Kamishna Chagonja aruhusu polisi washughulikiwe

Kamishna wa operesheni za jeshi la Polisi nchini, Paul Chagonja amewaruhusu wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka Mgodi wa North Mara, kuwapiga KAMA WEZI, askari wakorofi wanaowavamia na kuwanyanyasa kinyume na taratibu za jeshi hilo. Ruhusa hiyo ilikuja kufuatia tukio la jumanne wiki hii, la askari walioendesha operesheni ya kukamata watu kwa kulipua mabomu ya machozi, kwa maelezo kuwa walikuwa wanadhibiti waliongia mgodini kinyume cha taratibu. (chanzo:Mwananchi 27.8.11)

Mimi naona hii imekaa vibaya. Tena kwa pande zote mbili - wananchi na polisi.
Nawasilisha wanajamvi tuijadili.
 
Hawa watu wana matatizo.. ndio yale yale ya kina Pinda.. "wanaoua Albino na wao wauawe.."... grrrrrr
<br />
<br />
hapa ni kama anasema "mtajua wenyewe kuwa mnawafanya nini, sisi tumechoka, hatutak kelele"
 

Kamishna wa operesheni za jeshi la Polisi nchini, Paul Chagonja amewaruhusu wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka Mgodi wa North Mara, kuwapiga KAMA WEZI, askari wakorofi wanaowavamia na kuwanyanyasa kinyume na taratibu za jeshi hilo. Ruhusa hiyo ilikuja kufuatia tukio la jumanne wiki hii, la askari walioendesha operesheni ya kukamata watu kwa kulipua mabomu ya machozi, kwa maelezo kuwa walikuwa wanadhibiti waliongia mgodini kinyume cha taratibu. (chanzo:Mwananchi 27.8.11)

Mimi naona hii imekaa vibaya. Tena kwa pande zote mbili - wananchi na polisi.

Nawasilisha wanajamvi tuijadili.
 
Huyu Changnja ndiye aliyetoa taarifa ya polisi kuhusu tukio la askari kuua raia kule Arusha - anareconcile vipi aliyosema Arusha na haya ya Tarime?
 
Huyu ni kiongozi mkubwa sana,lazima apime kauli zake mara mbili kabla ya kutamka!wapi polisi jamii ya IGP mwema?lets wait and see..
 
hahaah........huyu yuko sahihi.polisi wakati mwingine ni wasumbufu sana
 
Sasa asubiri mishkaki ya askari wake, watabondwa na kutiwa kiberiti, shauri yake. Yaani Kamishina mzima wa polisi hawezi kuelewa athari za kauli yake mbele ya watu ambao tayari wameshakuwa na uadui wa nyoka na binadamu na askari polisi.
 
Kamishina, amekosea, aliatakiwa kuwajenga wananchi na wanajamii wa mgodini kujitambua kama watanzani na wote kusimama pamoja kupinga unyonyaji wa wezi a.k.a wawekezaji. Kuruhusu kupiga polisi ni sawa na kutangaza vita, na kama kweli watasikia ushauri wake, tutarajia athari mbaya zaidi.

ikumbukwe polisi hawatakubali kupigwa, watajibu mapigo. sasa itakuwa vita.

Polisi jamii na ulinzi shirikishi inaitaka jamii kushiriki kudhibiti uhalifu na sio kupambana na uhalifu. Alichotakiwa kukisema kamishina Chagonja, ni kutafakari kwa kina kwa nini polisi waitwe kufanya operation, wanafanya kwa manufaa ya nani, na wao wananufaika vipi na operation hiyo?

wakitafakari maswali hayo, nadhani polisi wataungana na wananchi kumpinga mwekezaji, kwani kwa mda mrefu amekuwa akipora rasilimali za watanzania kwa gharama ya watanzania wenyewe.
 
Acha yawe mapigano maana bila damu kumwagika pande zote, hakutakuwa na adabu nchi hii.Huyu Kamishina ana akili sana na nampongeza sana kwa hili. Huu ukunguru wa Watanzania ndiyo umetufikisha hapa.Wao pia wakiuawa wawili watatu, next time watafikiri mara mbili kabla ya kuvamia wananchi.Si unaona yule Mjinga alipeleka Mabaunsa kuhamisha watu Dar? Walichukua kipigo na sidhani kama kuna watu watathubutu kwenda kumfanyia kazi hata kama wana njaa maana wanajua watu watawatoa Baru, chupi mkononi. Kudadeki kamishina, you made my day.Tunahitaji NGOSHA wa kiukweli kama huyu Kamishina. Mkikutana naye kwa wale wanamfahamu, mpeni HONGERA zangu kutoka kwake.Mambo ya kupata kibao na unageuza shavu la pili, My Masaburi.
 
Mh. tumekwisha ukisikia mauaji ya halaiki yalihamasishwa hivyo kule Rwanda. Hakuna Polisi mwema . Nimekumbuga tag moja ya jamaa yangu humu JF anasema STILL NOT LOVING POlice
 
Back
Top Bottom