Kamati ya siasa CCM mkoa wa Mwanza yamvua uenyekiti mwentekiti wa Halmashauri Wilaya ya Misungwi

Godwin Mneng'ene

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
215
84
Nimefurahishwa sana na uamuzi wa kamati ya siasa ccm mkoa wa mwanza kumvua nafasi ya uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya misungwi ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha uliogunduliwa na CAG.

DED alishasimamishwa yeye alishauriwa ajiulzulu na kamati ya siasa ccm wilaya ziadi ya wiki sasa alikuwa hajatekeleza ushauri huo.

Hongereni ccm mkoa wa mwanza
HATIMAYE Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, kimeamua kuchukuwa maamuzi magumu ya kumvua nafasi ya uenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, Bernard Polycap, kutokana na tuhuma nzito za ufisadi wa fedha za miradi ya maendeleo wilayani humo zinazomkabili.

Maamuzi hayo magumu yametolewa jana na kamati ya siasa ya mkoa wa Mwanza, chini ya uenyekiti wake, mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Clement Mabina, baada ya kile kinachodaiwa
Polycap kukaidi maagizo ya chama hicho tawala kupitia kamati yake ya Siasa ya wilaya ya Misungwi, iliyomtaka kiongozi huyo kujiuzulu nafasi hiyo ya uenyekiti ndani ya siku tatu, kuhusiana na tuhuma zilizopo katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akitoa taarifa ya Kikao cha Kamati hiyo ya siasa jijini hapa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM mkoani Mwanza, Simon Mayunga Mangelepa alisema, CCM kimelazimika kuchukuwa hatua hiyo nzito baada ya kiongozi huyo kukaidi maamuzi ya chama ngazi ya wilaya.

Mangelepa alieleza kwamba, chama chake kinajiandaa kupeleka taarifa rasmi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, ili afanye utaratibu wa kuitisha uchaguzi mwingine wa kushika nafasi hiyo miongoni mwa madiwani wa halmashauri hiyo.

"Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Mwanza, imemvua nafasi ya uenyekiti wa halmashauri ya Misungwi ndugu Bernard
Polycap. Maamuzi haya ni mazito na yamechukuliwa na chama baada ya kujiridhisha na tuhuma zilizopo kwenye ripoti ya CAG dhidi ya Polycap", alisema Mangelepa.

Halmashauri ya wilaya ya Misungwi, inakabiliwa na tuhuma nzito za ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni 4 za miradi mbali mbali ya maendeleo, na kwamba unaomhusisha pia aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kabla ya kuvuliwa madaraka, Xavier Tilweselekwa, zilizofichuliwa katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ya mwaka wa fedha wa 2008/2009 na 2009/2010.

"Pamoja na Bernard kutakiwa aachie ngazi kwa hiari kupisha hatua za kisheria ziendelee, hakufanya hivyo badala yake amekuwa akidai kakata rufaa kupinga maamzi hayo na kutamba kuwa mkoa usubiri kupata maagizo toka ngazi ya juu", alisema Mangelepa.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Clement Mabina alisema leo ofisini kwake kwamba, hatua hiyo ya Polycap kuvuliwa nafasi ya uenyekiti wa halmashauri hiyo ya Misungwi, imetarahisisha vyombo vya dola kufanyakazi zake vizuri juu ya tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo.

Alisema, kwa namna moja au nyingine, vyombo vya dola vinaweza kushindwa kufanyakazi zake vizuri iwapo mtuhumiwa husika ataendelea kuwepo katika nafasi yake, na kwamba CCM ilichofanya ni kumvua uenyekiti ili kuvipa mwanya mzuri vyombo hivyo vya dola vimshughulikie zaidi kisheria, na kwamba ataendelea kuwa mwanachama wa CCM na nafasi yake ya udiwani wa kata ya Igokelo.

"Jana Polycap chama kilimvua nafasi yake ya uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi. Haya ni maamuzi magumu ambayo yamechukuliwa na kamati ya siasa ya mkoa baada ya kuona mwenyewe amekaidi maagizo ya ngazi ya wilaya.

"Ikumbukwe kwamba, CCM inafanya maamuzi yake kwa kufuata taratibu, kanuni na katiba ya chama. Hatukurupuki. Aliitwa akaja kwenye kikao cha kamati ya siasa na akaelezwa tuhuma zake, kisha kuvuliwa nafasi yake hiyo. Lakini anayo haki ya kukata rufaa ngazi za juu", alisema mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mwanza, Mabina na kuongeza:

"Unajua chama ndicho kilichompitisha kugombea nafasi ya uenyekiti. Kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama CCM ngazi ya mkoa inayo mamlaka ya kumwondoa kwenye nafasi hiyo pale kitakapojiridhisha juu ya tuhuma zinazomkabili kiongozi".

Hata hivyo, Polycap alipotafutwa leo kwa simu yake ya kiganjani, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa, na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms), akiombwa kuelezea taarifa za kuvuliwa kwake nafasi ya uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, pia alikaa kimya hadi tunakwenda mitamboni.

Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma - FikraPevu, Mwanza.
 
Ninachoweza kuwashauri watu wa misungwi ni kuongeza idadi ya madiwani wa upinzani ktk halmashauri. Hali ilivyo sasa hivi ni vigumu sana kuinua wilaya kimaendeleo bila kuwapunguza nguvu wana CCM.

Hiki kilichofanyika inaweza kuwa ni kazi ya muda tu na baada ya siku chache akarudishwa ofisini.
 
Chama kimepotoka,labda kama ccm wamevua uanachama wao,Chama kama chama hakina mamlaka ya kung'oa kwenye uenyekiti wake kama diwani ,isipokuwa baraza kuu la Halmashauri kupitia kikao chake na agenda kuungwa mkono na 2/3 ya wajumbe wote ambao ni madiwani.Kama mleta taarifa utakuwa unamaanisha mapendekezo ya ccm kwenye kikao cha madiwani hiyo iwe agenda yao ikiwa na sababu pia mwenyekiti lazima apewe muda na nafasi ya kujitetea.Kwa kuwa Mwenyekiti wa halmashauri anaungwa mkono na madiwani wengi wa ccm kamati ya siasa bado inakazi nzito labda Mwenyekiti mwenyewe arahisishe mambo na kujiuzulu mapema kama amavyo chama kinamshinikiza.
 
haya ndiyo maneno sahihi.
Umepoint jambo muhimu sana.
Kamati ya siasa ya chama inauhalali kisheria kumvua uenyekiti mwenyekiti wa halmashauri ambaye hawakumchagua? Ni dhahiri ccm wamechanganyikiwa!!!
 
Usanii mtupu! Kwani wao ndio walimchagua!? Amechaguliwa na madiwani na ndio wenye uwezo wa kumtoa. Hata kama angekuwa ameelekezwa na kamati ya siasa ya ccm Taifa, labda wamvue uanachama!
 
Atapewa ukuu wa wilaya hiyo hiyo, hao ndio magamba ukiwa mwizi ukifukuzwa watakurudisha kwa kukupa cheo.
 
Chama kimepotoka,labda kama ccm wamevua uanachama wao,Chama kama chama hakina mamlaka ya kung'oa kwenye uenyekiti wake kama diwani ,isipokuwa baraza kuu la Halmashauri kupitia kikao chake na agenda kuungwa mkono na 2/3 ya wajumbe wote ambao ni madiwani.Kama mleta taarifa utakuwa unamaanisha mapendekezo ya ccm kwenye kikao cha madiwani hiyo iwe agenda yao ikiwa na sababu pia mwenyekiti lazima apewe muda na nafasi ya kujitetea.Kwa kuwa Mwenyekiti wa halmashauri anaungwa mkono na madiwani wengi wa ccm kamati ya siasa bado inakazi nzito labda Mwenyekiti mwenyewe arahisishe mambo na kujiuzulu mapema kama amavyo chama kinamshinikiza.

nashukuru mdau na mjumbe wa mtandao umejaribu kueleza haki sheria inavyoelekeza.Kutokana na sheria ya serikali za mitaa, ni waziri au baraza la madiwani ndo lenye mamlaka ya kumvua mwenyekiti au meya.Hapa chama hakina nafasi vinginevyo chama kimvue uanachama.Mleta thread hii ni mtambo hajui anachosema, na pia inaonyesha kama ccm imefanya hivyo hawana akili , hawezi kung'oka sababu sheria itakuwa imekiukwa.
 
jinsi madiwani wanavyowakaba roba HODS , DT NA MKURUGENZI WA HWILAYA SIDHANI kumuondoa MWENYEKITI KUTASAIDIA lolote . madiwani ndio kichocheo cha ulafi na umchwa wa HW kwakweli kuna wakti MADIWANI wanafanyakazi kwa syndicate huku mbarali ag DED amepona kwa style hiyo SIO kwasababu ya usafi wa halmashauri yake. lakini ni kwasababu ya amewasoften in some ways. madiwani watekeleze majukumu yao waache kutafuta mchawi.kauli zao ni za kinafiki wilaya hata iwe haina hela wao pesa yao kwanza huu unafiki bora kuacha kazi hali ni mbaya sana jamani. halmashauri hazina hata hela ya kununua karatasi na katriji za wino kazi zitafanywaje juzijuzi LUKU Imeisha siku 2 hakuna kazi yaani hovyo kabisa . mambo ya kubinafisisha HW NI JAMBO LISLIO KUBALIKA
 
Back
Top Bottom