Kamanda Kamuhunda awageuka wakubwa...

mara nyingi majina huwa yanasadifu matukio katika maisha
mfano aliekuwa kamanda wa polisi DSM enzi hizo alikuwa anaitwa MAJI akaenda na maji kwa kutimuliwa
DR kafumu alifumuliwa,
kamuhanda kichaga cha rombo ni kumtoboa mtu kwa mkuki au mshale sasa aangalie asije akajitoboa mwenyewe kwa uongo wake
video ziko wazi,picha ziko wazi ukweli anaujua moyoni kuwa anajitetea kulinda wakubwa
Damu ya mwangosi lazima itamuhanda tu(kumtoboa popopote atakapokuwa)
 
Nafikiri kuna guidance ya namna ya kutekeleza order ndani ya majeshi yote. Ukipitiliza kwa sababu ya kukosa akili au kuleta ujuaji hilo ni tatizo lako.
 
Bora wangeliua li kamuhanda ambalo limemuua mwangosi bila hatia,wamemuua kamanda barlow wa mwanza ambae alikua anapambana kiukweli na mijambazi na jiji limetulia,mwanza wamepoteza kamanda mahirisana.
 
Jamani anatupa ushahidi ili atakapokwenda mahakama ya kimataifa ya mauaji isiwe vikugumu kuandaa ushahidi.
 
Huyu ni mjinga tu anataka kusema alipokea maagizo ya kumuua mtu asiye na silaha nae akatekeleza sasa nani mjinga zaidi yeye ama waliomtuma aue so stupid...
 
jua kwa kawaida huwaga teke wakati wa hasubui, na ndivyo ilivyo kwa serikali ya jk. sasa cjui aanze na lipi. la mwangosi au la ulimboka? na walimu haooo wanajiandaa kupika la kwao. jk cjui ataanza na lipi. 2angalie yaliyo saulika: Epa,Rich mond, Tanesco,Tucta. 2kiangalie upande wapili wa shilingi: kwa upande wapili huku kuna kuvuja kwa mitihani ya kidato cha nne.
 
kumwaga damu ya binamu yeyote aliyeumbwa na Mungu ni dhambi mbaya sana.na hiyo damu haipotei hv hv kazi wanayo
 
Hiyo ni kweli kabisa kaka. Kwani nakumbuka nikiwa nipo shule, nilienda kumtembelea shangazi yangu aliekuwa anaishi pale karibu na shule.Nikawa nimelala mimi na mwanae na Shangazi yangu, usiku jamaa akaondoka nikawa niko pekee yangu pale ndani. Kumbe jamaa alikuwa na msala kwa hiyo polisi wakaja kufanya arrest pale home kufika wanagonga mlango mimi nafungua jamaa akatupa kofi mimi nikawahi kukwepa Shangazi anakuja kuwaambia sio huyu jamaa wakaanza kuomba msamaha.HATUNA JESHI LA POLISI KWA SASA ILA NI GENGE LA WAHUNI WALIOKUSANYWA KWA KAZI YA KULINDA CCM.
 
Nimelisoma gazeti la Mwananchi Kamhanda anajigonga gonga sana kwa haya yafuatayo
kwanza anasema yeye hakuwepo sehemu ya tukio halafau hapohapo anatoka kusema kuwa wafuasi wa CHADEMA waliwavamia Polisi na kuwarushia mawe mpaka kofia zikapasuka, sasa aliwezaje kuyaona haya ilihali hakuepo eneo la tukio watu wanapolinda haki wanapokuwa kuwa waongo ujue nchi ipo hatarini, sasa polisi ndio wanaofanya majukumu ya kijambazi
 
Katika kumbukumbu zangu mikutano aliyofanya na waandishi wa habari siku hiyo kabla ya tukio na kauli kadhaa baada ya tukio alieleza kuwa anatekeleza maagizo kutoka kwa wakubwa wake, jaribu kuwa na kumbukumbu, kuna wakati nilikusudia kuanzisha uzi wa kauli hiyo ya Kamuhanda hapa.

Si jambo la kawaida RPC awepo kwenda tukio dogo kama lile la kufungua tawi kijijini, kuna sughuli nzito iliyokusudiwa kufanywa siku hiyo. Wenye kusoma hali hiyo waliishaiona mapema na ndio maana walitoa tahadhari kwa Dr. Slaa asiende huko kwenye tukio kwani aliyekudiwa wa siku hiyo huenda si Mwangosi, pale walimalizia hasira baada ya kumkosa waliyemdhamilia.

Hata polisi waliokuwepo pale hata Mkuu wa kituo cha Mafinga huenda alikuwa gizani, na polisi wa kuchomekewa walioandaliwa kwa shughuli maalum kufanya mauaji hayo. Niwape dondoo moja hapa chini:



Kwa tukio hilo ni kwamba Kamuhanda ndiye aliyeamrisha bomu lipigwe, kuna aliyeandaliwa kwa kazi hiyo ndiyo maana honi ile ilikuwa amri ya kuashiria kufanya kilichokusudiwa.
Ni kweli pale OCD alikuwa anatosha kabisa.Hiyo ni kutokana na level ya kata,however nakubaliana na dhana ya kwamba Slaa ndiye walikuwa wakimuwinda.
 
Wamemuua wakadhani wanamkomoa, mwenzao sasa amelala usingizi wa milele,hasikii maumivu wala uchungu wa maisha wao wapo macho wanahangaika na shida za dunia siku si nyingi nao watatamani wafe, damu ya Mwangosi haiwezi kukauka pale ilpomwagika bila haki kutendeka ni kiasi cha muda tu hata kama wanaichelewesha, taratibu wanaanza kuropoka na kunyoosheana vidole mwisho watararuana wenyewe kwa wenyewe.......Pumzika kwa amani Mwangosi raha ya milele Mungu akuangazie.
Sifongo imebidi ni comment, maneno mazito RIP wote waliokufa kwa unyanyasaji wa polisi wa CCM na utawala wao wa Magamba!
 
Yuko wapi Ditopile na jeuri yake yote sembuse Kamuhanda piga sala ya kutosha tu Mungu mjua yote atatenda lililojema malipo ni hapahapa
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, akiojiwa kamanda kamuhunda kuhusu kifo cha mwangosi alisema “Kazi yetu ni kutekeleza majukumu na maagizo tu na mimi niliyafanya hayo yote.”

Unaona, ngoma hiyo ameshaanza kuwatumia salamu waliomtuma ki aina kwamba alikuwa anatekeleza maagizo yao waliomtuma, hii inaweza kutoa jawabu la kwanini JK amekaa mbali sana na issue Mwangosi hasa kuhusiana na kitendo chake cha kukataakatakata kuunda tume huru ya uchunguzi.

Kkuhusu mengine amezungumzia kuwa gari lake lilikuwa mbali na eneo la tukio na kwamba polisi ilibidi watumie nguvu kujitetea kwani walirushiwa mawe na raia.

Yaani sijui Kamuhanda kama anajua kuwa kuna kitu kinaitwa video ambayo haisemi uongo pengine hajui kuwa tukio zima liko kwny youtube hata kipofu anaona kuwa hakuna jiwe lilorushwa na raia.

ningehuzunika sana kama ANGEULIWA KAMUHANDA,,,,,,haya yote nisingeyajua
 
jua kwa kawaida huwaga teke wakati wa hasubui, na ndivyo ilivyo kwa serikali ya jk. sasa cjui aanze na lipi. la mwangosi au la ulimboka? na walimu haooo wanajiandaa kupika la kwao. jk cjui ataanza na lipi. 2angalie yaliyo saulika: Epa,Rich mond, Tanesco,Tucta. 2kiangalie upande wapili wa shilingi: kwa upande wapili huku kuna kuvuja kwa mitihani ya kidato cha nne.

are u sure au unahisi tu??????
 
jua kwa kawaida huwaga teke wakati wa hasubui, na ndivyo ilivyo kwa serikali ya jk. sasa cjui aanze na lipi. la mwangosi au la ulimboka? na walimu haooo wanajiandaa kupika la kwao. jk cjui ataanza na lipi. 2angalie yaliyo saulika: Epa,Rich mond, Tanesco,Tucta. 2kiangalie upande wapili wa shilingi: kwa upande wapili huku kuna kuvuja kwa mitihani ya kidato cha nne.
nahisi wewe ni teeneger
 
Sasa ulifikiri jeshi lolote mafunzo yao makubwa ni nini? ni kutekeleza majukumu na maagizo tu.

Halafu unayapika utafikiri kuwa hilo ni ajabu na kumbe ni kawaida ya majeshi yote duniani.


Kiwanda at work.
 
Watajidai kufungua kesi ili asiende kule The Hague. Hapo tutatoa mifano ya akina Kombe na hawa majaji wa darasa la 12 ili tugomee mahakama za CCM.

Wao waende tu tena ikiwezekana labda hata huyu msanii wa ikulu aitwe kuonyesha burudani mahakamani.
 
Aiseeee babaangu kimenuka damu ya mwangosi inaanza kuwatafuna watu wataanza kuwa wehu sasa ivi
 
Back
Top Bottom