Kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya ziko kikatiba?

ngonani

JF-Expert Member
Aug 27, 2012
1,366
596
Ni moja ya maeneo ambayo katiba mpya inabidi iyaangalie kwa makini sana.Kamati izi kusema ukweli zimekuwa zikitumika visivyo.Kamati izi kwanza zimekuwa zinatumiwa na wajumbe au jamaa zao kuwaadhibu watu wanaotofautiana nao kwa namna moja au nyingine.Ukaa kama kamati kujadili watu mbali mbali ,bila ushahid wa dhati na mara nyingi kwa kusikiliza upande mmoja na kisha kutoa maamuzi mazito yakiwemo kufukuza watu kazi,kufukuza watu kwenye mkoa,kumfungia mtu biashara etc ili mradi ni maamuzi ya kukomoa komoa.Mara nyingi wajumbe wote ukianzia mkuu wa koa wanakuwa ni watu wasio na elimu ya haki za binadamu wala sheria na wengi wao hata upeo wa maisha ya kawaida na dunia inavyokwenda kwa sasa ni mdogo sana kwani wanasiasa wengi wa kizamani ni wavivu wa kusoma vitu vipya.Hivyo wanapokaa kamati izo zinakuwa za kiumbea umbea ,za kipwagu na pwaguzi lakini uhitimisha na maamuzi magumu yasiyo na legitimacy kisheria.Nampongeza sana raisi Kikwete kwani katika utawala wake amekuwa makini sana na muangalifu kutoa maamuzi kutokana na ushauri wa kamati hizi,tofauti na mtangulizi wake Ndugu Mkapa ambaye amevictmize watu wengi sana kwa kufuata mapendekezo ya kamati izi bila kuchukua taadhali esp kustaafisha watumishi etc
Ninaomba kwanza kwenye katiba mpya kiwepo kipengele cha kuonyesha kuwa kamati hizi zinapokaa kujadili fate ya mtu awepo mwanasheria wa serikali ,pia maamuzi wanayotoa yazingatie sheria za nchi ,pia maamuzi yanayohusu kustaafishwa mtu ajulishwe muhusika kabla ya kupeleke mapendekezo kwa raisi na apewe nafasi ya kuambatanisha defence yake kwa raisi.Na pia uwepo uwazi zaidi ili wale wanaosingiziwa na kamati hizi wawe na uwezo wa kushtaki na kudai fidia.Vinginevyo wenyeviti wa kamati hizi katika ngazi za wilaya na mkoa wamekuwa na tabia ya kujifanya miungu watu.
 
Back
Top Bottom