matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,653
- 15,481
Wasalaam.
Kwa sababu ya uhaba wa umeme, maji safi, uwezekano wa ajali, na magonjwa ya kushtukiza na kujisababishia wabongo wengi wamekata tamaa na wanaishi kana kwamba sekunde yoyote anakufa.
Hii imepelekea ufisadi, wizi, ujanjaujanja na ukosefu wa mipango mikubwa endelevu maana watu wanajua watakufa muda wowote na wanaowaacha watafaidi.
Utafiti wa kisayansi unaonyesha mapinduzi makubwa ya kisayansi na AI yanakusudiwa kupunguza uwezekano wa kufa kuliko miaka ya zamani. Chanjo, kinga na mapinduzi ya kidaktari nayo ni kichocheo.
Mfano mwla 1999 nilishuhudia mtu anaaanza kukohoa kikohozi cha kwanza hadi anakohoa cha mwisho akiaga dunia akiwa na kilo zisizozidi kumi kwa shambulizi la HIV.
Sasa hivi ukikutwa hivyo, nitakupiga kofi nikumalizie maana ni uzembe na matumizi mabovu ya uvumbuzi wa kitabibu. Nimeona mtu anatoka kwenye hali ya semiskeleton na leo ni bonge hafikirii kifo kwa matibabu ya kisasa.
Yote haya lengo langu ninini? Ni kutaka ujiulize ikiwa utapewa uchague miaka mingapi uishi ili ufe kifo cha asili, unangechagua miaka mingapi?
Binafsi huwa namwambia Mungu ikimpendeza anipe 120, ambayo nimeikata katika vipindi vya miaka 20 kwa 20. Akiruhusu anisaidie kitu cha pili ndani ya kipindi hicho niwe nimesaidia watu Bilioni nane wampende na kuishi sawsawa na mapenzi yake hasahasa wazungu.
Ukipewa uchague uishi miaka mingapi utachagua kuishi mingapi na utaifanyia nini?
Ni hayo tu.
Karibuni.