Kama wewe ni mgeni Shinyanga mjini, usilale Buchosa guest house inafuga vibaka na majambazi

Shinyanga kuna hotel/guest nyingi tu ambazo ni nzuri. Ukifika shinyanga uliza KARENA, VIGIMARK, MASU, MALAIKA, FM LODGE, EMPIRE, MAKONDA, SUMAYE, LA' FAMILIA, MAKOA, hizi hazina upuuzi kama huo.....

Mwandu Hotel, Kibondo Guest, Malekos Guest, Liga Hotel, na Dami Hotel
 
Hata hapa kibaha huo mchezo upo mgeni wangu alilala Qman bar, akapuliziwa madawa ya usingizi wakampiga laki nne, cha kusikitisha polisi alipofika pale mhudum akajifungia kaunta,mwenye hoteli akadai yuko safali, ikala kwetu
 
Asante mkuu kwa taarifa,haya majumba mengine ya kulala wageni ni majanga tu..tumekusikia tutachukua hatua stahiki once tukitia maguu Shinyanga!
 
taarifa zako nilizisikia.. Nakushauri acha kuchafua biashara ya watu, hakuna mmiliki wa hotel ashirikiane na vibaka kuibia mteja.. Uliyeongea nae kwanza si mmiliki ni meneja wa gest.. Pili hiyo gest wapo kinadada wanaojiuza wamepanga hapo, na ndicho kilichokupeleka wewe ukae nao karibu.. Hilo ni jambo la kawaida kwa miji yote.. Tatu, Buchosa ipo uswahilini sana, wewe mgeni umefikaje kama si kuuliza watu sehemu ya dadapoa ukaishi.. Kama gesti cheap, Shinyanga zipo mamia zaidi ya hiyo, ila bado ulipenda pale.. Nne, kuhusu kugongewa usiku, kumbuka ile gest biashara kubwa ni short time so mtu anaingia na kutoka halali, we ukapenda kuweka kambi.. Mtu aliyekuwa mchana kasahau saa yake; ni dhambi kukugongea aichukue ili asubuhi usiondoke nayo????

Nb: ukiwa mgeni mahala uliza sehemu ya matakwa yako sio kuvamia tu na kuishia kutoka povu Jf huku ukichafua biashara za watu.. Vipi ulienda polisi au umbea uliosikia umetimiza haki yako ya msingi???

Usimwandame mtoa uzi, amepata kadhia ndo maana kutupa angalizo. Hata kama ipo uswahilini sana huo ndo uwezo wake. Eg kama bosi kampa tsh 15, kujikimu kwa siku unadhani atamudu karena au virgmark? La hasha, ila kuna hotel za bei nzuri eg tsh 7, na zina usalama.
 
Mwoleka imechoka ni ya kizamani sana! Katemi ni nzuri iko mwisho ngokolo na Dami iko town kabisa Rwegisora srt!! Ila hadi Ibinzamata kuna hotel!! Nzur tu
Halafu kule ngokolo kulikuwa na shinyanga by night sijui bado ipo?Butiama club je bado ipo?
 
Du iyo too much hata kuvuka daraja la kigamboni haitoshi. Nasikia likikamilika tutakuwa tunavuka kwa hera. Kama huwezi ogelea.

duuh acha utani mkuu Hunyu! vingnevyo basi kigamboni wataishi wazee wa escrow tu, sisi nani kajamba tutakomea pale magogoni penye shombo la vibua!
 
Last edited by a moderator:
duuh acha utani mkuu Hunyu! vingnevyo basi kigamboni wataishi wazee wa escrow tu, sisi nani kajamba tutakomea pale magogoni penye shombo la vibua!

Hahaa ngoja tumuulize mzee wa mabarabara
 
Last edited by a moderator:
Gesti za buku 3 hizo,ukiingia lazima uingie na jibwa la kipolisi au begi lililosheheni silaha za maangizi.
 
taarifa zako nilizisikia.. Nakushauri acha kuchafua biashara ya watu, hakuna mmiliki wa hotel ashirikiane na vibaka kuibia mteja.. Uliyeongea nae kwanza si mmiliki ni meneja wa gest.. Pili hiyo gest wapo kinadada wanaojiuza wamepanga hapo, na ndicho kilichokupeleka wewe ukae nao karibu.. Hilo ni jambo la kawaida kwa miji yote.. Tatu, Buchosa ipo uswahilini sana, wewe mgeni umefikaje kama si kuuliza watu sehemu ya dadapoa ukaishi.. Kama gesti cheap, Shinyanga zipo mamia zaidi ya hiyo, ila bado ulipenda pale.. Nne, kuhusu kugongewa usiku, kumbuka ile gest biashara kubwa ni short time so mtu anaingia na kutoka halali, we ukapenda kuweka kambi.. Mtu aliyekuwa mchana kasahau saa yake; ni dhambi kukugongea aichukue ili asubuhi usiondoke nayo????

Nb: ukiwa mgeni mahala uliza sehemu ya matakwa yako sio kuvamia tu na kuishia kutoka povu Jf huku ukichafua biashara za watu.. Vipi ulienda polisi au umbea uliosikia umetimiza haki yako ya msingi???

Je mlimtahadharisha kigogo1ivi na kumwambia kuwa hiyo hotel ni ya mapimpi kama wewe? Kama mnawafuga hao wakidada wawafanyie bishara na sio ya kulala kwa nini mlimkubalia na kummpa chumba mpaka asubuhi? Na huwezi kumchagualia mtu sehemu ya kulala au kupanga hata kama hiyo hoteli ipo juu ya mti. Samahani kaka jamabazi kama nimekukwaza. Siku nyingine wakija wateja au wageni wakichukuwa chumba muwaambie kuwa sio sehemu ya kulala mpaka asubuhi kwa kuwa mnafanyabiashara ya kuuza wakinadada, mteja haruhusiwi kulala mpaka asubuhi.
 
next time kalale empire lodge...lakini ufanye booking mapema au makoa motel, sehemu hizo mbili huwezi kusikiawala kuon issue hizi.

Makoa ni poa sana ,nimelala mara nyingi hapo na zipo Makoa kama mbili hivi hapo karibu na stand,ukiona guest ni buku 5,kuna akina dada poa na haina vitasa imara basi geuka haraka sana afadhali ukalale kwenye benchi la kupokea wageni polisi au hospitali mkuu.
 
Back
Top Bottom