Kamati ya Katiba: Prof. Baregu kuapa bila Biblia wa Quaran nini tafsiri yake?

Hello Bandugu:

Tafadhali rejea site hii: matukio-michuzi

Nimeshangaa sana Prof. Baregu kuapa bila Biblia wala Quaran. Naomba kuelewesha maana/tafsiri yake. Please! Tafadhali!

Suala la mtu kuapia Biblia/Qur'an wakati haendi kutenda kazi ya kanisa ni kuzibana mdomo. Lakini pili hivi ni vitu ambavyo vilitumika na wazungu ili mtu asikikiuke maagizo alopewa hata kama kuuwa eti Mungu atamlaani au atakuwa ametenda dhambi.

Kama mtu anaweza kupata kitabu cha NOT YET UHURU-OGINGA ODINGA akisome kinaweza kumsaidi kuelewa wazungu walivyo tubrainwash kwa kutumia dini, eti lazima upewe majina kama Joseph, Mohammed ndiyo uonekane wewe ni wa dini fulani, lazima uhudhurie Masjid/kanisan ili uonekane wewe ni mtu wa imani hiyo.

Yale maeneo ni ya kukutania hasa katika dunia ya sasa ambapo tamaduni zetu zimepungua nguvu na mshikamano umepungua hivyo kama mtu angesema yeye ni CDM/CCM/ADC nk.

=
NAWASILISHA=
 
Mawaziri na raisi wako si wameapa kwa hivi vitabu vitakatifu lakini wametuibia mara ngapi! Ni kutomuonesha mungu unafiki ilihali unajua ipo siku utakosea, siku hizi kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu vya mungu imekuwa ni kama kanuni au fasheni fulani hivi.
 
kama kuna jambo ambalo linazidi kuwadidimiza watu weusi basi ni hizi dini tunazozing'ang;ania ambazo zililetwa na wageni kwa manufaa yao,hakuna kitu kibaya kama DINI...matokeo yake ndio tuko kama tulivyo leo hii...wetu weusi ni HOPELESS KABISA KWA DINI....HONGERA BAREGU!
 
hello bandugu:

Tafadhali rejea site hii: matukio-michuzi

nimeshangaa sana prof. Baregu kuapa bila biblia wala quaran. Naomba kuelewesha maana/tafsiri yake. Please! Tafadhali!

hakuna andiko lolote linaloturuhusu kuapa kwa biblia. La quaran siwezi kulisemea maana huko sihusiki.biblia inaelekeza kutokuapa kwa anga wala mbingu. Kiapo cha kibiblia ni kusema ndio au hapana basi hatupaswi kuongeza wala kupunguza. Mbona hao hao wanaoapa kwa vitabu ni majizi makubwa. Jamani tuache kumchezea mungu

Moja ya tafsiri yaweza kuwa ni hii;

Kama memory yangu inanielekeza sawa huyu ni MARXIAN BELIEVER AND A GOOD FOLLOWER (The late Chachage's type) na ni sehemu ya ujuzi wao kuwa dini ni OPIUM OF THE PEOPLE so huwa watu wa aina hii ni kawaida kabisa kuiweka mbali dini na mambo ambayo yanafanyika hapa usoni mwa ulimwengu wakati hayahitaji imani yoyote ili yaweze kuwa kama yanavyotarajiwa.

Inapokuja kwenye utekelezaji mambo ya msingi katika maisha wao huamini kwamba ni lazima ujiondoe kwenye sifa zote ulizonazo kutokana na malezi yako (dini,mila.....n.k) ili uweze kutumia ujuzi wako kikamilifu katika kutimiza azma yako kama msomi (learned specie) na si zao la jamii fulani (social being) ndo maana kakataa hivyo vitabu kwa sababu mafundisho yake yanatufanya tuwe learned species with a taste of social beings ambayo madhara yake ni kama haya tunayosikia......fulani mdini......huyu ana ukabila.....anapedelea wanawake/ wanaume......na mambo kama hayo

Naomba kuwasilisha wanabodi
 
Sio kweli hata kidogo! machafuko na vita nyingi duniani vimesababishwa na dini. Watanzania sasa hivi wameanza kuchukiana na kutoaminiana kwa sababu ya misingi ya dini. Dini ni bange mbaya sana!

Duh! Umenikumbusha Karl Marx - Religion is the opium of the people.
 
Atakuwa ni mpagani. maana yake hana dini

Acha uzuzu wewe kwani kuwa na dini wewe ndio mtakatifu? mtu mwema tutamtambua kwa matendo yake na Dini iliyosafi ni kutembelea na kusaidia wajane na Yatima soma yakobo sura ya 4 yote, utajua nini maana ya dini
 
Mimi ni mkristu na naamini mungu yupo,ofcourse kiimani nitakuambia beyond reasonable daught!
Lakini pia naamini mwenyezi Mungu anapower kuliko kiumbe chochote kile at least hapa duniani!point yangu ni kwamba pamoja na ukatoliki wangu,siamini kwamba kuna mtu ataenda mbinguni kwa sababu yeye ni mkatoliki,mhindu,mpagani,msuni or anything!ndivyo pia siamini kwamba kuna mtu hataenda peponi kwa sababu yeye ni wa dini fulani!akili za kawaida kabisa zinakuambia huo utakuwa ni uwendawazimu!matendo jamani matendo!hivi leo kuna baazi ya sehemu hawajawahi,nahawatakuja pata sikia uislamu,ukrstu,uhindu,ubaniani na nyinginezo!na wengine walishatangulia mbele za haki,sasa inakuwaje kwa hawa!!!?
 
Moja ya tafsiri yaweza kuwa ni hii;

Kama memory yangu inanielekeza sawa huyu ni MARXIAN BELIEVER AND A GOOD FOLLOWER (The late Chachage's type) na ni sehemu ya ujuzi wao kuwa dini ni OPIUM OF THE PEOPLE so huwa watu wa aina hii ni kawaida kabisa kuiweka mbali dini na mambo ambayo yanafanyika hapa usoni mwa ulimwengu wakati hayahitaji imani yoyote ili yaweze kuwa kama yanavyotarajiwa.

Inapokuja kwenye utekelezaji mambo ya msingi katika maisha wao huamini kwamba ni lazima ujiondoe kwenye sifa zote ulizonazo kutokana na malezi yako (dini,mila.....n.k) ili uweze kutumia ujuzi wako kikamilifu katika kutimiza azma yako kama msomi (learned specie) na si zao la jamii fulani (social being) ndo maana kakataa hivyo vitabu kwa sababu mafundisho yake yanatufanya tuwe learned species with a taste of social beings ambayo madhara yake ni kama haya tunayosikia......fulani mdini......huyu ana ukabila.....anapedelea wanawake/ wanaume......na mambo kama hayo

Naomba kuwasilisha wanabodi

Wewe ni mmoja kati ya wasomi wachache wenye busara humu JF. Ni mara chache sana humu mtu kuongea na kuchangia kwa mambo tuliyoyasoma na kufanya reference. Baregu is my teacher, mtazamo wake ni huohuo wala hujakosea....you are very right.
 
Mimi ni mkristu na naamini mungu yupo,ofcourse kiimani nitakuambia beyond reasonable daught!
Lakini pia naamini mwenyezi Mungu anapower kuliko kiumbe chochote kile at least hapa duniani!point yangu ni kwamba pamoja na ukatoliki wangu,siamini kwamba kuna mtu ataenda mbinguni kwa sababu yeye ni mkatoliki,mhindu,mpagani,msuni or anything!ndivyo pia siamini kwamba kuna mtu hataenda peponi kwa sababu yeye ni wa dini fulani!akili za kawaida kabisa zinakuambia huo utakuwa ni uwendawazimu!matendo jamani matendo!hivi leo kuna baazi ya sehemu hawajawahi,nahawatakuja pata sikia uislamu,ukrstu,uhindu,ubaniani na nyinginezo!na wengine walishatangulia mbele za haki,sasa inakuwaje kwa hawa!!!?

Hako kenye red kamenichanganya nimekapeleka kwenye Ms Word komputer ime ka - undeline....nimechange language into Spanish, French, lakini bado imekapigia red line.....nimeamua kuka - google nikapata hii... kutoka Urban Dictionary

Daught15 up, 20 down
The female and lesser version of son! Used when girls want to be as cool as those who call eachother son!Not every girl is a daught. They must pass strict compatability tests with the sons to gain recognition.
What ya up to daught!?
buy daught mugs & shirts
daught son face business female
by Ciaran Carney Nov 27, 2006 share this add a video

Ulimaanisha hiyo?

Katika moja ya speech za mwalimu aliwahi kuonya na kusema "Hatutamchagua mtu kwa sababu ya dini yake na baada ya kuchaguliwa ataapishwa ama kwa korohan au biblia lakini kama yeye hatakuwa na dini itatafutwa njia nyingine ya kumfanya aape "
 
kuna tafsiri nyingi:

moja...pengine haamini katika hizi dini zenu za mapokeo kutoka kwa waarabu na wazungu

mbili....pengine anayo dini ya mapokeo lakini si katika zile ambazo vitabu vyake vilikuwepo pale ikulu(niulize swali..kitabu cha wayahudi, baniani, bahai, zoroastrians kilikuwepo?)

tatu...pengine haamini kuwa mungu huyo unaemuamini wewe kama ana mchango au nafasi yoyote katika kubadilisha maisha ya watu(kwani waliokunywa kikombe cha loliondo kwa jina la mungu wana nini, si wengine wameshakufa kwa kikombe kushindwa kuwatibu?)

..........muhimu ni aliapa na kwa vile tunachohitaji ni katiba si biblia wala quran basi inatosha.
 
Huko Chadema si kwa kawaida kila wiki kuna kituko kimoja kutoka kwa mmoja wao kinacho draw national attention duh hawa watu ni chanzo cha mijadala ya kitaifa kwa sasa
 
Mbona unaposhitakiwa mahakamani na kuapa vitabu kuw utasema kweli! Kweli tupu, Ukikanusha shitaka huachiwi kwa vile umeapa?
 
Ule ulikuwa mtego..wamkatali waone. asinge apa na angejitoa kwenye tume halafu walio baki wangejibeba. Ile tume aliye ishikilia au anaye ifanya kidogo iheshimike ni baregu tu. ajitoe uone kinacho fuata ITV.
Najua una mapenzi makubwa sana na mwanazuoni huyu, lakini sikubaliani na msimamo wako kwamba yeye ni zaidi ya wote!Nakubaliana nawewe kwamba mchango wake utaleta changamoto muhimu, lakini mimi binafsi namkubali zaidi Prof. Shivji na nimefurahi Kikwete amefungua milango ya kuongeza majembe kama haya!
 
Mawaziri na raisi wako si wameapa kwa hivi vitabu vitakatifu lakini wametuibia mara ngapi! Ni kutomuonesha mungu unafiki ilihali unajua ipo siku utakosea, siku hizi kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu vya mungu imekuwa ni kama kanuni au fasheni fulani hivi.

Walioasisi kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu walikuwa waadilifu na walikuwa na hofu ya Mungu mioyoni mwao, ndo maana waliamini kuwa huwezi kuapa ukiwa umeshika mkononi kitabu kitakatifu kisha ukatenda kinyume na mapenzi ya Mungu! Mtindo huu ulianza zamani sana enzi za Nabii Ibrahim, pale alipomwapisha mtumishi wake aliyemtuma kwenda kumtafutia mwanae wa kiume Mke, pale alipoweka mkono wa kijana huyu kwenye paja lake na kumwapisha kwamba ataenda kumtafutia mwanae mke kutoka katika ukoo wake Ibrahim. Baada ya kiapo ulifuAta utekelezaji kwa mujibu wa kiapo na si vinginevyo! Lakini tumebaki TUNAIMBA KIJAMAA NA KUCHEZA KIBEPARI!
 
Back
Top Bottom