Kama Unalalamika Biashara Ni Ngumu, Bado Hujajua Mbinu Hii Rahisi Ya Kuendesha Biashara Yako

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Kwenye makala ya jana tuliona kuna njia kuu mbili za kuendesha biashara yako. Tuliona kuna njia rahisi ya kuendesha biashara na kufikia mafanikio na pia tuliona kuna njia ngumu ya kuendesha biashara na kufikia mafanikio. Na pia tuliona tofauti ya njia hizo mbili na ufanyeje ili uweze kuendesha biashara yako kwa mafanikio.

Ni kweli kabisa kwamba biashara sio rahisi, biashara inahitaji umakini, biashara inahitaji kujitoa na biashara inahitaji kujali. Lakini kuna njia rahisi na mbinu rahisi za kuendesha biashara yako. Kwa mfanyabiashara yeyote makini kama ulivyo wewe ni lazima azijue mbinu hizi ili aweze kufikia mafanikio kupitia biashara.

Unapoingia kwenye biashara, na hata kama upo kwenye biashara kwa sasa na unataka kuleta mabadiliko, leo utajifunza kitu kimoja kikubwa sana cha kufanya ambacho kitageuza biashara yako kwa kiasi kikubwa sana.

Kitu kikubwa cha kwanza kabisa kufanya kwenye biashara yako ni kupata mteja wa bidhaa au huduma unayotoa. Jitengenezee mbinu ambazo zitaweza kumshawishi mteja kununua kutoka kwako, halafu ukishapata mteja mmoja tu, tayari umefikia mafanikio. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu sasa hivi utatumia mbinu ile uliyotumia kupata mteja wa kwanza kupata mteja mwingine wa pili na wa tatu na wa nne na hatimaye una wateja wengi kuliko ulivyokuwa unafikiri.

Ndio sio rahisi kama ulivyosoma hapo, ila ni kitu kinachowezekana, hasa kama utakuwa tayari kujifunza na kutoa huduma nzuri kwa wateja wako.

Sasa kama ninaanza na mteja mmoja, halafu nikimaliza nitafute wa pili nitafikia wateja wengi lini? Swali zuri sana ambalo unajiuliza na linakuumiza kichwa.

Jibu ni kwamba hiyo sio kazi yako kwa sasa, bali itakuwa kazi ya wateja wako. Yaani wewe jukumu lako ni kuwafanya wateja wako wa sasa waende kuwaambia wateja wengine na wengine ili nao waje kupata bidhaa au huduma kwako.

Sasa ni nini kitawafanya wateja wako waende kuwaambia wengine?

Kitu rahisi sana, utawashangaza. Ndio utawashangaza kwa kuwapa huduma ambayo hawajawahi kuipata sehemu nyingine yoyote. Utawapa huduma bora sana. Watategemea kupata kitu X kutoka kwako ila wakija wanatona na kitu X + Y, yaani kuna kitu cha ziada wameondoka nacho.

Sasa kwa ilivyo asili ya binadamu, yeyote anayeshangazwa huwa hataki kushangaa peke yake, bali atataka kuwashangaza ndugu zake, jamaa zake na hata marafiki zake. Hivyo atamwambia kila anayekutana naye jinsi ambavyo ameshangazwa. Akikutana na mtu mwenye tatizo kama alilokuwa nalo yeye hatosita kumwambia nenda kwa fulani, tatizo lako litakwisha, na utapata cha ziada pia.

Bado unasema biashara ni ngumu? Tupigie kwenye 0713 666 445 utuambie ni eneo gani la biashara yako linakuwa gumu sana kwako na tutakupa mbinu bora za kulitatua.

TUPENDE BIASHARA, NDIO MKOMBOZI WETU PEKEE.
 
Hii aina ya biashara uliyoieleza ni ya 'Network Marketing'.Ni aina ya biashara ambayo ninataka kuifanya ila bado naifanyia tafiti ili nikianza nisikwame.Ila umeielezea katika 'Simple language'.Aksante Sana.
 
Mi nimeelewa tofauti kidogo na wewe atatusahihisha mwanzilishi. Ni biashara yoyote ya kawaida sema ishu ni kutoa huduma bora ambayo/zo kwa kawaida wengine hawatoi kwa namna yako ili mteja aone tofauti ya huduma yako na zile alizozizoea. Kwa kawaida mteja akiridhishwa na huduma huwa anakusaidia kukutangaza kwa kuwaeleza watu wake wa karibu namna alivyohudumiwa.
 
Hata mimi nimeelewa hivyo hivyo kama wewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom