Kamati za Bunge na majukumu yake, muongozo wake na muundo wake

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
180
KAMATI ZA BUNGE: MUUNDO NA MAJUKUMU YAKE


MUUNDO WA KAMATI ZA BUNGE
Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 96, Bunge limepewa madaraka ya
kuunda Kamati za Bunge za aina mbalimbali na kwamba muundo wa
Kamati hizo umefafanuliwa na Kanuni za Kudumu za Bunge. Kwa
hiyo, kwa mujibu na Kanuni za Bunge, Kamati zifuatazo
zimebainishwa:
3.3.1 KAMATI ZA KUDUMU
3.3.1.1 Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 89 limeunda Kamati 15
zifuatazo:
(i) Kamati ya Uongozi;
(ii) Kamati ya Fedha na Uchumi;
(iii) Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
(iv) Kamati ya Hesabu za Serikali;
(v) Kamati ya Uwekezaji na Biashara;
(vi) Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje;
(vii) Kamati ya Kanuni za Bunge;
(viii) Kamati ya Ulinzi na Usalama;
(ix) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge;
(x) Kamati ya Huduma za Jamii;
(xi) Kamati ya Maliasili na Mazingira;
(xii) Kamati ya Maendeleo ya Jamii;
(xiii) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa;
(xiv) Kamati ya Kilimo na Ardhi;
(xv) Kamati ya Miundombinu.
3.3.2.1 Aidha, Kanuni 88(12) imetoa fursa kwa kila Kamati kuunda
Kamati Ndogo kwa ajili ya uendeshaji bora wa shughuli
zake.
6
3.3.2 KAMATI TEULE
Kamati Teule zimewekewa utaratibu wa kuundwa katika Kanuni ya 104. Kwa
mujibu wa Kanuni hii Kamati Teule itaundwa na Bunge kwa madhumuni
maalum, kwa hoja mahsusi itakayotolewa kwa ajili hiyo na kuafikiwa. Aidha,
Kamati Teule inaweza kuundwa kama Bunge litaamua kwamba hoja fulani
iliyojadiliwa ikafanyiwa kazi zaidi na Kamati Teule. Kamati Teule hukoma
mara imalizapo kufanya kazi iliyopangiwa na Bunge.
Katika vifungu vinavyofuata, mada hii itajihusisha zaidi na Kamati za
Kudumu. Kwa mantiki hii, basi vifungu vilivyotangulia vihesabiwe kama ni
vifungu vya kufungua macho tu na kuona jinsi Bunge lenyewe, Kamati na
Kanuni zake zivyopewa uzito Kikatiba.
4.0 MAJUKUMU YA MSINGI NA YA JUMLA YA KAMATI
4.1 Kwa mujibu wa mgawanyo wa Mamlaka kama ilivyoainishwa katika
vifungu vilivyotangulia, Bunge na Kamati zake za Kudumu hufanya
kazi za kusimamia Utendaji wa Serikali kwa niaba ya Wananchi.
Bunge na Kamati zake ndiyo darubini (Oversight or Watch-dog organ)
ya kuhakikisha kwamba mambo yote ya uendeshaji wa kazi za Dola
unafanywa kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni zilizowekwa.
Kwa hiyo, kuna majukumu ambayo hutekelezwa na Bunge lenyewe na
baadhi ya majukumu ambayo utekelezaji wake ni wa siku hadi siku
yanashughulikiwa na Kamati za Kudumu.
7
4.2 Kila Kamati ya Kudumu ma majukumu ya msingi na inalo jukumu la
jumla la kufuatilia utekelezaji wa Ahadi za Serikali zilizotolewa
Bungeni ambazo zinagusa mambo yaliyo katika Mamlaka ya Kamati
inayohusika. Aidha, Kamati inaweza kupendekeza kwa Spika
nyongeza ya majukumu ambayo yatajitokeza katika kutekeleza
majukumu ya msingi. Kwa upande mwingine, Spika anaweza
kukabidhi jambo lingine lolote kwa Kamati yoyote kama atakavyoona
inafaa, kwa ajili ya kushughulikiwa na Kamati hiyo, kwa mujibu wa
Kanuni za Kudumu za Bunge Kanuni ya 90(1) na (2).
5.0 AINA YA KAMATI NA KAZI ZAKE
5.1 AINA YA KAMATI
Kamati za Kudumu za Bunge ambazo ziko Kumi na Tano
(15) kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 3.3.1 zinaweza
kugawanyika katika makundi matatu (3):
(a) Kamati zenye Majukumu ya Msingi ya kushughulikia mambo ya
Ndani ya Bunge (Parliamentary Institutional Functions).
(b) Kamati zenye Majukumu ya Msingi ya Kusimamia Uendeshaji
wa Shughuli za Serikali (Oversight or Watch-dog Functions) au
Kamati zenye “Portfolio”.
(c) Kamati zenye Majukumu ya Msingi yanayohusu Maeneo
Maalum yanayogusa Uendeshaji wote wa Serikali (Specific
Oversight or Watch-dog Functions).
8
5.1.1 KAMATI ZENYE MAJUKUMU YA MSINGI YA
KUSHUGHULIKIA MAMBO YA NDANI YA BUNGE
(PARLIAMENTARY INSTITUTIONAL FUNCTIONS)
Ziko Kamati Tatu (3) zenye majukumu ya aina hii nazo ni:
(i) Kamati ya Uongozi
(1) Wajumbe wake ni:
(a) Spika, ambaye ndiye Mwenyekiti,
(b) Naibu Spika
(c) Kiongozi wa shughuli za Serikali
Bungeni au Mwakilishi wake;
(d) Kiongozi wa Upinzani Bungeni au
Mwakilishi wake;
(e) Wenyeviti wa Kamati za Kudumu;
(f) Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(2). Katibu
Katibu wa Bunge ndiye Katibu wa Kamati
(3) Majukumu ya Kamati
Majukumu ya Kamati ya Uongozi ni kufikiria na kumshauri
Spika kuhusu mambo yote yanayohusu shughuli za Bunge
kwa jumla; ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu
utakaorahisisha maendeleo ya shughuli za Bunge au za
Kamati yake yoyote endapo itatokea haja ya kufanya hivyo.
9
(ii) Kamati ya Kanuni za Bunqe
(1) Wajumbe wa Kamati wanateuliwa na Spika na Mwenyekiti
wake ni Spika na Naibu Mwenyekiti ni Naibu Spika.
(2) Katibu huteuliwa na Ofisi ya Spika
(3) Majukumu ya Kamati
(a) Kufikiria na kutoa mapendekezo juu ya kufanya
mabadiliko katika Kanuni za Bunge.
(b) Kuchunguza na kutoa taarifa juu ya pendekezo
lolote linalohusu Kanuni za Bunge ambalo
limepelekwa kwenye Kamati hiyo na Spika au
na Mbunge yeyote.
(c) Kuchunguza na kutoa taarifa juu ya lalamiko lolote
kuhusu uamuzi wa Spika ambalo limepelekwa
kwake na Mbunge yeyote.
(iii) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
(1) Wajumbe wake huteuliwa na Spika.
(2) Katibu huteuliwa na Ofisi ya Spika.
(3) Majukumu ya Kamati;
(a) Kuchuguza masuala yote yahusiyo Haki,
Kinga na
10
Madaraka ya Bunge yanayopelekwa kwake na
Spika;
(b) Kushughulikia mambo yanayohusu Maadili ya
Wabunge;
(c) Kufikiria jambo lingine lolote litakalopelewa
kwake na Spika
5.1.2 KAMATI ZENYE MAJUKUMU YA MSINGI YA
KUSHUGHULIKIA UENDESHAJI WA SERIKALI
(OVERSIGHT OR WATCH-DOG FUNCTIONS) AU
KAMATI ZENYE “PORTFOLIO”
Ziko Kamati Kumi (10) katika aina hii ya Kamati kama
ifuatavyo:
(i) Kamati ya Fedha na Uchumi
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Fedha;
(b) Wizara ya Mipango, Uchumi na
Uwezeshaji.
(ii) Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii,
UTUMISHI na Utawala Bora);
(b) Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano);
11
(c) Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Bunge, Maafa na Kampeni
Dhidi ya UKIMWI).
(d) Wizara ya Katiba na Sheria.
(iii) Kamati ya Uwekezaji na Biashara
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko;
(b) Wizara ya Nishati na Madini.
(iv) Kamati ya Mambo ya Nchi za Nje
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
(b) Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
(v) Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;
(b) Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi;
(c) Wizara ya Usalama wa Raia.
12
(vi) Kamati ya Huduma za Jamii
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii;
(b) Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya
Juu;
(c )Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
(vii) Kamati ya Mahasili na Mazinqira
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira);
(b) Wizara ya Maliasili na Utalii.
(viii) Kamati va Maendeleo ya Jamii
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto;
(b) Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya
Vijana;
(c) Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
(ix) Kamati ya Kilimo na Ardhi
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
(a) Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi;
(b) Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika;
13
(c) Wizara ya Maji;
(d) Wizara ya Maendeleo ya Mifugo.
(x) Kamati ya Miundombinu.
Kamati hii hushughulikia Wizara hizi:
Wizara ya Miundombinu (Ujenzi,Mawasiliano
na Uchukuzi).
5.1.2 KAMATI ZENYE MAJUKUMU YA MSINGI
YANAYOHUSU MAENEO MAALUMU
YANAYOGUSA UENDESHAJI WOTE WA
SERIKALI (SPECIFIC OVERSIGHT OR WATCH-DOG
FUNCTIONS)
Kamati zinazohusika na aina hii ya majukumu ni hizi:
(i) Kamati ya Hesabu za Serikali
Kamati hii ina majukumu yafuatayo.
(a) Kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu
yaliyoainishwa katika Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Serikali kuhusu Serikali Kuu.
(b) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyokwisha
kutolewa na Kamati hiyo ya kuondoa matatizo husika, ili
yasionekane tena katika Taarifa zitakazofuata.
14
(ii) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa
Kamati hii ina majukumu yafuatayo:
(a) Kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu
yaliyoainishwa katika Taarifa ya Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Serikali kuhusu Serikali za
Mitaa.
(b) Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo
yaliyokwisha kutolewa na Kamati hiyo ya kuondoa
matatizo husika, ili yasionekane tena katika Taarifa
zitakazofuata.
5.2 MAJUKUMU YA MSINGI YA KAMATI
Majukumu ya Msingi ya kila Kamati ya Kudumu ya Bunge yameorodheshwa
kwenye Kanuni za Kudumu za Bunge kuanzia Kanuni ya 91 hadi 103B.
5.2.1 Kamati tano (5) zifuatazo:
(i) Kamati ya Uongozi (Kanuni 91);
(ü) Kamati ya Kanuni za Bunge (Kanuni 97);
(iii) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge (Kanuni 99);
(iv) Kamati ya Hesabu za Serikali (Kanuni 94);
(v) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Kanuni 103).
Majukumu yake yameelezwa katika Vifungu 5.1.1 na
5.1.3 vilivyotangulia
15
5.2.2 Kamati nyingine Kumi (10) zenye Majukumu ya Kusimamia
Uendeshaji wa Serikali (Oversight or Watch—dog Functions) au
Kamati zenye “Portfolio”, majukumu yake ya msingi na ya jumla ni
haya yafuatayo:
(i) Kushughulikia Bajeti za Wizara zilizowekwa chini ya kila Kamati;
(ii) Kushughulikia mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya kila mwaka;
(iii) Kushughulikia Miswada ya Sheria na Mikataba inayopendekezwa
kuridhiwa na Bunge ambayo chanzo chake ni Wizara hizo;
(iv) Kushughulikia Taarifa za kila mwaka za Utendaji na
Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya Umma yaliyo
chini ya Wizara zilizowekwa chini ya kila Kamati;
(v) Kufuatilia utekelezaji unaofanywa na Wizara hizo za kila Kamati kwa
mujibu wa Ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, na kama ilivyonukuliwa katika Kifungu 2.0 cha Mada hii.
5.2.3 UONGOZI WA KAMATI
Kila Kamati huongozwa na Mwenyekiti na kama hayupo, Makamu
Mwenyekiti ambaye huchaguliwa kutokana na Wajumbe wa kila
Kamati, isipokuwa tu kwa Kamati ya Uongozi na Kamati ya Kanuni za
16
Bunge kama ilivyokwisha elezwa ambazo Mwenyekiti wake ni Spika.
Aidha, Mawaziri hawawi Wajumbe wa Kamati isipokuwa tu kwenye
Kamati ya Uongozi ambayo Kiongozi wa Shughuli za Serikali
Bungeni au Mwakilishi wake huwa Mjumbe.
5.2.4 WAJUMBE WA KAMATI
• Kwa mujibu wa Kanuni 87, Spika huteua Wabunge kuingia katika
Kamati isipokuwa Kamati ya Uongozi ambayo Wajumbe wake ni
Wenyeviti wa Kamati za Kudumu.
• Kwa upande mwingine, Mbunge mmoja mmoja anaweza kuteuliwa
kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge zaidi ya kuwa kwenye zile Kamati nyingine kumi
na mbili.
5.2.5 UHAI WA KAMATI ZA KUDUMU
Uhai wa Kamati za Bunge na Wajumbe wake umeelezwa waziwazi katika
Kanuni 87(4) kama ninavyonukuu hapa chini:
“(4) Wabunge walioteuliwa watashika nafasi zao kama Wajumbe wa
Kamati zao kwa muda ambao wataendelea kuwa Wabunge (bila kuwa
Waziri au Spika) mpaka mwisho wa Mkutano unaofuatia mara baada
ya Mkutano wa Kumi wa Bunge (ambao ndio hukamilisha nusu ya
kwanza ya maisha ya Bunge) utakaofanywa baada ya kuteuliwa kwao,
lakini waweza kuteuliwa tena kwenye Kamati hizo katika kipindi cha
pili kilichobaki cha maisha ya Bunge la kipindi kinachohusika”.
17
6.0 UTARATIBU WA KUFANYA KAZI ZA KAMATI
Kama ilivyoelezwa kwenye vifungu vilivyotangulia, Kamati zina kazi nyingi
ambazo hapana budi zitengenezwe utaratibu mzuri wa kuzitekeleza. Kwa
hiyo, kila Kamati inawajibika kuwa na Ratiba ya Kazi ambayo imepata
mwafaka wa Wajumbe wa Kamati.
6.1 RATIBA YA KAZI
Ratiba ya Kazi za Kamati ina sehemu mbili zifuatazo:
6.1.1 KAZI ZINAZOPANGIWA KAMATI NA SPIKA
Kazi zinazopangiwa Kamati na Spika ndizo hupewa
kipaumbele ili Ratiba ya Bunge lenyewe itekelezwe bila
matatizo. Na kwa utaratibu ulivyo, Mikutano ya Bunge ya
mwaka mzima inafahamika na Kalenda ya mwaka mzima
hutolewa ambayo inatakiwa kuzingatiwa na kila Kamati wakati
wa kupanga kazi zake.
6.1.2 KAZI ZINAZOPANGWA NA KAMATI
Kila Kamati ina wajibu wa kupanga Ratiba yake ambayo
inazingatia Ratiba ya Bunge lenyewe na kutoa nafasi ya
kwanza kwa kazi ambazo zinatakiwa kutolewa Taarifa Bungeni
na kwa muda uliowekwa na Spika. Kazi nyingine ni zile
ambazo zinafanyika wakati Bunge limeahirishwa lakini
zinazingatia siku 60 zilizotengwa kwa kazi za Kamati kila
18
mwaka. Na kwa mujibu wa utaratibu, siku 15 zimetengwa kwa
kazi za Kamati kabla ya kila Mkutano wa Bunge na hufanyikia
Jijini Dar es Salaam au Dodoma kwa jinsi Spika
atakavyoelekeza.
6.2 MBINU ZA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA KAMATI
Kila Kamati inatakiwa kujiwekea utaratibu mzuri wa kutekeleza kazi
zake. Mbinu mbalimbali hutumika kama ifuatavyo:
6.2.1 Kufanya kazi kwa kutumia Mikutano ya Kamati nzima au Kamati
Ndogo.
6.2.2 Kutembelea maeneo ya uendeshaji wa kazi za Serikali ili kupata
uelewa zaidi wa hali ya utekelezaji wa majukumu ya Serikali.
6.2.3 Kuandaa Semina ambapo Wataalam wa fani mbalimbali hutoa Mada
za kuongeza uelewa na elimu ya Wajumbe kuhusu maeneo mbalimbali
ya shughuli za uendeshaji wa Serikali, Taasisi na Asasi zake.
6.2.4 Kufanya Mikutano na Wadau (Public Hearing) mbalimbali ili kupata
michango au maoni yao kuhusu masuala mbalimbali na hasa kwenye
baadhi ya Miswada ambayo inatazamiwa kuwasilishwa Bungeni na
inagusa maisha ya Wananchi wengi.
19
6.3 BAJETI
Shughuli za Kamati hufanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Kamati ya kila
mwaka. Ila uzoefu umeonyesha kwamba Semina mbalimbali zinaweza kwa
kuafikiana, kugharamiwa na Wizara au Taasisi hapa Nchini na za Kimataifa
7.0 TAARIFA ZA KAZI ZA KAMATI
7.1 Kila Kamati inawajibika kuwasilisha Taarifa za kazi ambazo
imepangiwa na Spika au kazi zake za msingi katika wakati
zinaotakiwa. Na kila mwisho wa mwaka kila Kamati inatakiwa
kuandaa Taarifa ya mwaka ya kazi zake na kuiwasilisha Bungeni kama
Spika atakavyoelekeza
7.2 Wakati wa kuwasilisha Taarifa Bungeni, Mwenyekiti kwa kuafikiana
na Wajumbe anaweza kutoa nafasi kwa Wajumbe wa Kamati
kuwasilisha Taarifa hizo kwa niaba yake. Ila Mwenyekiti anachukua
jukumu la kuwajibika kwa yale yatakayotolewa kwa niaba yake.
7.3 Utaratibu huu wa kuwashirikisha Wajumbe pia unatumika kwenye
kuongoza Vikao vya Kamati hasa vile vya kushughulikia Hesabu
zilizokaguliwa za Mashirika chini ya “Portifolio” ya Kamati. Utaratibu
huu ni mzuri kwa kuwa Mashirika ni mengi na kwa siku Kamati
inaweza kushughulikia Mashirika hadi matatu.
Utaratibu wa kuwashirikisha Wajumbe wa Kamati katika kuongoza
Vikao unajenga mshikamano wa dhati na uzoefu katika kazi za
Kamati.
20
8.0 HUDUMA KWA KAMATI
Ofisi ya Bunge inao utaratibu mahsusi wa kuhudumia Kamati za Bunge kwa
kuzipatia Makatibu wa Kamati, huduma za kuchapa Taarifa na Usafiri kama
Kamati itapanga kufanya kazi mahali ambapo usafiri unahitajika n.k.
9.0 HITIMISHO
9.1 Mada hii imejaribu kutoa maelezo kuhusu Kamati za Bunge
(Parliamentary Committees) Muundo wake, Majukumu yake na jinsi
zinavyofanya kazi zake za kusimamia uendeshaji wa shughuli za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Bunge.
Vilivyo, Kamati za Bunge hapana budi zitekeleze kazi zake kwa niaba
ya Bunge kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
pamoja na Kanuni za Kudumu za Bunge. Kwa mantiki hii kila Mbunge
anahitajika kujizoesha kusoma Katiba na Kanuni za Bunge ili ajipatie
uelewa wa kina wa nyenzo hizi zinazoongoza kazi za Bunge na Kamati
zake.
9.2 Mada hii pia imegusia uzoefu wa aina mbalimbali ambao kama
utatumika basi utaimarisha na kuongeza ufanisi wa utendaji wa
Kamati za Kudumu za Bunge.
 
Nakushukuru sana kamanda nimeelewa nin nini CUF wanalilia kweli KAMATI ZA BUNGE NI MUHIMU SANA
 
Anayeunda na kuvunja hizi kamati ni Bunge kwa ujumla au ni spika peke yake?
 
Back
Top Bottom