila kuvunjiwa mikataba yetu. Michango yetu ya NSSF haijalipwa tokea mwezi wa 12 mpaka sasa na hatuna hata termination letter ili iweze kutusaidia kupata stahiki zetu.
Hii ni njia mojawapo tumeamua kuitumia ili suala letu liweze kuwafikia wahusika ngazi za juu tuweze kupata msaada na kukomesha wamiliki wote wa kampuni wenye nia ovu kwa vijana wanaopambana kujikwamua kimaisha.
Ahsante