Kweli mkuu hata mimi nikichangia sredi ya awali jioni,nimekumbuka kwamba huyu Kamanda aliongoza mauaji mengine Songea. Kwasababu hakuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu,matokeo yake tumeyaona tena leo. Ni jukumu la Waziri na IGP kujiuzulu angalau kuonyesha huzuni yao kwa kitendo hiki cha aibu kwa Taifa letu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda Baada ya kuua raia waliokuwa katika maandamano ya amani huko songea - Ruvuma hivi karibuni, amehamishiwa Iringa ambako ameua Mwenyekiti wa mwandishi wa habari akiwa kazini na vifaa vyake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda akizungumza na wanahabari leo
kuhusu sababu za kuzuia mkutano wa Chadema leo Mufindi
Tumejipanga kwa lolote asema kamanda wa polisi kuwa si Chadema pekee hata CCM na vyama vyote marufuku mikutano wanaruhusiwa kufanya vikao vya ndani ili kupisha zoezi la sensa hadi jumamosi litakapomalizika
Jina la Michael Kamuhanda nilipolisikia tu nilihisi kama nimewahi kulisikia tena siku si nyingi. Nina uhakika na wengine wamelikumbuka pia kuwa ndiye aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Ruvuma ambapo mapema mwaka huu (Februari) wananchi 4 waliuawa napolisi walipokuwa wakijaribu kuandamana kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Natamani wamlete Dar-es-Salaam pia ili watu waelewe tatizo tulilonalo. Nikimuita ni mhalifu sijui kama nitakuwa nimetia chumvi sana... haiwezekani ndani ya mwaka mmoja kamanda unasimamia mauaji ya raia kisa wanataka kuandamana tu! Hivi hana mbinu nyingine zozote kichwani mwake zaidi ya kuwa trigger happy!
Mzee Mwanakijiji hii ishu ya police kutumia nguvu na kuua raia kwenye mikutano ya CHADEMA ni trap. Na viongozi wengi wa CHADEMA wamefall into that trap. Kwangu mimi naona ni kama mkakati unaosukwa kwa ajili ya kuiangamiza kabisa hiki chama na kuipoteza kwenye ramani ya politics.