Kamati kuu ya CCM trh 30.7.2011

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Taarifa kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinasema tayari chama hicho kimepanga kumuita Rostam katika mkutano wa Kamati Kuu (CC) uliopangwa kufanyika 30 Julai 2011 kwa lengo la kumwangukia. MwanaHalisi.

Nini kimejiri, amekubali kuhudhuria au kagoma tutaarifiane hapa jamvini.
 
Kama ni kwa ajili ya uchaguzi wa Igunga basi wamenoa. Kwa sababu ukiisha tu wanamtimua tena.
 
Hawana la maana hao! Magamba yamegoma kutoka sasa hawajui cha kufanya. Badala ya kuwaita waliogoma, wanamwita aliyetoka. Upuuzi mtupu!
 
Hapo ndiyo uzaifu wa CCM unapoonekana wazi,mtu alichajitoa sasa wanambembeleza wa nini?
 
wanamuita aje afanye nini wakati alishawaaga na hataki tena gutter politics!!.....
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hawana la maana hao! Magamba yamegoma kutoka sasa hawajui cha kufanya. Badala ya kuwaita waliogoma, wanamwita aliyetoka. Upuuzi mtupu!
Mkuu umesema kweli hawa jamaa siwaelewi wametaka ajiuzulu kafanya kama walivyotaka sasa wanamuita aje kufanya nini na kwa nini isiwaite waliogoma wawalazimishe?
 
Kwani ajenda ni kumjadili Rostamu au wale waliokataa kuachia ngazi baada ya siku 90??
 
Tunamwomba mkaanga sumu Nape athibitishe kama magamba yanabandikwa tena,sijuhi ni kwa solotepu ama supa gluu
 
Wengi tuko mbali, tunaomba taarifa nini kimejiri ktk kikao cha kamati kuu (CC) ya CCM, miongoni mwa hadidu rejea:

1. Jairo
2. Kujiuzulu kwa Rostam
3. Umeme
4. Sitta na wenzie kujiunga na CCJ
 
walikuwa wanalishana kiapo cha kuhakikisha bajeti ya ngeleja inapita kwa njia yoyote ile na walisema bora punda afe lakini mzingo ufike
 
5. Mafisadi waliobaki afta rostam azizi.
6. Tathimini ya hali ya Siasa ya chama (ccm) ndani ya bunge etc.
Tuvute subra!
 
Wengi tuko mbali, tunaomba taarifa nini kimejiri ktk kikao cha kamati kuu (CC) ya CCM, miongoni mwa hadidu rejea:

1. Jairo
2. Kujiuzulu kwa Rostam
3. Umeme
4. Sitta na wenzie kujiunga na CCJ

5. Mafisadi waliobaki afta rostam azizi.
6. Tathimini ya hali ya Siasa ya chama (ccm) ndani ya bunge etc.
Tuvute subra!

7. Marekebisho ya sheria ya maandamano, yafutwe kabisa bse ndio yaliyokifikisha chama hapa.

8. Mtu atakayereplace RA kupiga deal kwa ajili ya kupata mkwanja wa 2015

9. kwa kuwa tathamini inaonesha njia ya kura halali haitaturejeshea jimbo la igunga, njia gani mbadala za kutumia ili kulipata lile jimbo.

10. sababu tunazowapa TZ kuwa ndio chanzo cha tatizo la umeme, wameanza kuzishtukia kuwa ni feki, tu brain storm kupata visingizio vipya (hapa mwenyekiti atasisitiza, LAZIMA TUWE CREATIVE :) )
 
Back
Top Bottom