Kamati ya Bunge: Bwawa la Nyerere litakamilika Juni 2024, Tsh. Trilioni 5.85 zimelipwa tayari

Hili bwawa kila leo tarehe zinasogezwa mbele hii nchi kuna vituko sana..
 
Mradi wa JNHPP umefika 95.83% na mwezi Juni mwaka huu utakamilika huku kiasi Cha pesa Tsh. 5.85t,tayali kilisha lipwa kwa mkandarasi.

Mpaka sasa kiasi cha maji kilicho jazwa kwenye bwawa ni kina cha maji cha mita 167,ni kiasi tosha kwa kuanza uzalishaji wa umeme ambapo mwezi Februari 16,2024 mtambo wa kwanza utawashwa na ifikapo mwezi machi 2024 mtambo wa pili utawashwa.kiasi cha megawati 470 zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Chanzo : Jamiiforum toka mtandao wa X
 
NISHATI: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dkt. David Mathayo amesema Utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), umefikia 95.83% na utakamilika Juni 2024 huku Tsh. Trilioni 5.85 (89.24%) zikiwa zimelipwa kwa Mkandarasi.

Amesema, Kamati ya Bunge imejulishwa kuwa Ujazo wa Maji umefikia Kina cha Mita 167 kutoka usawa wa Bahari, kiasi kinachoruhusu kuanza Uzalishaji wa Umeme na Mtambo wa Kwanza utawashwa Februari 16, 2024, wa Pili utawashwa Machi 2024 ambapo Megawati 470 zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Kuhusu hali ya Umeme hadi kufikia Desemba 2024, uwezo wa Mitambo ya Kufua Umeme kutoka Vyanzo mbalimbali ulikuwa Megawati 1,889.84 ikiwa ni ongezeko la Megawati 195.29 kutoka Megawati 1,694.55 zilizokuwepo mwaka 2022.

Hata hivyo, Uzalishaji wa Umeme nchini bado ulikuwa chini ya Wastani wa Megawati 1,200 wakati Mahitaji ya Umeme ni Wastani wa Megawati 1,482.80, hali inayosababisha upungufu wa Nishati hiyo nchini kote kwa Megawati 283.
Na SGR itakamilika baada ya uchaguzi mkuu!!
 
Back
Top Bottom