Kamati kuu ya CCM trh 30.7.2011

Kwa taarifa za humu? au umeenda mbali zaidi kujiridhisha katika kutafuta ukweli? subiri dk chache watu watakavyo kuja kumeza matapishi yao maana taarifa nyingi hapa ni speculation.

Nduka

Hivi Yule Jamaa alikuambia jina lako kwenye lugha ya kwao ni nini vile?

katiba ya ccm haisemi chochote kuhusu kuwepo au kutowepo waalikwa. Nadhani kuwapo kwao ni FIKRA SAHIHI ZA MWENYEKITI WA CCM.

Mpaka sasa sijapata picha kamili ya yalichojili CC. Now I can see the gap hapa JF when MS, FMES wasipojitokeza kwenye habari za CCM.

Ndugu yangu Mizizi naomba ufafanuzi kidogo.

Humo ndani ya kikao cha kamati kuu siku hizi kuna wajumbe waalikwa?

Maana kwa nijuavyo, Si Lowasa, Chenge, wala Membe ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu.

Chenge aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Maadili siku za nyuma, lakini kwa kanuni mpya za maadili CCM za February 2010, Mwenyekiti ni rais na wajumbe wote ni lazima wawe members wa Kamati Kuu.

Sasa napata tabu kukufuatilia, maana mara unasema Guninita haungi mkono hoja za Nape, mara Chenge kaonesha dharau za wazi kwa mwenyekiti, mara Lowasa yupo kimya wanamsemea wengine. Yani haya yote ni ndani ya kikao au vipi?

Maana kwenye wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM sioni majina ya Lowasa, Chenge, Guninita, Membe etc etc

soma post zingine za nyuma ndio uandike.

ngoja nimalizie hii taarifa hapa halafu nije rasmi janvini......naona kuna mchanganyiko wa habari hapa jf juu ya kikao cha jana na upotoshwaji mkubwa...

alwatan
jf imekuwa chuo cha kuwadanganya wasioelewa.

wajumbe wote watajwa hapo juu hawako cc lakini hawa wasoma vyuo vya kata hapa jf wanapiga makofi pwaaaa.

wajumbe wa kamati kuu hawa hapa
1. Ndugu Jakaya Mrisho KIKWETE – Mwenyekiti
2. Ndugu Pius MSEKWA - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani KARUME - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Wilson MUKAMA - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) John Zefania CHILIGATI - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Vuai Ali VUAI - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed SHEIN – Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza PINDA – Mjumbe
9. Alhaj Ali Hassan MWINYI – Mjumbe
10. Ndugu Benjamin William MKAPA - Mjumbe
11. Dr. Salmin AMOUR – Mjumbe
12. Ndugu John Samwel MALECELA – Mjumbe
13. Ndugu Nape NNAUYE - Mjumbe
14. Ndugu Mwigulu MCHEMBA - Mjumbe
15. Ndugu January MAKAMBA – Mjumbe
16. Ndugu Asha Abdallah JUMA – Mjumbe
17. Dr. Hussein Ali MWINYI
18. Dr. Maua Abeid DAFTARI
19. Ndugu Samia Suluhu HASSAN
20. Ndugu Omar Yussuf MZEE
21. Prof. Makame Mnyaa MBARAWA
22. Ndugu Mohammed Seif KHATIB
23. Ndugu Shamsi Vuai NAHODHA
24. Ndugu Abdulrahaman KINANA
25. Ndugu Zakiah Hamdani MEGHJI
26. Ndugu Abdallah Omar KIGODA
27. Ndugu Pindi Hazara CHANA
28. Ndugu Steven Masatu WASSIRA
29. Ndugu Constansia BUHIE
30. Ndugu William LUKUVI

kuna mibaba inadanganya jf bila kuona haya.

Ulichosema ni kweli, ila kumbuka hiki ni kikao kilichojadili hatima za watu, kwahiyo wajadiliwa ilibidi lazima waitwe na kusikilizwa kwa maslahi ya chama chao na taratibu zao.
Kwa mfano, suala la Igunga, Rostam ameshirikishwa kwa kiasi kikubwa, na amepewa kazi kubwa ilibidi lazma aitwe.
Kwahiyo hakuna uongo hapa mkuu.
Labda wewe mwona karibu ndio unakurupuka kutoa matusi

Ulichosema ni kweli, ila kumbuka hiki ni kikao kilichojadili hatima za watu, kwahiyo wajadiliwa ilibidi lazima waitwe na kusikilizwa kwa maslahi ya chama chao na taratibu zao.
Kwa mfano, suala la Igunga, Rostam ameshirikishwa kwa kiasi kikubwa, na amepewa kazi kubwa ilibidi lazma aitwe.
Kwahiyo hakuna uongo hapa mkuu.
Labda wewe mwona karibu ndio unakurupuka kutoa matusi
mizizi wewe soma tu huo ujumbe mwingine. membe alikaa kimya hakusema kitu. membe sio mjumbe. je aliitwa halafu akawa hawezi kusema kitu. lowasa haongei bali anaongelewa na watu. ameitwa na mwenyekiti kujitetea akawa haongei na anaongelewa na watu. lowasa angekuwa mjumbe ningeelewa lakini si mjumbe. hiyo taarifa imepikwa kwa mabua ya mahindi. haijaiva kabisa.

nape amelahidi kuongea na media saa tano leo. sasa ni saa sita mchana!!!!!!!!!!!!!
Sirikali

duh ..jamaaa kweli wamewadhibiti....yaani hakuna hata ka habari kadogo reliable kalikovuja?
six alikuwa anatoa siri za vikao. kaachwa nje ya cc huko sasa hata fmes hawezi kupata habri.

sosi ya habari za fmes sio mzee malecela. mama kilango alikuwa sosi baada ya kuambiwa na sita.

malecela noma anamficha hata mkewe.

milango yote imefungwa hiyo jf mlie tu. subirini nec sita na wenzake watatoa siri

Naona BMW amechoshwa na taarabu anahitaji matendo. Ameona asipoteze muda (hamna maamuzi magumu). By the way, Chenge akiachia ngazi sote lakini sio ubunge inamaanisha nini? Does it mean ubunge hauhitaji mtu safi; au wenye chama wata-spin waseme alichaguliwa na wananchi hivyo ni wananchi wenyewe wanatakiwa wamkatae. Mmh!! Hii dhana ya gamba sijaielewa sawa sawa.

CCM ili boogie step kuwasimamisha kwenye ubunge watu wenye questionable scandals kama hawa.

Mtu ukishachaguliwa na wananchi, chama kukuvua ubunge njia pekee inayoweza ku make sense ni kukuvua uanachama kabisa.

Ndiyo maana hata Rostam -scandalous as he is- nilisema angejiuzulu vyeo vyake chamani lakini amalize kazi aliyoahidi kwa watu waliomchagua.

Uongozi wa CCM ukitaka kuwavua ubunge hawa watu utakuwa unatuambia kwamba hauaoni mbali zaidi ya pua . Kwa nini umsimamishe mtu kugombea ubunge, umpigie kampeni kwa wananchi halafu umfukuze kwa sababu ya rushwa iliyojulikana kabla ya kampeni na uchaguzi?

six alikuwa anatoa siri za vikao. kaachwa nje ya cc huko sasa hata fmes hawezi kupata habri.

sosi ya habari za fmes sio mzee malecela. mama kilango alikuwa sosi baada ya kuambiwa na sita.

malecela noma anamficha hata mkewe.

milango yote imefungwa hiyo jf mlie tu. subirini nec sita na wenzake watatoa siri

kwani Nape hayumo humo ndani?

Taarifa kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinasema tayari chama hicho kimepanga kumuita Rostam katika mkutano wa Kamati Kuu (CC) uliopangwa kufanyika 30 Julai 2011 kwa lengo la kumwangukia. MwanaHalisi.

Nini kimejiri, amekubali kuhudhuria au kagoma tutaarifiane hapa jamvini.

Ikiwa Rostum atakubali ombi hilo la wanamagamba hakika yeye ndo atakuwa mwanasiasa uchwara kuwahi kutokea tangu kuundwa kwa msingi wa dunia hii..."

kwani Nape hayumo humo ndani?
nape ana kila sababu za kulinda chama kuliko kuwalinda wagombea 2015. pia yeye ndiye wa kuyatoa maamuzi nje. hawezi kuvujisha siri tena. cc imejaa wazanzibari. hao sio waropokaji kama wabara. kwasasa kupata habari za vikao vya cc itakuwa ngoma nzito. subirini nec huko mtapata watu wa kuvujisha siri.

nape ana kila sababu za kulinda chama kuliko kuwalinda wagombea 2015. pia yeye ndiye wa kuyatoa maamuzi nje. hawezi kuvujisha siri tena. cc imejaa wazanzibari. hao sio waropokaji kama wabara. kwasasa kupata habari za vikao vya cc itakuwa ngoma nzito. subirini nec huko mtapata watu wa kuvujisha siri.

Naona leo umewapumzikia chadema

Back
Top Bottom