Kamati ya Katiba: Prof. Baregu kuapa bila Biblia wa Quaran nini tafsiri yake?

Dini ya kwanza ni imani katika nafsi. Kushika Quaran au Biblia ni Mbwembwe tu kwani tumeshuhudia waliozibeba kwa unyenyekevu katika viapo lakini wakatukaanga. Isitoshe Prof. haendi kunadi dini bali kutafuta mustakabali wa nchi kwa kupima utayari wa nafsi yake kuwatumikia watanzania.
Hello Bandugu:

Tafadhali rejea site hii: matukio-michuzi

Nimeshangaa sana Prof. Baregu kuapa bila Biblia wala Quaran. Naomba kuelewesha maana/tafsiri yake. Please! Tafadhali!
 
Maana yake ni kuwa anayachukulia serious maneno yetu wenyewe kuwa "TAIFA AU SERIKALI HAINA DINI, ILA WATU BINAFSI WANA DINI ZAO". Yuko tayari kwa kazi ya Serikali na si ya mtu binafsi.

Namuunga mkono nami nitafanya hivyo wakaa utapowadia.
 
Taratibu mnaelekea wapi.Kwenye World donination?Pole,wewe wamekudanganya,you are not one of them,ni karai tu.
Taratiiibu tunaelekea. Sasa kama mtu si Mkristo/Muislam na hana imani ya dini utamlazimisha?

Hili mbona hata mchongameno alishasema siku tukipata rais mteule asiye na dini tutamuapisha tu bila biblia wala Quran (wakati akipinga udini katika siasa na kuonyesha ukomavu wa mawazo kwamba Tanzania hatujali mtazamo wa kidini wa kiongozi).
 
Walioasisi kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu walikuwa waadilifu na walikuwa na hofu ya Mungu mioyoni mwao, ndo maana waliamini kuwa huwezi kuapa ukiwa umeshika mkononi kitabu kitakatifu kisha ukatenda kinyume na mapenzi ya Mungu! Mtindo huu ulianza zamani sana enzi za Nabii Ibrahim, pale alipomwapisha mtumishi wake aliyemtuma kwenda kumtafutia mwanae wa kiume Mke, pale alipoweka mkono wa kijana huyu kwenye paja lake na kumwapisha kwamba ataenda kumtafutia mwanae mke kutoka katika ukoo wake Ibrahim. Baada ya kiapo ulifuAta utekelezaji kwa mujibu wa kiapo na si vinginevyo! Lakini tumebaki TUNAIMBA KIJAMAA NA KUCHEZA KIBEPARI!
kweli kabisa mkuu!
 
Wewe ni mmoja kati ya wasomi wachache wenye busara humu JF. Ni mara chache sana humu mtu kuongea na kuchangia kwa mambo tuliyoyasoma na kufanya reference. Baregu is my teacher, mtazamo wake ni huohuo wala hujakosea....you are very right.

Pamoja mkuu.............thanx kwa compliment mkuu.

We need to live by our words TaMuga.......those people up there made us the way we baheve now.....atleast to have some pillars to lean on
 
Nadhani kuna mantiki zaidi kwa watu wenye msimamo mkali wa dini kukataa kuapa kwa kutumia misahafu.

Kuapa kwa misahafu kunamaanisha kuwa kwa muapaji, msahafu ndio mamlaka ya juu zaidi kuliko kitabu chengine chochote.

Tukichukulia Muislam kwa mfano, Quran inasheria za wazi zinazopinga uzinzi wakati Katiba anayoapa kuilinda haikubaliani na sheria hizo.

Hapa ina maana kuwa ana apa kwa Quran kulinda sheria zinazopingana na Quran yenyewe

Ikiweza kumaanisha kuwa huyo mtu si muadilifu kwa hiyo Quran anayoiapia na hivyo haina athari yoyote katika kiapo chake

Ni bora wangeacha tu kutumia misahamu
 
Wewe ni mmoja kati ya wasomi wachache wenye busara humu JF. Ni mara chache sana humu mtu kuongea na kuchangia kwa mambo tuliyoyasoma na kufanya reference. Baregu is my teacher, mtazamo wake ni huohuo wala hujakosea....you are very right.

Pamoja mkuu.............thanx kwa compliment mkuu.

We need to live by our words TaMuga.......those people up there made us the way we bahave now.....atleast to have some pillars to lean on
 
Function ya dini ikichukuliwa kama social gathering haina tatizo. Tatizo la dini ni kwamba milele yote imekuwa inalazimishwa kuwa "a spiritual thing" kinafiki, wakati ukweli ni kwamba dini "is a social thing." Nothing else!

Zipo sababu nyingi za kisaikolojia kuhimiza wanadamu kufanya "socialization." Na kwa mantiki hii mimi nakubali na kuhimiza ndugu, marafiki na wapenzi kwenda Masjid au Kanisani. Ni sehemu nzuri ku-make friends, kuona mitindo mipya ya bargashia, kanzu, suti na mavazi mengine; ni sehemu nzuri kuona mitindo mipya ya magauni, nywele na staili mpya za kuongea na kucheka. beyond that church na masjid turns into an enclave of liars na unafiki kibao! bwana yesu asifiwe--halaf jioni yupo kwenye viroba na soda kama siyo gesti. mwingine sigda imeota sugu kabisa kwenye paji la uso lakini tapeli wa kuogopwa kama ukoma. the best dini on earth is truth and justice.

Ukweli na Haki ndiyo dini ya kweli duniani. nothing else!

Mungu wangu tuokoe!
Ina maana kutokufuata dini kunasababisha dini isiwe na thamani yoyote? HAPANA kutokutekeleza dini kama ulivyosema huo ni udhaifu wetu wanadamu na kuendekeza matashi ya nafsi zetu na kuacha mafundisho ya mungu.
Nakukatalia ukisema udhaifu huo udisqualify dini kabisa HAPANA mkuu wangu!
 
Sio kweli hata kidogo! machafuko na vita nyingi duniani vimesababishwa na dini. Watanzania sasa hivi wameanza kuchukiana na kutoaminiana kwa sababu ya misingi ya dini. Dini ni bange mbaya sana!

Nakugongea LIKE,
 
kimsingi ni unafiki mtupu kumshirikisha mungu kwa kuapa wakati unajua kabisa unayoapia una nafasi ndogo sana ya kuyazingatia. BIG UP my true Prof.
 
Mimi ni mkristu na naamini mungu yupo,ofcourse kiimani nitakuambia beyond reasonable daught!
Lakini pia naamini mwenyezi Mungu anapower kuliko kiumbe chochote kile at least hapa duniani!point yangu ni kwamba pamoja na ukatoliki wangu,siamini kwamba kuna mtu ataenda mbinguni kwa sababu yeye ni mkatoliki,mhindu,mpagani,msuni or anything!ndivyo pia siamini kwamba kuna mtu hataenda peponi kwa sababu yeye ni wa dini fulani!akili za kawaida kabisa zinakuambia huo utakuwa ni uwendawazimu!matendo jamani matendo!hivi leo kuna baazi ya sehemu hawajawahi,nahawatakuja pata sikia uislamu,ukrstu,uhindu,ubaniani na nyinginezo!na wengine walishatangulia mbele za haki,sasa inakuwaje kwa hawa!!!?

Mwambie Baba Paroko maneno hayo uone kama hujapigwa ban ya kupokea sakramenti.
 
Mi namuunga mkono, huwezi kushika vitabu vilivyo jaa historia na tamaduni za watu wengine na ukavitumia kujiapiza....
 
Mimi ni mkristu na naamini mungu yupo,ofcourse kiimani nitakuambia beyond reasonable daught!
Lakini pia naamini mwenyezi Mungu anapower kuliko kiumbe chochote kile at least hapa duniani!point yangu ni kwamba pamoja na ukatoliki wangu,siamini kwamba kuna mtu ataenda mbinguni kwa sababu yeye ni mkatoliki,mhindu,mpagani,msuni or anything!ndivyo pia siamini kwamba kuna mtu hataenda peponi kwa sababu yeye ni wa dini fulani!akili za kawaida kabisa zinakuambia huo utakuwa ni uwendawazimu!matendo jamani matendo!hivi leo kuna baazi ya sehemu hawajawahi,nahawatakuja pata sikia uislamu,ukrstu,uhindu,ubaniani na nyinginezo!na wengine walishatangulia mbele za haki,sasa inakuwaje kwa hawa!!!?

Ukatoliki wako umeegemea wapi? Kama ni Biblia basi inasema; "Hakuna Jina jingine tulilopewa wanadamu liwapasalo kukolewa kwalo ila ..." Hivi Mungu tunamchukulia kama shemeji yetu? Biblia hiyohiyo inasema kuwa aliziangamiza Sodoma na Gomora. Watoto kwa wakubwa. Aliwaua wazaliwa wote wa kwanza wa binadamu na mnyama katika Misri. Tena, akaiangamiza dunia kwa gharika. Kama kweli wewe ni muumini wa kikatoliki unajua kuwa hakumuachia hata mwanawe wa pekee katika kifo cha msalabani. Eti Mungu huyo huyo "kwa akili za kawaida" leo atahurumia wengine. Kweli ni akili chini ya kawaida kuamini vinginevyo kama kweli wewe ni muumini wa Kikatoliki. Wataka uthibitisho, subiri siku inakuja.
 
kama kuna jambo ambalo linazidi kuwadidimiza watu weusi basi ni hizi dini tunazozing'ang;ania ambazo zililetwa na wageni kwa manufaa yao,hakuna kitu kibaya kama DINI...matokeo yake ndio tuko kama tulivyo leo hii...wetu weusi ni HOPELESS KABISA KWA DINI....HONGERA BAREGU!

Inashangaza sana kuzikebehi dini eti kwa sababu tumeletewa na wageni. Leo hii katika nchi hii ni kipi cha kwetu? Huyo profesa mwenyewe, uprofesa, elimu yake na hata imani yake (sijui mmeiitaje kwa kidhungu - hyumanizim) vyote hivyo ni vya kuletewa na wageni hao hao walioleta dini. Tanzania yenyewe tumeletewa, katiba, serikali hata nguo. Ee bwana we hata huu mtandao tumeletewa. Kwanini kuzishutumu dini kwa msingi wa kuletewa ili hali vingi tulivyonavyo tumeletewa? Tafuta msingi mwingine. Halikadhalika, hoja yako inataka kuwaaminisha watu kuwa dini zetu za asili zilikuwa bora jambo ambalo si kweli. Kama uliwahi kusoma kitabu cha Things Fall Apart. Ukatili ule aliofanyiwa Ikemefuna ndio fasheni ya dini zetu. Zilikuwa za "kishenzi"! Jiulize kwanini miongoni mwa jamii ambazo bado zinafuata imani hizo hakuna albino? Ndugu yangu ni majuzi tu ndipo vijijini kunaonekana albino (dini za asili hizo). Unajua maana ya kigego? Watoto wengi walipoteza maisha wakati wa kuzaliwa chini ya himaya ya dini za asili. Hivyo si sahihi kudhani kuwa dini za asili zilikuwa bora.
Watu kushindwa kutenda mema ilihali wanafuata dini ni ubinadamu tu wala haitokani na kufuata dini za kuletewa. Msimsifu profesa kuwa kajikomboa kwani naye anafuata elimu na imani ya kuletewa japo si Uislam wala Ukristo.
 
Back
Top Bottom