Elections 2010 Kampeni za KIkwete Dodoma, Kumbe wananchi wanafuata Muziki ktk kampeni za CCM!

Hata hapa alihutubia hardly dk kumi na tano tu. Kwani wananchi walikuwa wanatoka continously!! Akahofia angekuwa akiongea mwenyewe!!


Hii ya wananchi kuondoka mikutanoni hasa baada ya JK kupanda jukwaani si nzuri hata kidogo kwani inawapatia muda CCM kujipanga na kuweka mkakati mpya - kuiba kura etc.

Wananchi wangekuwa wanakaa na kumsikiliza tuuuu mpaka mwisho na siku ya uchaguzi, wanamtwanga chini kwa kishindo
 
Ni kweli kabisa. Tuungane kwa pamoja tumnyime kura zetu. Halafu hivi watu wa Ingunga, Bariadi (kwa Chenge), Monduli na Rombo wamelishwa nini mpaka wakubali hata kuhudhuria mikutano ya kampeni ya wahujumu uchumi wa nchi yetu?w

Mzee mbona unamsahau Rage aliyepata kufungwa kwa kuiba pesa za TFF?
 
Nimehudhuria Kampeni za kikwete leo hapa Dodoma katika uwanja wa jamuhuri. Mkutano ulianza kwa wanamuziki mbali mbali kutumbuiza na wananchi wakawa wanashangilia sana.
Baada ya muda kupita Mgombea Uraisi akapanda jukwaani kwa ajili ya kuwahutubia wananchi.

Baada ya kupanda tu jukwaani na kuanza kuongea, watu walianza kutoka kwa wingi mno mpaka wakawa wanabanana milangoni, baadhi ya mageti yalikuwa yapo upande aliotazama mgombea, nikaona Askari wakiwazuia wanachi wasitoke na kufunga mageti yote yaliyombele ya kikwete hivyo wananchi kulazimika kutoka kwa kutumia mageti ya nyuma, hata hivyo bado wananchi waliendelea kutoka.

Je! hii inaashiria kuwa wananchi wanafuata burudani tu ktk mikutano ya CCM, na si Sera za chama?? Au wananchi wanaona hakuna jipya la kulisikia kutoka kwa CCM, kwani wamekuwa wakiimba wimbo huohuo lakini hali za maisha za wananchi ziko duni kili kukicha????

Pia mpaka naondoka saa kumi na mbili na nusu, alikuwa bado hajaondoka uwanjani,na miziki ilikuwa ikiendelea, hapa si ameibanjua sheria ya uchaguzi????

John Samuel Malecela naye alikuwepo kwenye meza kuu?
 
KURA YANGU NI KWA SLAA, MWACHE JK ACHUKUE NCHI KUPITIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jeshi la ulinzi na Polisi lakini si kwa Kura yangu
 
KURA YANGU NI KWA SLAA, MWACHE JK ACHUKUE NCHI KUPITIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jeshi la ulinzi na Polisi lakini si kwa Kura yangu
Point.
But piga kura simamia, na THIBITI. utafanikiwa kumuondoa huyu nguli.
 
jana pale uwanja wa jamhuri nilimuona MS amavumilia jua kali hadi mwisho wa Kampeni, hongera MS kwa mapenzi yako kwa JK japo sina uhakika kama mnafamiana.
 
wingi wa shamra za kampeni za JK ni kuficha udhaifu wake, huyu jamaa sasa hivi kila uchao afya ya ubongo inazidi kutetereka, hawezi kusimama zaidi ya robo saa. Ila amejitahidi kupata uzoefu akijisikia kiwi cha macho fasta anashuka kwenye jukwaa na wadakaji wanamuwahi kumpeleka akazimikie kwenye chopa. Hivi sasa kuanguka ni oder of the day kwa JK.
 
Tuwe wakweli ccm mwaka huu wana wakati mgumu sana,kwani wanalazimisha wananchi kwenda kwenye mikutano yao, nimesikitishwa sana na hawa wenzetu wa ccm jana kwenye kampeni zao wamewalazimisha wanafunzi wa shule za msingi tena bila aibu na uniform zao waje wajaze uwanja,kweli wamefilisika na wamezidiwa!!wasiwalazimishe watu kwenye mikutano yao wawawche waende wenyewe kwa kufuata sera zenye matumaini kwani zao zimeshindwa japo kuwapa wananchi matumaini!!
 
Back
Top Bottom