Kampeni ya kwenda shamba siyo ushamba

ndo vile

Member
Mar 11, 2023
25
12
“KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA, KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA COMPAIGN”

UTANGULIZI
Upatikanaji wa fursa za ajira kwa vijana wanaohitimu katika ngazi mbalimbali za vyuo imekuwa moja ya changamoto kubwa inayoikabili dunia ya sasa,ukosefu wa ajira kwa vijana umekuwa mwiba mchungu kwa serikali za nchi zinazoendelea hata nchi zilizopiga hatua kimaendeleo.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakifanya jitihada kubwa sana katika kupunguza tatizo la ajira haswa kwa vijana wanaohitimu katika ngazi mbalimbali za elimu ila kumekuwa na idadi kubwa sana ya vijana wanaohitimu katika vyuo mbalimbali na kuingia sokoni kila mwaka,idadi ambayo ahilingani na fursa za ajira zilizopo, kwa mwaka mmoja vijana wanaohitimu na kuingia kwenye soko la ajira ni zaidi ya 800,000 ila wanaopata ajira serikalini na sekta binafsi ni 10% tu jambo ambalo linachochea kuongezeka kwa idadi wa wahitimu wasiokuwa na ajira.

Katika kupunguza tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi, serikali ya Tanzania imeamua kuweka nguvu katika kilimo cha kisasa ili kilimo kiwe chanzo cha ajira, kiongeze kipato kwa mkulima,kiwezeshe nchi kujitosheleza kwa chakula,na kilimo kitumike katika kuimarisha uchumi wa nchi.

Miongoni mwa maeneo muhimu na yaliyopewa kipaumbele na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani ni sekta ya kilimo ambapo kupitia bajeti ya serikali ya mwaka 2022/2023 imeweka msukumo mkubwa katika kuboresha kilimo kwa kutenga bajeti kiasi cha bilioni 954 ikiwa ni ongezeko la 224%,ambapo fedha hizi zimeelekezwa katika ruzuku kwa ajili ya kushusha bei ya pembejeo kwa wakulima na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji ili kilimo kiweze kuwa kina tija na kuleta manufaa kwa wakulima na nchi kwa ujumla. Serikali pia ina mpango wakuanza kuwapatia vijana wa kitanzania mashamba yenye hati nakuwaunganisha na mabenki ili vijana hawa waweze kupata mikopo yenye riba nafuu ili kusaidia upatikanaji wa ardhi na rasilimali fedha kwa vijana jambo ambalo litaongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo.

Pamoja na serikali kutoa kipaumbele kwa sekta ya kilimo kwa kuja na mipango na mikakati mbalimbali ili sekta ya kilimo iwe chanzo cha ajira kwa vijana walio wengi,bado kundi kubwa la vijana haswa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu wanakichukulia kilimo kama shughuli ya watu wasiokuwa na elimu,kilimo ni kwa ajili ya wazee tena wanaoishi vijijini,kilimo ni kwa ajili ya watu wasiokwenda na wakati,kilimo ni sekta ngumu isiyotabirika,kiujumla kundi kubwa la vijana wanamtazamo kuwa”KWENDA SHAMBA NI USHAMBA”mtazamo hasi ambao unapelekea vijana wengi wanaohitimu vyuo kukosa shughuli za kuwaingizia vipato na kubaki kwenye lindi kubwa la umasikini.

KWANINI KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA, KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA COMPAIGN?
Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa(NBS),utafiti unaonyesha asilimia 56 ya nguvu kazi ya taifa la Tanzania ni vijana hususani wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 na wengi wao hawana ajira hivyo basi, kama vijana wakipata uelewa katika kutambua fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani ya sekta ya kilimo na kuzifanyia kazi,sekta ya kilimo ndiyo sekta pekee itakayowakwamua vijana kutoka kwenye changamoto ya ukosefu wa ajira na kuwatoa kwenye umasikini wa kipato,vijana wakitanzania wanapaswa kubadilishwa mitazamo hasi waliyonayo kuhusiana na sekta ya kilimo,”KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA,KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA”ni kampeni itakayokuja kuzitangaza fursa zinazopatikana kwenye sekta ya kilimo na kuondoa mitazamo hasi ya vijana kuhusiana na sekta ya kilimo na hivo kuongeza ushiriki wa vijana kwenye sekta hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais Samia Suluhu Hasani imeweka mazingira wezeshi kwa vijana kushiriki katika sekta ya kilimo,bajeti ya kilimo kuongezeka kwa 224%, utoaji wa ruzuku kwa ajili ya pembejeo, utoaji wa mafunzo ya kilimo na ufugaji kwa vitendo,utengaji wa maeneo mahususi ya uwekezaji ya pamoja kwa vijana,kupungua kwa riba kwenye mikopo ya sekta ya kilimo, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na utekeezaji wa programu mbalimbali za kilimo mahususi kwa vijana kama “JENGA KESHO BORA KUPITIA KILIMO” ni sababu tosha za kumuaminisha kijana wa kitanzania kuwa kwa sasa “KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA, KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA”

Pamoja na vijana wengi haswa kundi la vijana wasomi na vijana waliozaliwa na kukulia mijini kuchukulia kilimo kama kama kazi isiyo maana yoyote wakiamini kuwa watapoteza muda mwingi mashambani,lipo kundi la vijana wachache,waliotazama fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo na kujiajiri kwenye sekta hii ya kilimo na kuweza kufikia matarajio mazuri ya maendeleo binafsi, hivo kuepukana na tatizo la ajira na umasikini wa kipato,kundi hili la vijana ni sababu tosha na ni ushuhuda wa kuwa “KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA,KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA”

“KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA COMPAIGN”
Ni kampeni inayolenga kuwashawishi vijana wakitanzania haswa waliopo vyuoni na waliomaliziza vyuo katika ngazi mbalimbali kushiriki kikamilfu katika shughuli za kilimo, kampeni hii imelenga kuwaondolea vijana wa kitanzania haswa kundi la wasomi mitazamo hasi yote walionayo kuhusiana na sekta ya kilimo, kwa kupitia kampeni hii vijana wa Kitanzania watapata nafasi ya kuelezewa kwa mapana fursa zote zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo, mikakati iliyonayo serikali na wadau wa maendeleo katika kumuwezesha kijana wa Kitanzania kushiriki kikamilifu kwenye sekta ya kilimo na pia viijana watapata fursa ya kupata ushuhuda kutoka kwa vijana wenzao ambao wapo kwenye sekta ya kilimo na sekta hii imeweza kuwasaidia kufanikiwa kiuchumi ili vijana hawa waliofanikiwa waweze kuwaonyesha vijana wenzao kuwa inawezekana kufanikiwa kupitia kilimo na “KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA, KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA”

Vilevile kwa kupitia kampeni hii vijana wakitanzania watapata kufahamishwa taarifa zote muhimu na sahihi zinazohusiana na shughuli za kilimo kama, upatikanaji wa ardhi kwa vijana kwa ajili ya kilimo, upatikanaji wa rasilimali fedha na mitaji, upatikanaji wa miundombinu bora kwa ajili ya umwagiliaji, upatikanaji wa pembejeo bora na huduma za ugani kwa vijana, upatikanaji wa masoko ya uhakika ya bidhaa za kilimo,elimu ya ujasiriamali na biashara, ili basi vijana hawa waweze kuondokana na mitazamo hasi kuhusiana na sekta ya kilimo na kuongeza ushiriki wa vijana kwenye sekta ya kilimo.

MALENGO
LENGO KUU
Kupunguza tatizo la ajira kwa kuwahamisisha vijana wengi haswa wanafunzi waliopo vyuoni na wahitimu wa vyuo mbali mbali kushiriki katika shughuli za kilimo.

MALENGO MENGINEYO
Kuondoa dhana potofu walizonazo baadhi ya vijana kuhusiana na kilimo,kwamba kilimo siyo shughuli yenye staha na kushiriki kwenye kilimo ni kupoteza muda.

Kuhainisha fursa zote zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya kilio na kuongeza uelewa kwa vijana kutambua fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo.

Kuwapa taarifa sahihi vijana kuhusiana na mipango yote iliyonayo serikali pamoja na wadau wa maendeleo katika kumuwezesha kijana kushiriki kikamilifu katika sekta ya kilimo.

Kuwakutanisha vijana waliopo vyuoni,wahitimu na vijana wenzao ambao wamefanikiwa kupitia sekta hii ya kilimo ili vijana hawa waliofanikiwa waweze kushiriki katika kuwahamasisha vijana wenzao kujihusisha na shughuli za kilimo.

UTEKELEZAJI
Utekelezaji wa kampeni hii ya “KWENDA SHAMBA SIYO USHAMBA, KWENDA SHAMBA NDIYO UJANJA” utafanyika kwa kutumia makongamano na semina zitazokuwa zinafanyika kwenye taasisi mbalimbali za elimu za vyuo vinavyojumuisha vyuo vya kati na vyuo vikuu,kutokana na umuhimu wa kampeni hii vyombo vya habari kama runinga na runinga za mitandao zitakuwa zinaonyesha mubashara makongamano na semina hizi ili basi vijana wengi wapate kupata taarifa hizi muhimu kwa mustakabali wao na mustakabali wa nchi kwa ujumla.

WALENGWA
  • Vijana
  • Serikali kupitia wizara na taasisi zake
  • Taasisi za elimu za vyuo,vyuo vya kati na vyuo vikuu
  • Taasisi za kifedha, benki ya kilimo na benki ya kibiashara
  • Vyombo vya habari
“Vijana njooni kwenye sekta ya kilimo, tumejipanga kuwapatia mashamba na mashamba hayo yatakuwa na hati, hati zitatoka kwa majina ya vijana yatakayokuja kwa makundi au mmoja mmoja, lakini tumejipanga kuwaunga na mabenki ili kupata mikopo ya riba nafuu, tumejipanga vyema na masoko-Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan akihutubia kwenye kilele cha maazimisho ya sikukuu ya nanenane Mbeya tarehe.
 
Jambo jema na lakuungwa mkono, swali la kujiuliza huko shambani watatumia nyenzo zipi,je watafanya kilimo cha kutegemea mvua?je soko lipo la uhakika la mazao yao?
 
Matajiri wakubwa katika sekta ya kilimo waalikwe nchini, ili waweze kuajiri vijana kwa kilimo watakachofanya na kuweza kulipa mishahara minono laki 500,000/-kwa mwezi, tatizo watanzania kujisimamia kwenye kilimo ni ngumu sana.

Watakapofanya hivi mijini hakutabakia kijana,

N. B, wengi wanaozamia ughaibuni by75% huajiriwa mashambani.
 
Back
Top Bottom