Kama umesahau password windows xp

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
UMESAHAU PASSWORD WINDOWS XP ?

Kama wewe umewahi kupoteza au kusahau password yako ya kulogin kwenye windows xp ukashindwa kutumia kwa njia moja au nyingine somo hili fupi litakufaa sana kama ukilifuatilia ukaelewa .

Kabla ya kwenda kwenye somo lenyewe , kuna jambo moja unatakiwa ujue watumiaji wa kawaida wa computer huwa wanaweka password kwenye computer zao na kusahau administrator , njia rahisi ya kuweza kuingia kwenye administrator ni unapowasha computer yako bonyeza f8 unaweza kwenda katika safe mode hapo utaweza kuingia kwenye account ya administrator ambayo ina mamlaka ya kukusaidia kuondoa password ya account nyingine ambayo ndio password yake imepotea au kubadilishwa hii inawezekana tu endapo mtu alisahau kulock administrator .

Kama administrator nayo imekuwa locked kwa password , basi unaweza kufuata maelezo hapo chini ambayo ni ya uhakika zaidi kama computer yako haina matatizo mengine yoyote yale .

1 - Ingiza cd yako ya windows Xp katika CDROM ambayo ni bootable , hakikisha kwenye bios yako umebadilisha iwe inaboot to CDROM au first boot iwe CDROM , kama unacomputer aina ya dell hauhitaji kwenda kwenye bios unabonyeza f12 kisha unaweza kuchagua kuboot na CD.

2 – Angalia kwenye kioo cha computer vizuri utaona maneno yaliyoandikwa ( press anykey to boot from cd ) ina maanisha bonyeza key yoyote kwenye keyboard yako ili uweze kutumia cd ya windows xp iliyomo ndani ya cdrom , kumbuka kuna wakati unapobonyeza keys inaweza isifanye kazi kama computer yako imeingiliwa na aina Fulani ya virus ambaye analock keyboard yako , kwahiyo unachotakiwa ni kubadilisha kama unatumia PS2 tumia Usb Utaweza kufanya hicho kitu .

3 - Ukisha bonyeza hizo keys utaona maneno mengine SETUP IS INSPECTING YOUR SYSTEM AND LOARDING FILES .

4 – Halafu utaona Screen iliyoandikwa WELCOME TO WINDOWS SETUP bonyeza ENTER Ili iendelee kusetup .

5 – Kisha Utaona maandishi LICENCE AGREEMENT bonyeza f8 kukubali

6 - Utaona Setup Screen nyingine bonyeza R ili uweze kufanya repair , kama una operating system zaidi ya moja tafadhali chagua moja ambayo ndio umepoteza password yake .

7 – Kwahiyo Computer itaanza kurepair, inachofanya kwenye hatua hiyo ni kuondoa baadhi ya files za kwenye system na kuweka nyingine kisha computer ita restart .

8 – Ikiwaka tena angalia katika hatua ambazo zitajiandika angalia hatua ya kwanza inayosomeka INSTALLING DEVICES bonyeza SHIFT NA F10 .
9 – Kuna Screen ndogo itafunguka andika NUSRMGR.CPL Kisha bonyeza ENTER utaona Account zako zote zilizokwepo kwenye computer hiyo hapo sasa unaweza kubadilisha password .

10 – Ukishamaliza funga hiyo Box kisha Exit endelea na vingine vitakavyokuuliza kama kuweka product key ya computer yako na maelezo mengine ikishamaliza basi utaweza kutumia password nyingine ambayo ulibadilisha kwenye hatua ya 9 .

Kumbuka Files zako na programu nyingine katika computer yako hazitobadilika au kupotea .

Yona F Maro
www.askmaro.blogspot.com
Monday, September 28, 2009
 
Nita upload kwenye moja ya domain zangu ili uweze ku download kwasababu download site kama rapidshare au mediafire hazi ruhusu ku upload files zaidi ya 100MB

kumbuka hii ni image file lazima uwe na software yakufungulia images kama vile Poweriso, Magiciso au InfraRecorder ili uweze kuburn hiyo image file.

Mimi binafsi huwa napendelea kutumia InfraRecorder kwasababu ni rahisi.
 
Last edited:
Chamoto

mambo vp sasa naomba ile Video iliyokuwa kwenye you tube unipe kwenye Download nyingine kama DAP
 
UMESAHAU PASSWORD WINDOWS XP ?

Kama wewe umewahi kupoteza au kusahau password yako ya kulogin kwenye windows xp ukashindwa kutumia kwa njia moja au nyingine somo hili fupi litakufaa sana kama ukilifuatilia ukaelewa .

Shy,

Mara zote kumbuka ku - acknowledge the author/source! Hata kama umetafsiri kwa Ki-ha

Siku Njema
 
Ukiona imetolewa sehemu nyingine ni vizuru wewe utoe hiyo source unaonaje wewe ukiwa wa kwanza
 
Back
Top Bottom