Kama umekutana na shida ya kusaidia au kusaidiwa pita hapa

kocha Nabi

JF-Expert Member
Feb 1, 2022
590
1,467
Suala la kumsaidia mtu au watu katika maisha ni jambo la kawaida kwa wanadamu, yaani ni kawaida kwa wanadamu kusaidiana.

Kuna baadhi ya watu tendo la kumsaidia mtu au kitu kwao ni kama tendo la ulazima, kwani hata ujizuie vipi lakini msukumo unaotoka moyoni ni mkubwa.

Msukumo huo unaweza kusababishwa na:

-Imani
-Ukaribu wa mtu unayemsaidia au kitu
-Mazingira yaliyomkuza msaidiaji
-Asili ya mtu/jinsi alivyozaliwa

Suala la msaada sio sheria kwamba ukihitaji msaada ni lazima usaidiwe, ama usiposaidiwa na ndugu/rafiki basi na mahusiano yenu iwe kazini au popote pale basi yafe. la hasha! msaada ni hiari ya mtu.

Kuna mda mtu unaweza kuona kabisa mtu fulani ana uwezo wa kunisaidia lakini haufahamu ni kiasi gani utaharibu utulivu wake, utaratibu/mipango yake ya maisha. Inategemea na aina ya msaada.

Usithubutu kutoa msaada ambao unajua/ unafahamu kwamba unaweza kukuumiza aidha kiakili, kiuchumi, ama kwa namna yoyote ile ili kumfurahisha unayempa msaada.

Kuna mda inaweza kukupata hali ya wewe kumsaidia mtu na wewe ikakugharimu maisha yako au maendeleo yako, unaweza kumsaidia huyo mtu kama utajiridhisha kuna uhakika wa wewe kusaidiwa kurudi katika hali yako ya zamani.

Kumsaidia mtu isiwe kigezo cha kumdidimiza katika kuinuka kwake, usiwe na wivu baada ya yeye kufanikiwa kupitia msaada wako, wala msaada wako usiwe njia ya wewe kujipatia haki kwake kwa kila jambo.

Pia usiwe mtu wa kupenda sana misaada kwani roho za binadamu zinatofautiana, watu wengi hutoa msaada huku wakiwa wanafatilia majibu ya huo msaada, wachache sana wanatoa msaada na kupotezea. jambo la kufatiliwa linaweza kukurudisha nyuma kiimani au kimaendeleo kutegemeana na msaada husika.

Toa msaada pale ambapo moyo wako unakusukuma kusaidia, hii hupelekea kuwa na furaha ya moyo pale unapomsaidia mtu na kuona kuna mafanikio kupitia huo msaada.
 
Back
Top Bottom