Kama ni kweli hawa wasanii wanapelekwa Dubai kwa mission maalum Dubai Port, hakika inafikirisha!

Watanzania wenzangu hatima ya ustawi wa Taifa letu upo mikononi mwetu. Ni wajibu wetu kama Watanzania tujizuie kwa namna yeyote ima kununuliwa ama kushawishiwa kwa namna yeyote ile ilmradi tuligawe Taifa na rasilimali zetu.

Safari za namna hiyo za watu maarufu na wasanii wetu kwenda huko Dubai kwa nyakati za SINTOFAHAMU kubwa ihusuyo bandari yetu na wao badala ya kueleweka hakika zinaongeza maswali mengi mno kwa wenzetu wenye mashaka na mradi wetu pendwa tarajiwa.

Nakemea kwa nguvu zote, njia za aina yeyote zifananazo na hiyo ya ushawishi kwa jamii yetu kuhusu hilo!

Vilevile, siamini hao wasanii na watu maarufu wanatumia pesa zao kutoka mfukoni kuhimili gharama za hoteli za aina hiyo ya hapo juu kwa zaidi ya siku nne!

JE, KAMA HAWA WASANII WANATUNZWA KIFALME HIVYO (kama ni kweli) ILIKUWAJE KWA WAWAKILISHI WETU WALE 30?!

NAANZA KUHOFIA PENGINE TUPO KWENYE HATARI TARAJIWA!

Chama changu CCM naomba kama kikombe hicho kinaweza kutuepuka kwa kuzingatia MASLAHI MAPANA kwa Taifa letu tulipendalo na tukiepuke!

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
View attachment 2666858
Tatizo kubwa sana ninalolishuhudia kwa Watanzania wengi ni ujinga mbaya, tuelewane kuwa ujinga siyo tusi, ujinga ni sifa ya kutokuelewa. Sifa inaweza kuwa nzuri au mbaya, sifa ya ujinga mbaya ni ile ya kutokuelewa kuwa huelewi, sifa nzuri ya ujinga ni ile ya kutokuelewa lakini unafahamu kuwa huelewi.

Ukishaelewa kuutofautisha ujinga katika sifa nzuri na mbaya basi itakuwa wepesi sana kutokana na ujinga mbaya mwingi na kubaki na ujinga mzuri mchache wa yale mapya usiyoelewa. Na namna ya kuufuta ujinga mbaya ni kujifunza kile usichokielewa, ukishakielewa ina maan hu mjinga tena kwenye hicho unabaki kuwa mjinga katika kile tu ambacho hujajifunza.

Mfano mzuri tena ni mfano hai, ni huu wa sakata la bandari. Wengi tunajifanya tunaelewa kumbe hatuelewi chochpote, tunakuwa washitaki sisi, watowa hukumu sisi, waadhibuji sisi, wachimba makaburi sisi ya tuliowahukumu sisi. Siyo vibaya yote hayo, si ndiyo tunafanya kazi zote hizo kwa bidii, hatungoji kufanyiwa, au sivyo? Ni sifa kubwa hiyo.

Lakini ni sifa ya ujinga mbaya, sana tena sana. Kwa sababu huyo tunaemhukumu hatumjuwi. Tunamhukumu bila hata ya kumuona. Ujinga mbaya unazidi pale aliyekwenda kumuona, akmjuwa huyu ni nani, anafanya nini, tunamuona yeye ni mjinga. Nadiriki kusema tulionao ni zaidi ya ujinga mbaya, ni uhayawani kabisa.

Anaebisha atwambie, yeye kishafanya biashara ipi inayohusu bandari? Na kishafanya na nani? na kaifanya wapi?

Kama hana qualification hata kidogo za kuyajuwa hayo, na haujafanya hata utafiti japo kidogo wa kupata uelewa wa hayo, basi huna haki ya kunyanyua mdomo. Mao Tse Tung alisema "haujanya tafiti hauna haki ya kuongea". Nyerere alisema mmoja katika maadui zetu ni ujinga. Na mimi nakubaliana nae kwenye hilo 100%, nisichokubaliana nae ni zile sifa nyingine za maadui zetu. Nna sababu yangu moja tu ya kuzikataa hizo. Nayo ni kuuta ujinga, naamini tukifuta ujinga zile sababu zake mbili zingine hazitakuwepo tena.

Ambae hajafanya biashara za kimataifa au hata za kitaifa zinazohusiana bandari na ambae hajafanya japo utafiti wa anachokipinga katika sakata la bandari, hana haki ya kupinga na hana haki hata ya kufunguwa mdomo wake, yeye akubali tu, awawachie waliokwishafanya biashara hizo na au waliokwishafanta tafiti kwenye hilo.

Mimi napinga wajinga wote wanaopinga kijinga kwenye sakata hili. Haya, leta ujinga wako tuupime hapa ni ujinga mzuri au ujinga mbaya.
 
Mkuu umejenga hoja yenye mantiki nzuri sana. Ila pia kuna kauwezekano wengine huwa wana mabasha zao kule, kwa hiyo wanaenda kwa ajili ya kutoa huduma ya upendo na kufanyiwa "shopping spree" kupitia ofa za ma "Mr" wao wa Kiarabu.
 
Mimi napinga wajinga wote wanaopinga kijinga kwenye sakata hili. Haya, leta ujinga wako tuupime hapa ni ujinga mzuri au ujinga mbaya.
Andiko refu likiwalaumu unaowafikiria ni wajinga uwasemao "kijinga" lenye vina vingi vya "kijinga" lisilo elezea utofauti wa wajinga na uwingi wa "ujinga" uliouandika kusifia "kijingia" pasi kuelewa ndaniye ya sifazo hami nyingi zimejaa kupumbazwa "kijinga" ili uuhami "ujinga!"

Ajabu ni hii, mhami ujinga anawachukulia wajinga wale wote wanao hoji ujinga wadhanio uliingizwa kwenye MKATABA wa kijinga na WAJINGA WALIOAMINIWA NA TAIFA LISILO LA WAJINGA kama udhanivyo ewe MJINGA!
 
Deal gani la kishamba hivyo? Yaani uuze urithi wako kwakwenda kulazwa hotel na kulishwa kama mwali huku wewe ni mwanaume rijali si aibu hii mchana kweupe?
Au kupangisha mpaka chumba cha wazazi wako baada ya wao kuaga dunia. Aisee!!
 
Shida yao ni kutoelewa mipaka ya propaganda, tukio lipi linahitaji mbinu zipi na what is proportionate.

Wao wanafanya mpaka inakuwa kero ili mradi kuna fungu la kupiga basi huo ni mwanya kwa majizi

Unaanza kuona labda kuna maslahi ya mtu binafsi badala ya nchi.
 
Tatizo kubwa sana ninalolishuhudia kwa Watanzania wengi ni ujinga mbaya, tuelewane kuwa ujinga siyo tusi, ujinga ni sifa ya kutokuelewa. Sifa inaweza kuwa nzuri au mbaya, sifa ya ujinga mbaya ni ile ya kutokuelewa kuwa huelewi, sifa nzuri ya ujinga ni ile ya kutokuelewa lakini unafahamu kuwa huelewi.

Ukishaelewa kuutofautisha ujinga katika sifa nzuri na mbaya basi itakuwa wepesi sana kutokana na ujinga mbaya mwingi na kubaki na ujinga mzuri mchache wa yale mapya usiyoelewa. Na namna ya kuufuta ujinga mbaya ni kujifunza kile usichokielewa, ukishakielewa ina maan hu mjinga tena kwenye hicho unabaki kuwa mjinga katika kile tu ambacho hujajifunza.

Mfano mzuri tena ni mfano hai, ni huu wa sakata la bandari. Wengi tunajifanya tunaelewa kumbe hatuelewi chochpote, tunakuwa washitaki sisi, watowa hukumu sisi, waadhibuji sisi, wachimba makaburi sisi ya tuliowahukumu sisi. Siyo vibaya yote hayo, si ndiyo tunafanya kazi zote hizo kwa bidii, hatungoji kufanyiwa, au sivyo? Ni sifa kubwa hiyo.

Lakini ni sifa ya ujinga mbaya, sana tena sana. Kwa sababu huyo tunaemhukumu hatumjuwi. Tunamhukumu bila hata ya kumuona. Ujinga mbaya unazidi pale aliyekwenda kumuona, akmjuwa huyu ni nani, anafanya nini, tunamuona yeye ni mjinga. Nadiriki kusema tulionao ni zaidi ya ujinga mbaya, ni uhayawani kabisa.

Anaebisha atwambie, yeye kishafanya biashara ipi inayohusu bandari? Na kishafanya na nani? na kaifanya wapi?

Kama hana qualification hata kidogo za kuyajuwa hayo, na haujafanya hata utafiti japo kidogo wa kupata uelewa wa hayo, basi huna haki ya kunyanyua mdomo. Mao Tse Tung alisema "haujanya tafiti hauna haki ya kuongea". Nyerere alisema mmoja katika maadui zetu ni ujinga. Na mimi nakubaliana nae kwenye hilo 100%, nisichokubaliana nae ni zile sifa nyingine za maadui zetu. Nna sababu yangu moja tu ya kuzikataa hizo. Nayo ni kuuta ujinga, naamini tukifuta ujinga zile sababu zake mbili zingine hazitakuwepo tena.

Ambae hajafanya biashara za kimataifa au hata za kitaifa zinazohusiana bandari na ambae hajafanya japo utafiti wa anachokipinga katika sakata la bandari, hana haki ya kupinga na hana haki hata ya kufunguwa mdomo wake, yeye akubali tu, awawachie waliokwishafanya biashara hizo na au waliokwishafanta tafiti kwenye hilo.

Mimi napinga wajinga wote wanaopinga kijinga kwenye sakata hili. Haya, leta ujinga wako tuupime hapa ni ujinga mzuri au ujinga mbaya.
Nonsense.

Muambiwe mara ngapi ili muelewe? mmeshaambiwa tatizo letu na mwarabu sio uwekezaji, tatizo lililopo ni muda wa mkataba, kwanini mwarabu amepewa mkataba usio na ukomo?

Ina maana kama kizazi chetu kimeshindwa kuiendesha bandari( akili mbovu ya mtawala), ndio aamue kuitoa bandari moja kwa moja mpaka kizazi kijacho nacho kisiiendeshe?

Kwanini mwarabu amepewa Exclusive Rights kwenye ule mkataba? kwanini amefanywa kuwa kama "republic" inayojitegemea ndani ya ardhi ya Tanganyika?

Kwanini amepewa anga, ardhi, na maji afanye atakavyo kulingana na ule mkataba? na bado tunajibana kwake kumjulisha yeye kwanza, juu ya fursa nyingine zozote zitakazojitokeza kiuchumi? huu utumwa tumeutoa wapi? kwanini kama taifa Tanganyika tumejivua nguo kiasi hiki?

Iko wapi thamani ya Tanganyika kwenye ule mkataba mliosaini na mwarabu?

Hebu kakae na shangazi yako wa Makunduchi mje na majibu ya hayo maswali, msijitoe akili kutudanganya na uwekezaji kama vile hatujui maana yake, muwe na adabu.
 
Watanzania wenzangu hatima ya ustawi wa Taifa letu upo mikononi mwetu. Ni wajibu wetu kama Watanzania tujizuie kwa namna yeyote ima kununuliwa ama kushawishiwa kwa namna yeyote ile ilmradi tuligawe Taifa na rasilimali zetu.

Safari za namna hiyo za watu maarufu na wasanii wetu kwenda huko Dubai kwa nyakati za SINTOFAHAMU kubwa ihusuyo bandari yetu na wao badala ya kueleweka hakika zinaongeza maswali mengi mno kwa wenzetu wenye mashaka na mradi wetu pendwa tarajiwa.

Nakemea kwa nguvu zote, njia za aina yeyote zifananazo na hiyo ya ushawishi kwa jamii yetu kuhusu hilo!

Vilevile, siamini hao wasanii na watu maarufu wanatumia pesa zao kutoka mfukoni kuhimili gharama za hoteli za aina hiyo ya hapo juu kwa zaidi ya siku nne!

JE, KAMA HAWA WASANII WANATUNZWA KIFALME HIVYO (kama ni kweli) ILIKUWAJE KWA WAWAKILISHI WETU WALE 30?!

NAANZA KUHOFIA PENGINE TUPO KWENYE HATARI TARAJIWA!

Chama changu CCM naomba kama kikombe hicho kinaweza kutuepuka kwa kuzingatia MASLAHI MAPANA kwa Taifa letu tulipendalo na tukiepuke!

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
View attachment 2666858
Vijitu vya hovyo
 
Mbona kambeba halafu kamziba nyuma. Samia kakosa pa kutokea analeta maigizo sasa huyu Stev nani sijui ndio atakuja kuongea nini juu ya huu utumwa. Samia why asiwape hao DP WORLD bandari ya Pemba ambako kuna hali mbaya?
 
Hao hawapo kwenye kusaini madokoment ,hao wapo kikazi zaidi wanaambiwa kuna mchongo huo kazi ya yako ni kupiga ngenga tu tunakupa usd 10,000 na safari yote gharama juu yetu utakataa? wakuwamaindi ni wale wabunge 30 Aunt na mwenzake Dr M-Push wao ndiyo waliouza nchi ,hao wasanii tunawaonea bure ,wao kazi yao ni kupiga ngenga tu.,yeye anamezeshwa script tu.
Ni kweli wasanii tunawaonea, wakulaumiwa hao wasomi wetu
 
Sasa hekaheka zote hizi ni za nini kama mkataba ni mzuri? Nguvu kubwa inatumika kuwakamata hawa ili waanze porojo za kuwaaminisha Watanzania kuwa hawa jamaa hawana tatizo lolote. Kinachouma ni kuwa Rais wetu anayajua haya vizuri tu.
 
Kwenye hii ishu ya bandari kuna genge kubwa limeamua kuwanunua watu wengi ili kuwapigia debe, ukishamuona mahali Rostam yupo ogopa sana...ni mwanamikakati maslahi kwelikweli, yeye pesa kwanza uzalendo haumhusu...by the way yeye kwao ni Iran.
Hii cartel angeimudu JPM tu huyu mama hamna kitu, twafaaa!.
 
Watanzania wenzangu hatima ya ustawi wa Taifa letu upo mikononi mwetu. Ni wajibu wetu kama Watanzania tujizuie kwa namna yeyote ima kununuliwa ama kushawishiwa kwa namna yeyote ile ilmradi tuligawe Taifa na rasilimali zetu.

Safari za namna hiyo za watu maarufu na wasanii wetu kwenda huko Dubai kwa nyakati za SINTOFAHAMU kubwa ihusuyo bandari yetu na wao badala ya kueleweka hakika zinaongeza maswali mengi mno kwa wenzetu wenye mashaka na mradi wetu pendwa tarajiwa.

Nakemea kwa nguvu zote, njia za aina yeyote zifananazo na hiyo ya ushawishi kwa jamii yetu kuhusu hilo!

Vilevile, siamini hao wasanii na watu maarufu wanatumia pesa zao kutoka mfukoni kuhimili gharama za hoteli za aina hiyo ya hapo juu kwa zaidi ya siku nne!

JE, KAMA HAWA WASANII WANATUNZWA KIFALME HIVYO (kama ni kweli) ILIKUWAJE KWA WAWAKILISHI WETU WALE 30?!

NAANZA KUHOFIA PENGINE TUPO KWENYE HATARI TARAJIWA!

Chama changu CCM naomba kama kikombe hicho kinaweza kutuepuka kwa kuzingatia MASLAHI MAPANA kwa Taifa letu tulipendalo na tukiepuke!

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
View attachment 2666858
Umeanza vizuri sana ila hapo kwenye "kidumu chama cha mapinduzi" daah bora ungekaa kimya tu. Watawala wa chama chako niwabinafsi, wanafiki, na ndio wanaoliangamiza Taifa, maana wamekosa utashi na maarifa ya kuweza kusonga mbele kwa manufaa ya Taifa.
 
Ukicheka na nyani (CCM), utavuna mabua...

Watanzania mmekuwa mkicheka na nyani kila uchaguzi, na mmekuwa mkivuna mabua kila baada ya uchaguzi...

Na chaguzi zijazo bado mtaendelea kucheka na nyani...
 
Back
Top Bottom