Kamati ya Wazee wa Wanafunzi waliofutiwa matokeo, Zanzibar.

mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
185
Kamati ya wazee
haikubaliani na uamuzi
wa kuwafutia matokeo
wanafunzi wale tu
walioshutumiwa
kufanya udanganyifu bali kuwafutia wote
kwa kuwa mitihani
ulivuja. Kufuatia hoja
hizo za msingi Baraza
halina budi kukubali
kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, na Baraza
litapungukiwa na
ubebaji wa lawama
kwa kuondoa dhana hii
ya kuvuja kwa mitihani
kwa kurejewa kuliko kubakia katika
kung’ang’ania
kutorejewa na kuanza
kuibua msuguano
mwengine wa mvutano
kati ya Zanzibar na Tanzania Bara katika
suala la elimu na
hatimae kuweza
kuhatarisha Muungano. KAMATI YA WAZEE WA WANAFUNZI WALIOFUTIWA MATOKEO, ZANZIBAR. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE) ILIYOTOLEWA TAREHE 21-02-2012. TAMKO LA WAZEE WA WANAFUNZI WALIOFUTIWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2011. Elimu ni suala muhimu katika maisha ya mtu na maendeleo ya taifa kwa jumla. Suala la kufanyiwa mitihani katika elimu ni muhimu na lina uzito wa kipekee
kwa vile ndio kipimo cha uwezo wa mwanafunzi juu ya uwelewa kwa alichokisoma. Kwa kuanzia mitihani ya kidato cha nne mwanafunzi
huandaliwa kuendelea kidato cha tano na sita hadi chuo kikuu baada ya kufaulu mitihani iliyopangwa kulingana na mfumo wa elimu wa Tanzania. Ni imani yetu kwamba kila kitu kina utaratibu wake, na panapo kiukwa utaratibu basi sheria huchukua mkondo wake, pia kwa utaratibu unaokubalika. Na ikitokea hukumu ambayo haikufuata sheria wala utaratibu, pia sheria hio hio huchukua nafasi yake. Kwa kulizingatia hili Tanzania inayo sheria ya mitihani katika kila ngazi ya elimu ikiwemo kidato cha nne. Wanafunzi waliofanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011 ambapo matokeo yamekuja mwaka 2012, baadhi yao wamefutiwa matokeo, bila ya kua na ushahidi bali ni shutma jambo ambalo haliwezi kuhalalisha uamuzi huo. Kwa kuzingatia maamuzi hayo ya Baraza la Mitihani la Tanzania kuwafutia matokeo wanafunzi hao, wazee tumeona ni busara zaidi kuja na madai ambayo yanaweza kubainisha ukweli dhidi ya maamuzi hayo. 1). ADHABU ILIYOTOLEWA NA BARAZA LA MITIHANI. Baraza la Mitihani Tanzania limefanya uamuzi wa kuwafutia matokeo wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne bila ya kuwa na ushahidi. Katika elimu suala la kufanana majawabu si suala la kushangaza ukizingatia mwalimu ni mmoja, na wamesomeshwa kitu kimoja na swali lilikuwa
linahitaji jawabu moja. Hivyo, hoja hii haina nguvu kwa kuzingatia mfumo na utaratibu wa utoaji elimu katika nchi yetu. Suala la kuwadhibu wanafunzi miaka 3 kutofanya mtihani ni hukumu ya mauwaji katika elimu. Kamati ya wazee haikubaliani na adhabu hio. Tukizingatia vijana hawa ndio tunaowatarajia kuwa viongozi na wasomi wa taifa hili baadae, ni vipi tutaweza kuwarudisha katika taaluma baada ya kutumikia adhabu ya miaka mitatu? Jawabu rahisi ni haiwezekani. Lakini jambo la msingi ni kuwa makosa ni ya aina tatu kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, cha kushangaza makosa hayo yametolewa adhabu moja. Hii inamaana aliyeandika Bongo Fleva na kuchora picha (katuni) hakukopia ila hajaandika jawabu sahihi, makosa hayo yangepelekea kufeli kwa somo hilo tu na si kumfutia masomo yote seuze kuhalalisha adhabu ya miaka mitatu. Adhabu ya kuwafuatia matokeo tu pekee tayari ni adhabu tosha, na ni somo kwa wanafunzi waliofutiwa, waliokuwa
hawajafutiwa, na hata wanaofuatia na hatimae mitihani kurejewa tena, hii itakuwa ni busara kubwa zaidi, Baraza likizingatia athari kwa taifa. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, wanafunzi wamefutiwa
matokeo kwa sababu tofauti, ikiwemo kukopia na kufanana jawabu, kuwa na muandiko tofauti katika mtihani mmoja, kuandika Bongo Fleva na kuandika matusi. Lakini Katibu ameshindwa kutueleza ni wanafunzi wa skuli gani waliyofanya makosa hayo, je ni wa Zanzibar au Tanganyika? Sababu nyengine ni kukosekana kwa baadhi ya vijitabu vya jawabu, je hili ni kosa la mwanafunzi au watendaji wa Baraza? Iweje ahukumiwe mwanafunzi peke yake? Pamoja na kuwa Baraza limetumia kanuni ya 6 (1) na (2) lakini limewacha kipengele cha (3). 2). TAKWIMU SAHIHI ZA WALIOFUTIWA MATOKEO. Katika maelezo ya Katibu juu ya suala la idadi ya waliofutiwa matokeo kwa upande wa Zanzibar imekosekana hadi sasa kwa kulingana na makosa yao. Alichokifanya katibu ni mjumuisho wa makosa ambayo nao amekosa ushahidi wa kutegemea. Ushahidi ambao ameutumia ni wa kimazingira ambao hauna nguvu katika kufanya maamuzi kwa kesi hii, hivyo ameshutumu ndipo akahukumu jambo ambalo si sahihi. Kufuatia utaratibu wa ufanyaji mitihani, kila kituo kinakua na wasimamizi wa mitihani na mkuu wa kituo, ambaye anatakiwa kuandika ripoti juu ya tokeo hilo, lakini Katibu ameshindwa
kuutanabahisha umma ni ripoti gani aliyotumia kuthibitisha ukopiaji na upoteaji wa karatasi za majibu hadi kufika kutoa hukumu ya kumfutia mwanafunzi matokeo. 3). KUVUJA KWA MITIHANI. Kuvuja kwa mitihani si suala geni kwa Tanzania. Ikumbukwe mwaka 1996 mitihani hio hio ya kidata cha nne ilivuja na kulazimisha mitihani hio kurejewa, hakufutiwa matokeo mwanafunzi wa Tanzania Bara wala wa Zanzibar. Mh. Katibu katika maelezo yake alipoambiwa mitihani imevuja alikana, lakini kwa hakika katika nafsi yake anakubali kuwa mitihani ilivuja. Ushahidi upo juu ya suala la kuvuja kwa mitihani mwaka 2011. Kwanza kabisa, Katibu mwenyewe aliionesha shati iliyo na majibu ya mtihani. Hebu na tujiulize vipi mwanafunzi aandike majibu ya mtihani katika shati kabla ya mtihani bila ya kujua litakaloulizwa? Ni wazi kuwa alikwishapata mtihani ndipo akaingia na jawabu. Pia, Katibu Mtendaji wa Baraza amedai kuwa baaadhi ya watahiniwa waliopo mashulini wamefanana majibu na watahiniwa wa faragha/ wakujitegemea, hebu na tujiulize ni kwa vipi wanafunzi hawa wafanane majibu ukizingatia, wamo katika vyumba tofauti vya mitihani, pia walikua masafa marefu baina ya chumba na chumba. Hapo inaonyesha wazi kuwa mtihani ulipatikana kabla, na hivyo kuhalalisha dai la kuvuja
mtihani huo. Hivyo, haya yote yanaonyesha wazi kuwa mitihani ilivuja, jambo ambalo linaonekana wazi lilitokea kwanza Bara. Katibu Mtendaji mama Joice Ndalichako anapinga hili kwa kuhofia kuwajibika yeye na watendaji wengine wa Baraza, na badala yake kumpiga ng’ombe wa nyuma wakati aliyefanya kosa ni ng’ombe wa mbele. Hii inaonyesha wazi jinsi Baraza linavyohofia
ukali wa sheria na. 21 ya 1973 kifungu cha 23 i a. 4). UZEMBE NA MAPUNGUFU YALIOONEKANA KWA BARAZA LA MITIHANI. Uwezo na Maendeleo ya mwanafunzi
hayapimwi tu na mtihani wa mwisho pekee bali pia kwa matokeo ya mitihani ya ndani ya skuli. Dalili na ushahidi unaonyesha kuwa wanafunzi ambao
wana uwezo mkubwa katika ufahamu na ufanyaji wa mitihani ndio pia waliofutiwa matokeo na wale wenye uwezo mdogo wamepewa matokeo yao. Hili linatupa mashaka juu ya utendaji na uadilifu wa Baraza la Mitihani. Pia kuna wanafunzi wameandikiwa
“Absent” kwa maana hawakufanya mtihani, lakini kiukweli wanafunzi hawa walifanya mtihani. Hilo pia nalo linapelekea kutokuwa na imani na Baraza la mitihani juu ya hukumu ya kuwafutia wanafunzi matokeo. Pia ni ushahidi kuwa Baraza limekosa umakini katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa upande mwengine, baya zaidi ambalo limezidi kutujenga Wazanzibari kupoteza imani na Baraza la Mitihani la Tanzania ni kuwa Baraza limetoa matokeo kwa baadhi ya wanafunzi ambao tayari washafutiwa matokeo, kwa nini iwe kwao wao tu, au wao wamebainika baadae kuwa hawajafanya udanganyifu? Au kwa sababu wao hawakufaulu ni Divisheni IV na ‘O’? Ipo haja kwa watendaji wa Baraza hasa Katibu Mtendaji kufikiria tena kwa umakini juu ya utendaji na uamuzi wa Baraza kufuta matokeo. HITIMISHO: Kamati ya wazee haikubaliani na uamuzi wa kuwafutia matokeo wanafunzi wale tu walioshutumiwa
kufanya udanganyifu bali kuwafutia wote kwa kuwa mitihani ulivuja. Kufuatia hoja hizo za msingi Baraza halina budi kukubali kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, na Baraza litapungukiwa na ubebaji wa lawama kwa kuondoa dhana hii ya kuvuja kwa mitihani kwa kurejewa kuliko kubakia katika kung’ang’ania
kutorejewa na kuanza kuibua msuguano mwengine wa mvutano kati ya Zanzibar na Tanzania Bara katika suala la elimu na hatimae kuweza kuhatarisha Muungano. Mbali na suluhisho la kurejewa kwa mitihani, kwa upande mwengine ipo haja ya vyombo husika vya Wizara ya Elimu visimame imara na kufanya uchunguzi wa kina wa matokeo haya na wahusika wote wa tokeo hili bila ya kuwaonea haya watakapobainika
wawajibishwe kwa kadhia hii mara moja, huku wizara husika zikifikiria
kuwabadilisha baadhi ya watendaji wake kutokana na kadhia hii ya kuvuja kwa mitihani kila mara. Hili ni la msingi kufanyika kwa kuzingatia dhana nzima ya utawala bora ambapo Tanzania inajisifia. Wakati huo huo Kamati inaunga mkono jitihada za Jumuiya ya DCPM kwa utafiti wa kisheria juu ya kadhia hii. Kamati ya wazee pia, inatowa tamko iwapo Baraza litaona kuna ugumu wa kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, jambo ambalo kwa hakika linawezekana pale ambapo kuna adhma njema, basi pia Baraza libainishe kwa walimu wao makosa ya kila mwanafunzi kwa wale waliofutiwa na wale wenye mashaka na matokeo yao. Mwisho, kamati ya wazee pia ina mashaka juu ya matokeo ya Tanzania Bara kwamba itakuaje skuli za aina Fulani tu iwe asilimia kubwa ya wanafunzi wake wawe ndio miaka yote wanaopata alama za ‘A’ kwa wingi (maana ya Division ya kwanza), na ndio skuli bora mara zote Tanzania, je Baraza la Mitihani hili halikupeni mashaka? Au hao ndio wenye uwezo peke yao? Ahsanteni, Naomba kuwasilisha, Katibu wa Kamati ya Wazazi, Saleh Mohammed Saleh.
 
dini bila elimu ni mzigo mzito! Hivi hawa wazee . . . . . . . ! Ewe Ndalichako nakuamini sana na hutoteteleka
 
Thinking disorder is what these wazee are suffering from

kazi kweli kweli. it is more than thinking disorders. Ili mradi wame :lol: ila iko kazi, nilifikiri wazee wanaweza kukaa na kutumia experience ya waliyoaona maishani wakadraw conlusion from their experiences, wakasaidia vijana. lakini hapa mhm :photo: I am now getting confused
A%20S%20embarassed.gif
 
2011 are real cause for concern. Compare the results with kcse results released yesterday. A total of 411.783 sat for kcse exam. 119.650 scored mean c+ and above hence eligible for university. 292.321 scored D+ and above hence eligible for absorption to middle level college.
 
Hao wazee wapewe kwanza mtihani mmoja wa NECTA kupima uwezo wao kama wanaqualify kutoa matamko
 
2011 are real cause for concern. Compare the results with kcse results released yesterday. A total of 411.783 sat for kcse exam. 119.650 scored mean c+ and above hence eligible for university. 292.321 scored D+ and above hence eligible for absorption to middle level college.

ipo kazi kama mtu namaliza F4 then yuko eligible kuingia university. Sioni sababu ya kujenga hoja nawe...sorry its simplemind
 
Kamati ya wazee
haikubaliani na uamuzi
wa kuwafutia matokeo
wanafunzi wale tu
walioshutumiwa
kufanya udanganyifu bali kuwafutia wote
kwa kuwa mitihani
ulivuja. Kufuatia hoja
hizo za msingi Baraza
halina budi kukubali
kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, na Baraza
litapungukiwa na
ubebaji wa lawama
kwa kuondoa dhana hii
ya kuvuja kwa mitihani
kwa kurejewa kuliko kubakia katika
kung'ang'ania
kutorejewa na kuanza
kuibua msuguano
mwengine wa mvutano
kati ya Zanzibar na Tanzania Bara katika
suala la elimu na
hatimae kuweza
kuhatarisha Muungano. KAMATI YA WAZEE WA WANAFUNZI WALIOFUTIWA MATOKEO, ZANZIBAR. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE) ILIYOTOLEWA TAREHE 21-02-2012. TAMKO LA WAZEE WA WANAFUNZI WALIOFUTIWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2011. Elimu ni suala muhimu katika maisha ya mtu na maendeleo ya taifa kwa jumla. Suala la kufanyiwa mitihani katika elimu ni muhimu na lina uzito wa kipekee
kwa vile ndio kipimo cha uwezo wa mwanafunzi juu ya uwelewa kwa alichokisoma. Kwa kuanzia mitihani ya kidato cha nne mwanafunzi
huandaliwa kuendelea kidato cha tano na sita hadi chuo kikuu baada ya kufaulu mitihani iliyopangwa kulingana na mfumo wa elimu wa Tanzania. Ni imani yetu kwamba kila kitu kina utaratibu wake, na panapo kiukwa utaratibu basi sheria huchukua mkondo wake, pia kwa utaratibu unaokubalika. Na ikitokea hukumu ambayo haikufuata sheria wala utaratibu, pia sheria hio hio huchukua nafasi yake. Kwa kulizingatia hili Tanzania inayo sheria ya mitihani katika kila ngazi ya elimu ikiwemo kidato cha nne. Wanafunzi waliofanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011 ambapo matokeo yamekuja mwaka 2012, baadhi yao wamefutiwa matokeo, bila ya kua na ushahidi bali ni shutma jambo ambalo haliwezi kuhalalisha uamuzi huo. Kwa kuzingatia maamuzi hayo ya Baraza la Mitihani la Tanzania kuwafutia matokeo wanafunzi hao, wazee tumeona ni busara zaidi kuja na madai ambayo yanaweza kubainisha ukweli dhidi ya maamuzi hayo. 1). ADHABU ILIYOTOLEWA NA BARAZA LA MITIHANI. Baraza la Mitihani Tanzania limefanya uamuzi wa kuwafutia matokeo wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne bila ya kuwa na ushahidi. Katika elimu suala la kufanana majawabu si suala la kushangaza ukizingatia mwalimu ni mmoja, na wamesomeshwa kitu kimoja na swali lilikuwa
linahitaji jawabu moja. Hivyo, hoja hii haina nguvu kwa kuzingatia mfumo na utaratibu wa utoaji elimu katika nchi yetu. Suala la kuwadhibu wanafunzi miaka 3 kutofanya mtihani ni hukumu ya mauwaji katika elimu. Kamati ya wazee haikubaliani na adhabu hio. Tukizingatia vijana hawa ndio tunaowatarajia kuwa viongozi na wasomi wa taifa hili baadae, ni vipi tutaweza kuwarudisha katika taaluma baada ya kutumikia adhabu ya miaka mitatu? Jawabu rahisi ni haiwezekani. Lakini jambo la msingi ni kuwa makosa ni ya aina tatu kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, cha kushangaza makosa hayo yametolewa adhabu moja. Hii inamaana aliyeandika Bongo Fleva na kuchora picha (katuni) hakukopia ila hajaandika jawabu sahihi, makosa hayo yangepelekea kufeli kwa somo hilo tu na si kumfutia masomo yote seuze kuhalalisha adhabu ya miaka mitatu. Adhabu ya kuwafuatia matokeo tu pekee tayari ni adhabu tosha, na ni somo kwa wanafunzi waliofutiwa, waliokuwa
hawajafutiwa, na hata wanaofuatia na hatimae mitihani kurejewa tena, hii itakuwa ni busara kubwa zaidi, Baraza likizingatia athari kwa taifa. Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, wanafunzi wamefutiwa
matokeo kwa sababu tofauti, ikiwemo kukopia na kufanana jawabu, kuwa na muandiko tofauti katika mtihani mmoja, kuandika Bongo Fleva na kuandika matusi. Lakini Katibu ameshindwa kutueleza ni wanafunzi wa skuli gani waliyofanya makosa hayo, je ni wa Zanzibar au Tanganyika? Sababu nyengine ni kukosekana kwa baadhi ya vijitabu vya jawabu, je hili ni kosa la mwanafunzi au watendaji wa Baraza? Iweje ahukumiwe mwanafunzi peke yake? Pamoja na kuwa Baraza limetumia kanuni ya 6 (1) na (2) lakini limewacha kipengele cha (3). 2). TAKWIMU SAHIHI ZA WALIOFUTIWA MATOKEO. Katika maelezo ya Katibu juu ya suala la idadi ya waliofutiwa matokeo kwa upande wa Zanzibar imekosekana hadi sasa kwa kulingana na makosa yao. Alichokifanya katibu ni mjumuisho wa makosa ambayo nao amekosa ushahidi wa kutegemea. Ushahidi ambao ameutumia ni wa kimazingira ambao hauna nguvu katika kufanya maamuzi kwa kesi hii, hivyo ameshutumu ndipo akahukumu jambo ambalo si sahihi. Kufuatia utaratibu wa ufanyaji mitihani, kila kituo kinakua na wasimamizi wa mitihani na mkuu wa kituo, ambaye anatakiwa kuandika ripoti juu ya tokeo hilo, lakini Katibu ameshindwa
kuutanabahisha umma ni ripoti gani aliyotumia kuthibitisha ukopiaji na upoteaji wa karatasi za majibu hadi kufika kutoa hukumu ya kumfutia mwanafunzi matokeo. 3). KUVUJA KWA MITIHANI. Kuvuja kwa mitihani si suala geni kwa Tanzania. Ikumbukwe mwaka 1996 mitihani hio hio ya kidata cha nne ilivuja na kulazimisha mitihani hio kurejewa, hakufutiwa matokeo mwanafunzi wa Tanzania Bara wala wa Zanzibar. Mh. Katibu katika maelezo yake alipoambiwa mitihani imevuja alikana, lakini kwa hakika katika nafsi yake anakubali kuwa mitihani ilivuja. Ushahidi upo juu ya suala la kuvuja kwa mitihani mwaka 2011. Kwanza kabisa, Katibu mwenyewe aliionesha shati iliyo na majibu ya mtihani. Hebu na tujiulize vipi mwanafunzi aandike majibu ya mtihani katika shati kabla ya mtihani bila ya kujua litakaloulizwa? Ni wazi kuwa alikwishapata mtihani ndipo akaingia na jawabu. Pia, Katibu Mtendaji wa Baraza amedai kuwa baaadhi ya watahiniwa waliopo mashulini wamefanana majibu na watahiniwa wa faragha/ wakujitegemea, hebu na tujiulize ni kwa vipi wanafunzi hawa wafanane majibu ukizingatia, wamo katika vyumba tofauti vya mitihani, pia walikua masafa marefu baina ya chumba na chumba. Hapo inaonyesha wazi kuwa mtihani ulipatikana kabla, na hivyo kuhalalisha dai la kuvuja
mtihani huo. Hivyo, haya yote yanaonyesha wazi kuwa mitihani ilivuja, jambo ambalo linaonekana wazi lilitokea kwanza Bara. Katibu Mtendaji mama Joice Ndalichako anapinga hili kwa kuhofia kuwajibika yeye na watendaji wengine wa Baraza, na badala yake kumpiga ng'ombe wa nyuma wakati aliyefanya kosa ni ng'ombe wa mbele. Hii inaonyesha wazi jinsi Baraza linavyohofia
ukali wa sheria na. 21 ya 1973 kifungu cha 23 i a. 4). UZEMBE NA MAPUNGUFU YALIOONEKANA KWA BARAZA LA MITIHANI. Uwezo na Maendeleo ya mwanafunzi
hayapimwi tu na mtihani wa mwisho pekee bali pia kwa matokeo ya mitihani ya ndani ya skuli. Dalili na ushahidi unaonyesha kuwa wanafunzi ambao
wana uwezo mkubwa katika ufahamu na ufanyaji wa mitihani ndio pia waliofutiwa matokeo na wale wenye uwezo mdogo wamepewa matokeo yao. Hili linatupa mashaka juu ya utendaji na uadilifu wa Baraza la Mitihani. Pia kuna wanafunzi wameandikiwa
"Absent" kwa maana hawakufanya mtihani, lakini kiukweli wanafunzi hawa walifanya mtihani. Hilo pia nalo linapelekea kutokuwa na imani na Baraza la mitihani juu ya hukumu ya kuwafutia wanafunzi matokeo. Pia ni ushahidi kuwa Baraza limekosa umakini katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa upande mwengine, baya zaidi ambalo limezidi kutujenga Wazanzibari kupoteza imani na Baraza la Mitihani la Tanzania ni kuwa Baraza limetoa matokeo kwa baadhi ya wanafunzi ambao tayari washafutiwa matokeo, kwa nini iwe kwao wao tu, au wao wamebainika baadae kuwa hawajafanya udanganyifu? Au kwa sababu wao hawakufaulu ni Divisheni IV na ‘O'? Ipo haja kwa watendaji wa Baraza hasa Katibu Mtendaji kufikiria tena kwa umakini juu ya utendaji na uamuzi wa Baraza kufuta matokeo. HITIMISHO: Kamati ya wazee haikubaliani na uamuzi wa kuwafutia matokeo wanafunzi wale tu walioshutumiwa
kufanya udanganyifu bali kuwafutia wote kwa kuwa mitihani ulivuja. Kufuatia hoja hizo za msingi Baraza halina budi kukubali kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, na Baraza litapungukiwa na ubebaji wa lawama kwa kuondoa dhana hii ya kuvuja kwa mitihani kwa kurejewa kuliko kubakia katika kung'ang'ania
kutorejewa na kuanza kuibua msuguano mwengine wa mvutano kati ya Zanzibar na Tanzania Bara katika suala la elimu na hatimae kuweza kuhatarisha Muungano. Mbali na suluhisho la kurejewa kwa mitihani, kwa upande mwengine ipo haja ya vyombo husika vya Wizara ya Elimu visimame imara na kufanya uchunguzi wa kina wa matokeo haya na wahusika wote wa tokeo hili bila ya kuwaonea haya watakapobainika
wawajibishwe kwa kadhia hii mara moja, huku wizara husika zikifikiria
kuwabadilisha baadhi ya watendaji wake kutokana na kadhia hii ya kuvuja kwa mitihani kila mara. Hili ni la msingi kufanyika kwa kuzingatia dhana nzima ya utawala bora ambapo Tanzania inajisifia. Wakati huo huo Kamati inaunga mkono jitihada za Jumuiya ya DCPM kwa utafiti wa kisheria juu ya kadhia hii. Kamati ya wazee pia, inatowa tamko iwapo Baraza litaona kuna ugumu wa kurejewa kwa mitihani kwa Zanzibar, jambo ambalo kwa hakika linawezekana pale ambapo kuna adhma njema, basi pia Baraza libainishe kwa walimu wao makosa ya kila mwanafunzi kwa wale waliofutiwa na wale wenye mashaka na matokeo yao. Mwisho, kamati ya wazee pia ina mashaka juu ya matokeo ya Tanzania Bara kwamba itakuaje skuli za aina Fulani tu iwe asilimia kubwa ya wanafunzi wake wawe ndio miaka yote wanaopata alama za ‘A' kwa wingi (maana ya Division ya kwanza), na ndio skuli bora mara zote Tanzania, je Baraza la Mitihani hili halikupeni mashaka? Au hao ndio wenye uwezo peke yao? Ahsanteni, Naomba kuwasilisha, Katibu wa Kamati ya Wazazi, Saleh Mohammed Saleh.

Tatizo lenu watu wa visiwani kila kitu mnapenda mtelemko tu na siku zote mnaota mnaonewa hapo hakuna mjadala, kama watoto wenu mnawaamini hawakuchakachua mtihani warudie mitihani na wafaulu ndiyo jambo la maana tofauti na hapo mnapoteza muda bure kulalamika maamuzi yakitoka yameshatoka hakuna baraza la wazee wala la vijana NECTA INAENDESHWA KWA SHERIA NA SIYO VIKAO NA MATAMKO YA WAZEE PALE NI UKWELI TU HAKUNA KUBEMBELEZANA. JUHUDI ZENU NI KAMA MIPANGO YA WATU FULANI WALIOENDESHA JUHUDI ZA KUMFUFUA MAREHEMU, KAMA MNAWEZA KUMFUFUA MAREHEMU ENDELEENI NA JUHUDI ZENU MTAFANIKIWA.

MBONA HAMSEMI KWA WANAFUNZI WA HUKOHUKO WALIOFANYA VIZURI NA KUPATA DIV. 1,2 NA III? KUWA WAMEPENDELEWA? HAKUNA CHA KATIBU WALA MWENYEKITI PELEKA WATOTO SHULE ACHA SIASA KWENYE ELIMU
 
Back
Top Bottom