Kamishna Chagonja aruhusu polisi washughulikiwe

kimsingi hakupaswa kutoa kauli hiyo kwani huu ni ukiukwaji wa good governance. Kwa kauli hii ni mauti kwa polisi hususani kwa kipindi hiki ambapo hakuna mahusiano mazuri kati ya wachimbaji wadogo na polisi huko mgodini. Alipasa kuagiza wao kuwakamata na kuripotia polisi na si kupiga hatimaye kifo.
kama kuna kitu hatari basi ndio hiki
 
Kamishna Chagonja amekodea sana hii kauli yake,
Polisi hawawezi kutulia tu wapigwe na Raia watajibu kwa nguvu zao zote,
Ametoa kauli kama mwanasiasa na si mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama,
Nchi hii inaongozwa kwa sheria hakuna anaepaswa kujichukulia sheria mikononi ila kupelekwa mbele ya vyombo vya haki/sheria,
Raisi na IGP wanapaswa wamuajibishe kwa kauli yake hii yenye kuchochea maasi ktk nchi hii ya Waungwana.
 
Ni wimbo wa Dr. Dre na unaitwa STILL. Sikiliza 1:10 kwenye wimbo.



Hii ilikuwa ni SOFT version baada ya Dre na kundi zima la NWA wakiwa chini ya Mjinga Easy E walipoimba wimbo huu hapa chini na kupata matatizo mengi sana na FBI. Kama sikosei walianza kuchunguzwa kila kona: F**k tha Police - by Nigga With Atitude.

N.W.A https://jamii.app/JFUserGuide Tha Police video - YouTube

Mh. tumekwisha ukisikia mauaji ya halaiki yalihamasishwa hivyo kule Rwanda. Hakuna Polisi mwema . Nimekumbuga tag moja ya jamaa yangu humu JF anasema STILL NOT LOVING POlice
 
Last edited by a moderator:
Godbless Lema alisema kwenye hotuba yake kuwa polisi wakatae kutii amri katili , serikali wakawa wakali sana na kusema ni uchochezi , hivi huyu kuamuru wananchi wawapige polisi wa chini sio uchochezi? Polisio wakianza kuuwawa na watakaouwa wakisema walipewa amri na Chagonja wataonekana kuwa ni wahalifu?
 
Hivi inakuaje mkuu kama Kamishna anapokosea - ingekuwa bungeni ningeomba muongozo, huku uraiani inakuaje, labda ajulishe ili akane au asahihishe/arekebishe tamko lake au?
 
Back
Top Bottom