Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Arusha yabanwa kuhusu Mabomu

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,698
22,735
KIKAO cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Arusha (RCC) kimetaka polisi na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, kuacha kutoa matamko ya haraka, badala yake wachunguze kubaini chanzo cha milipuko ya mabomu jijini hapa.

Miongoni mwa wajumbe wa kikao hicho ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema aliyesema matukio hayo si ya siasa, bali yanayodhuru jamii, hivyo ni vyema polisi wanapopewa taarifa wazifanyie kazi.

"Usalama wa wananchi uko wapi? Kila mara mabomu, mabomu, na baadhi ya wanasiasa wanatumia masuala haya ya mabomu kama ni umaarufu wa kisiasa. Hapana. Tuache mambo haya. Tunataka matukio haya yachunguzwe kwa kina ili kujua kiini cha tatizo hili ni nini na si kudai masuala ya kisiasa," alisema Lema.

Katika kikao hicho, ilishauriwa kila mfanyabiashara mwenye biashara yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 50, afunge kamera za CCTV. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Meru, Dk Paulo Akyoo, alisema ni vyema ulinzi na usalama ngazi ya kata, urejeshwe.

Alishauri viwepo vikao vya mara kwa mara na polisi wahakikishe wanajenga urafiki na wananchi. Pia, alihimiza taarifa zinapotolewa kwa jeshi hilo, wazifanyie kazi na kutoa majibu sahihi kwa wananchi.

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck ole Medeye alisema Arusha inapaswa kuangaliwa kwa jicho la pekee na kusisitiza Kamati ya Ulinzi na Usalama, ihakikishe inachunguza matukio hayo kwa makini na kutoa majibu sahihi.

Medeye alishauri kamati ya ulinzi baada ya kuchunguza kwa makini, imshauri Rais Jakaya Kikwete mambo ya kufanya kudhibiti matukio hayo.

Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha katika kikao hicho, Edith Salvas, aliomba ushirikiano kwa wananchi ili kubaini waliohusika na matukio ya ulipuaji wa mabomu jijini Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela aliyekuwa akiongoza kikao hicho, alisema inabidi vyombo vya ulinzi na usalama, vifanyie kazi michango ya wajumbe, kwa kuhakikisha vinakuja na majibu yatakayotoa picha kamili kwa wananchi juu ya matukio hayo.

Katika hatua nyingine, washitakiwa 16 wanaodaiwa kushiriki katika kikundi cha kigaidi, jana walipandishwa kizimbani kwa mara ngingine, mbele ya Hakimu Devota Msofe na kuomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, iwaeleze hatma ya dhamana yao. Walitaka kufahamu kama kesi yao ina dhamana au la, na wakati huo huo kufahamu ni lini watapata dhamana.

Pia, walidai baadhi yao wana nakala ya hati ya mashitaka, hivyo wanaomba wote wapewe. Hakimu alisema kesi yao haina dhamana na kuhusu hati, aliwaambia atawapatia wote.

"Kweli kesi yenu haina dhamana na kama mna hoja nyingine niambieni, ila kuhusu nakala ya hati ya mashitaka, nitawapatieni leo (jana) hii, maana ni haki yenu ya msingi," alisema Hakimu Msofe.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Gaudencia Joseph, alidai washitakiwa Abdulkarimu Hasia na Abdallah Wambura, hawakufika mahakamani kutokana na kuendelea kuumwa.

Washitakiwa wanaokabiliwa na kesi ni Abdala Athumani, Swalehe Hamisi, Abdallah Yasini, Hassani Saidi, Sudi Lusuma, Abdulkarim Hasia na Shaban Wawa.

Wengine ni Hassan Saidi, Rajab Hemedi, Ally Kidaanya, Abdallah Wambura, Shabani Wawa, Ally Jumanne na Yassin Sanga. Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na uchunguzi kutokamilika na itatajwa tena Julai 24 mwaka huu.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walilipua mabomu kati ya 2010 hadi Februari mwaka huu, maeneo mbalimbali. Ilidaiwa washitakiwa hao, walijaribu kusajili watu kujiunga na kikundi cha kigaidi.

Wanadaiwa walimuua Sudi Ramadhan, ambaye alikufa akiwa anapata matibabu Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Mei 13 mwaka huu.

Aidha, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa walijaribu kuwaua watu 14 katika tukio hilo la mlipuko wa bomu la Aprili 13 saa 1:30 mwaka huu katika baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini..


Source:
Habari Leo
 
mbowe na lema wanajua wamuulize mbowe aleta na ule ushahidi aliosema anao.
 
Arusha km iraq!wananchi wanamiliki mabomu bila police kujua.!MUNGU PEKEE NDIYE AWEZAYE KUTUOKOA KTK HILI.
 
"Walikuwa wanaandikisha watu kujiunga na vikundi vya ugaidi(al-shaabab)" Walikuwa wanafanyia mazoezi mafunzo ya awali, nadharia kwenye matendo. Siku wakifuzu sijui itakuwaje. Hapa watakuja jamaa na mapovu kutukana. FaizaFoxy@ifweero@MSALANI
 
Last edited by a moderator:
RC Mulongo uzoefu wa uongozi kaupata Bagamoyo, sasa kwa Arusha mnamuonea tuu. Yupo clueless na hapless
 
Vyombo vyetu vya usalama vinapaswa kufanya vizuri zaidi ya mazoea. Ulimwengu wa sasa ni wa uwazi zaidi na unataka matokeo yanayoonekana. Wimbo wa kila siku wa maelekezo, maagizo, maombi ya taarifa kutoka kwa watu yasiyo na ufanisi katika matukio yanayojirudia hayawapi imani watu kutoa ushirikiano unaodaiwa.

Ni vizuri tutafakari ni wapi tunakosea, kwa sababu hakuna maelezo ya kutosha matendo haya yanafanyika zaidi ya mara nne eneo moja, tusijue sababu au chanzo zaidi ya kauli za kisiasa na maagizo. Je tuseme hawa watu wanateremka toka angani na wakishatekeleza uhalifu wanarejea huko angani! Na mipango yao je nayo inapangwa huko angani! Ni kwa nini taarifa hazivifikii vyombo vyetu vya usalama ambavyo pia vinaishi pamoja na raia? Matokeo yake ni speculation zinazoongeza tahaluki ndani ya jamii yetu!
 
Back
Top Bottom