Kama wewe ni mgeni Shinyanga mjini, usilale Buchosa guest house inafuga vibaka na majambazi

kigogo1ivi

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
534
323
Mimi yamenitokea pale Buchosa nilipofika Shinyanga katika tafuta tafuta guest nikajikuta nimedondokea pale. Tokea nilipoingia pale ndiyo nikaanza kuona vituko wakina dada zaidi ya kumi wamechukua chumba kimoja na wanapishana kuleta wanaume kibaya zaidi ilipofika usiku wa saa 8 nikiwa nimelala nilianza kugongewa mlango na watu wasiojulikana wakitaka niwafungulie eti wamesahau begi lao chumbani kwangu nilikuwa mbishi ila wakawa wanagonga kwa nguvu ili uvunjike ndiyo nikavuta kitanda na kukiweka mlangoni baada ya kuona mlango umekuwa mgumu wakaondoka.

Kilichonishangaza hata muhudumu hakuwepo, Kulipokucha nikamweleza mmiliki wa hiyo guest yake haina vitu kama ivo lakini watu wengine ndiyo wakaniambia kuwa yeye ndiye hushirikiana na vibaka kuibia wateja wake hasa ukionekana una kitu cha thamani.

Kwahiyo BUCHOSA siyo nyumba yakulala wageni bali ni nyumba ya kulala vibaka.
 
Duh pole sana mkuu na asante kwa kutupa taarifa mi shinyanga nkilala huwa nalala empire ipo mazingira au karena motel mara chache lakin hiyo ipo mbali na town
 
Ipo majengo ni jirani sana kuliko karena motel pia gjarama yake nafuu kidogo kwa watu kama sisi wa hari ya chini
 
Shinyanga kuna hotel/guest nyingi tu ambazo ni nzuri. Ukifika shinyanga uliza KARENA, VIGIMARK, MASU, MALAIKA, FM LODGE, EMPIRE, MAKONDA, SUMAYE, LA' FAMILIA, MAKOA, hizi hazina upuuzi kama huo.....
 
ndiyo sababu ya kuweka upuizi wa hiyo nyumba ili watu wasije ingia mkenge kama mimi
 
Mimi yamenitokea pale Buchosa nilipofika Shinyanga katika tafuta tafuta guest nikajikuta nimedondokea pale. Tokea nilipoingia pale ndiyo nikaanza kuona vituko wakina dada zaidi ya kumi wamechukua chumba kimoja na wanapishana kuleta wanaume kibaya zaidi ilipofika usiku wa saa 8 nikiwa nimelala nilianza kugongewa mlango na watu wasiojulikana wakitaka niwafungulie eti wamesahau begi lao chumbani kwangu nilikuwa mbishi ila wakawa wanagonga kwa nguvu ili uvunjike ndiyo nikavuta kitanda na kukiweka mlangoni baada ya kuona mlango umekuwa mgumu wakaondoka.

Kilichonishangaza hata muhudumu hakuwepo, Kulipokucha nikamweleza mmiliki wa hiyo guest yake haina vitu kama ivo lakini watu wengine ndiyo wakaniambia kuwa yeye ndiye hushirikiana na vibaka kuibia wateja wake hasa ukionekana una kitu cha thamani.

Kwahiyo BUCHOSA siyo nyumba yakulala wageni bali ni nyumba ya kulala vibaka.

taarifa zako nilizisikia.. Nakushauri acha kuchafua biashara ya watu, hakuna mmiliki wa hotel ashirikiane na vibaka kuibia mteja.. Uliyeongea nae kwanza si mmiliki ni meneja wa gest.. Pili hiyo gest wapo kinadada wanaojiuza wamepanga hapo, na ndicho kilichokupeleka wewe ukae nao karibu.. Hilo ni jambo la kawaida kwa miji yote.. Tatu, Buchosa ipo uswahilini sana, wewe mgeni umefikaje kama si kuuliza watu sehemu ya dadapoa ukaishi.. Kama gesti cheap, Shinyanga zipo mamia zaidi ya hiyo, ila bado ulipenda pale.. Nne, kuhusu kugongewa usiku, kumbuka ile gest biashara kubwa ni short time so mtu anaingia na kutoka halali, we ukapenda kuweka kambi.. Mtu aliyekuwa mchana kasahau saa yake; ni dhambi kukugongea aichukue ili asubuhi usiondoke nayo????

Nb: ukiwa mgeni mahala uliza sehemu ya matakwa yako sio kuvamia tu na kuishia kutoka povu Jf huku ukichafua biashara za watu.. Vipi ulienda polisi au umbea uliosikia umetimiza haki yako ya msingi???
 
Back
Top Bottom