Kambi Gani ya JKT Inamafunzo Magumu?

Kambi ni mgambo 835 kj na ugumu wake unatokana na mashamba ambayo ya ukubwa unaoendana na wilaya kinondoni, ratiba za shamba ni kila siku
 
Kama amekwambia kapangiwa MAKUTOPOLA ametapeliwa.. Makutopola ni kambi ya malezi ya jkt na sio kambi ya mafunzo..
 
Kambi zote za Jeshi mafunzo ni magumu hapo Makotopora ndiyo balaa kuna maeneo hapo kama Mzakwe,miraba ya zabibu mirefu

Kubwa na muhimu ni utayari wa hali zote lakini kuanza kuuliza utajawa hofu buree
maana hujashtukizwa taarifa ya kwenda jeshini unayo jitahidi kupata somo la utayari naamini kila kitu kitakwenda sawaw
 
makutupora hamna depo la jkt, kilichopo ni kambi ya malezi ya servicemen(askari waliomaliza depo ya jkt kutoka vikosi mbali mbali vya mafunzo), sasa huyo mdogo wako kamwe hawez kwenda makutupora maana hapo wanatoa mafunzo ya jwtz tu so kuwa makini mtatapeliwa
 
kambi active za mafunzo ya jkt kwa sasa ni ...Kanembwa, Bulomborwa (zote Kigoma), Mgambo na Maramba (zote Tanga), Ruvu (Pwani), Msange (Tabora), Rwamkoma(Musoma), pamoja na Mlale(Songea). Hatuwez kusema kambi ipi ina ugumu au urahisi kimafunzo maana hilo suala linategemeana na wakufunzi ambao huwa wanahamishwa vikosi kila leo kwahyo cha msingi ufungue moyo uamini utamaliza depo regardless of kambi utakayopangwa na ujiulize hao waliopita huko wakahitimu wana nini cha ziada ambacho wewe huna?!. Lakini pia kwa upande mwingine wa shilingi kwenye suala la uzalishaji mali kambi ya Mgambo 835KJ wanalima sana wana mashamba ukubwa karibia sawa na umbali wa mbagala-kawe, mlale, msange na kanembwa pia wako vzuri ila cyo kama mgambo, ukitaka kazi wastani nenda maramba au rwamkoma maana viko town, ruvu hapo utalima mpunga mpaka utaomba poo, uwe na adabu maana degree yko unaiacha getini na si ajabu ukiamrishwa kufanya hzo kaz ngumu na katoto tu cha darasa la 7 kalichokuzid cheo so uvumilivu unahitajika
 
Ulichoongea ni sahihi kiongozi

Yale mashamba ya 835kj mgambo nayafahamu vizuri sana

"Genda genda" "Kwa msanga" ni makubwa kupita maelezo. Jeshi letu linalima si masihara
 
Hahahaaa! Mwambie afungue moyo anywe maji mengi atakutana na watu waliokunywa uji wa mgonjwa na mgonjwa kafa, mbwa kala mbwa, nyani kumkana mwanaye.... Hyo ataikuta akienda 841 kj mafinga
 
Ulichoongea ni sahihi kiongozi

Yale mashamba ya 835kj mgambo nayafahamu vizuri sana

"Genda genda" "Kwa msanga" ni makubwa kupita maelezo. Jeshi letu linalima si masihara

kabisa kiongozi na mara ya mwisho nilipotembelea mgambo niliacha shamba la kwa msanga linaongezwa ekari kama 4000 mpya yan ndio walikuwa wanakata miti na kuondoa visiki kwahyo hawa vijana wanaoenda intake hii hilo shamba litawahusu sana, mgambo mpaka imeongoza uzalishaji wa mahindi kwa vikosi vyote vya JKT mwaka jana ujue pale ngwimba ngumu sana kazi ipo
 
Makambi yote ukikuta na watu wanaoitwa WANAA hapo ndo kozi utaiona ngumu.
 
mossad 03
kwa uelewa wangu mafinga ni kambi ya mafunzo ya tpdf(bakabaka or jeshi kamili)
na si jkt

Mafinga ni kambi inayomilikiwa na jkt ila inaazimwa kwa tpdf kufanyia mafunzo. Ni kawaida sana mkuu.

Hadi Mwalimu Nyerere alipiga depo lake la mujibu wa sheria mafinga jkt

Angalia hiyo link ya official website ya jkt Mafinga JKT

Samahani kiongozi eti una undugu na mossad007?
 
Aliyeuliza hamnazo, Makutupola inahusika na mambo ya RTS, hapo wanaenda tu wale walioajiriwa na JWTZ, pia si kweli kwamba Makutupola kuna mazoezi magumu, huo ni upotoshaji, kama umepitia JKT basi kuna uwezekano mkubwa ukafanikiwa kumaliza miezi minne hadi mitano ya mwanzon wa mafunzo rasmi ya JWTZ (ya kivita).

Pia Makutupola sio kambi ya malezi, pale ni sehemu ambayo unaenda kufundishwa rasmi mafunzo ya kivita sababu Makutupola hamna habari za kulima kama ilivyo kambi za JKT.

ANGALIZO:
Makutopola ndio kwenye mazoezi rasmi ya kivita, hivyo ni sehemu inayohitaji umakini wa hali ya juu, endapo unajiona mvivu au mtoto wa Mama pale hapakufai kabisa, huwa watu wanapoteza maisha, kuzimia, hivyo ni vitu vya kawaida.

Pia ni sehemu ambayo ni ngumu kutoroka mafunzo tofauti na JKT ambapo wengi wao wanaoshindwa mshikemshike huwa wanatoroka!
 
Back
Top Bottom