Kama TLS watachagua mwanasiasa itakuwa ndio mwisho wa uhusiano wa serikali na TLS

Wanasheria mnajidharirisha sana. Badala ya kuchagua anaefaa mnaangalia ukada.
 
TLS inamchagua wakili kuwa kiongozi wao,,,,,,,,,,Kwa hiyo keep quite
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wewe yehodaya sijajua kama labda unazo kumbukumbu za marais wa hicho chama na vyama vyao vya kisiasa waliotangulia. Ninyi ni miongoni mwa wanufaika wa uongozi mbovu wa tls sasa mmebaki kuhangaika. Ilimradi Lissu siyo mkenya wala mkongomani acha awe rais awanyooshe na soon bunge litakuwa mubashara kwa nguvu ya sheria.
 
Yaani watu wengine mnasikitisha mnoo kwa hoja zenu za ajabu, mimi ni wakili na tangu niwe wakili wala sijawahi kuona jambo lolote la maana ambalo serikali inafanya kwa ajili ya mawakili wa TLS.

1. Kuchagua majaji, jaji ni lazima awe mwanasheria na wanasheria ni wengi na sio kila mwanasheria ni mwanachama hai wa TLS, wakitaka majaji wanaweza kuchagua kutoka katika mawakili wa Serikali ambao wengi wao sio wanachama hai wa TLS.

2. Kushika nyadhifa za serikali, umefanya utafiti ni mawakili wangapi ambao ni wanachama hai w TLS na wameteuliwa katika nyadhifa za serikali? Inasikitisha sana kuona unajenga hoja ya wanaTLS wajipendekeze ili wapewe vyeo.

3. Chama kingine cha siasa, nakushauri usome sheria iliyoanzisha Tanganyika Law Society

Tanganyika Law Society | Law Association or About TLS | Tanganyika Law Society

4. Kuna nguvu kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani, unasikitisha kwa hoja za hovyo kama hizi, tambua kuwa TLS haijaanza leo wala jana, ni bahati mbaya tu wakati huu viumbe wengine wanataka kufanya siasa kila sehemu kwa faida zao binafsi.

Siasa ni nzuri kama inafanywa kwa uwazi na nia njema, lakini siasa inakuwa mbaya kama inafanywa kwa kukandimiza wengine.
mkuu ubarikiwe
 
...kwa hiyo ni rukhsa kwa wana ccm kuchaguliwa kwenye nyadhifa mbalimbali nchi hii lakini si wanasisa wengine eh??

..hivi hii nchi mmefanya duka lenu?.. nyo.ko we...

...mwaka huu mtashindwa....na karata yenu ya ujaji itashindwa....tumewachoka dhalimu nyie...
 
Yani zile priorities walizokuwa wakipata wasahau.....ni jukumu lao sasa kusuka ama kunyoa.

Asiyesikia la mkuu....

Mimi kura yangu tayari nmeishatangaza hadharani simpi Lisu au Masha. Kuwapa watu hawa ni sawa na kukifanya chama cha TLS kuwa kamati ndogo ya chademaa jambo ambalo hatuwezi kukubali.

Lilobadilika hapa ni uongozi TLS ilikuwepo toka enzi za ukoloni na walivumilia uwepo wake. Maraisi wote waliopita waliweza kufanya kazi na TLS na hapakuwa na tatizo lolote. Uongozi wa sasa haupendi kufuata sheria na wanaona zinawazuia kuongoza kwa vichwa vyao na kwa hisia zao. Ndio maana walikataa hata katiba. Hilo ndio tatizo la msingi lilotuleta kwenye hili. Wengi wao wanapenda kutenda na kutendea watu wanavyojisikia. hawataki kufuata katiba, sheria wala taratibu ambazo cha ajabu ziliwekwa na chama chao wenyewe. Halafu hizo priorities unazosema si hisani. Ni sheria wala si favour. Inayoleta siasa kwenye uchaguzi huu ni chama tawala ambacho kinafanya upinzani kuwa ni uadui. Juzi mtu anasema hadharani kuwa kumtembelea mpinzani ni usaliti. Yaani unapandikiza chuki wazi wazi na hadharani si sawa. Tukatae hili. Lilitokea Zanzibar na tuliona matokeo yake. Bado hatukujifunza kitu.
 
TLS ni chama cha kitaalamu.Na kinatakiwa kibaki hivyo.Wakichagua wanasiasa itakuwa ni mwisho wa serikali kushirikiana na TLS NA HATA KUCHAGUA majaji na mawakili mbali mbali kutoka TLS kushika nyadhifa serikalini na kwenye vyombo vya kimataifa.SABABU KITAKUWA ni chama kingine cha siasa kama CHADEMA NK.

Kuna nguvu kubwa kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani.Tundu LISU ANATUMIKA tu kwenye hiyo agenda lengo likiwa kuifanya TLS iwe chama cha upinzani kisicho na hati ya kuandikishwa.
JE NIN NANI MGOMBEA ASIYE MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE HAPA TANZANIA? TUANZIE HAPO KWANZA
 
TLS ni chama cha kitaalamu.Na kinatakiwa kibaki hivyo.Wakichagua wanasiasa itakuwa ni mwisho wa serikali kushirikiana na TLS NA HATA KUCHAGUA majaji na mawakili mbali mbali kutoka TLS kushika nyadhifa serikalini na kwenye vyombo vya kimataifa.SABABU KITAKUWA ni chama kingine cha siasa kama CHADEMA NK.

Kuna nguvu kubwa kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani.Tundu LISU ANATUMIKA tu kwenye hiyo agenda lengo likiwa kuifanya TLS iwe chama cha upinzani kisicho na hati ya kuandikishwa.
.Chama cha siasa tena?kwani wao wanachama wengine watakuwa wanamuangalia tu huyo Lisu akiwa anafanya kiwe cha siasa.Jaribu kuwa na upeo wa kufikiria.Kila mtu anahaki sawa ya kugombea cha msingi uwe na vigezo tu basi,hayo mengine tuwaachie wenye chama waamue wenyewe msiwafanye nyie ndio mabingwa wa kuwaamulia wayatakayo.
 
Yani zile priorities walizokuwa wakipata wasahau.....ni jukumu lao sasa kusuka ama kunyoa.

Asiyesikia la mkuu....

Mimi kura yangu tayari nmeishatangaza hadharani simpi Lisu au Masha. Kuwapa watu hawa ni sawa na kukifanya chama cha TLS kuwa kamati ndogo ya chademaa jambo ambalo hatuwezi kukubali.
Priorities zipi hizo??

Huu ukondoo wenu ni huko huko CCM msituambukize unafiki na kujipendekeza kibashitebashite.
 
TLS ni chama cha kitaalamu.Na kinatakiwa kibaki hivyo.Wakichagua wanasiasa itakuwa ni mwisho wa serikali kushirikiana na TLS NA HATA KUCHAGUA majaji na mawakili mbali mbali kutoka TLS kushika nyadhifa serikalini na kwenye vyombo vya kimataifa.SABABU KITAKUWA ni chama kingine cha siasa kama CHADEMA NK.

Kuna nguvu kubwa kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani.Tundu LISU ANATUMIKA tu kwenye hiyo agenda lengo likiwa kuifanya TLS iwe chama cha upinzani kisicho na hati ya kuandikishwa.
braza acha blah blah ngenyosha maelezo kabisa kuwa wakichagua mwanasiasa wa mlengo wa upinzani yani mwanachama wa upinzani. Kwani hata waliokuwepo ni wanachama pia wanasiasa wa chama tawala.
 
Kuna nguvu kubwa kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani.Tundu LISU ANATUMIKA tu kwenye hiyo agenda lengo likiwa kuifanya TLS iwe chama cha upinzani kisicho na hati ya kuandikishwa.

Hapo kwenye red ni dalili tosha kuwa pumzi imekata na mgonjwa huenda tusiwe naye tena !!!!!!
 
TLS ni chama cha kitaalamu.Na kinatakiwa kibaki hivyo.Wakichagua wanasiasa itakuwa ni mwisho wa serikali kushirikiana na TLS NA HATA KUCHAGUA majaji na mawakili mbali mbali kutoka TLS kushika nyadhifa serikalini na kwenye vyombo vya kimataifa.SABABU KITAKUWA ni chama kingine cha siasa kama CHADEMA NK.

Kuna nguvu kubwa kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani.Tundu LISU ANATUMIKA tu kwenye hiyo agenda lengo likiwa kuifanya TLS iwe chama cha upinzani kisicho na hati ya kuandikishwa.

" Kuna nguvu kubwa kutoka mataifa ya nje kuifanya TLS iwe chama cha upinzani."

Ifike wakati muache upuuzi jamani, muwe na aibu, visingizio hivi mpaka lini, mataifa gani ya nje?
 
Back
Top Bottom