Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,940
20,400
loan-image.jpg

Jana, raisi wa Jamhuri ya Muungano na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania kaeleza kwamba kuna mtu amekopa benki 5 au 6 tofauti za Tanzania na hajulikani alipo, yaani amekimbia na kutoka nchini.

Sasa huu ni mtihani kwa TISS, vyombo vya fedha, uhamiaji na wizara ya mambo ya ndani kwa ujumla.

Haiwezekani mtu mmoja akafanya jambo hilo zito na asepe kilaini hivyo hiyo ni ishara tosha kwamba idara yetu ya usalama na vyombo vingine vimelala au vimejiruhusu kupwaya kupita kiasi.

Lakini mimi ntaikosoa zaidi idara ya usalama kwani yenyewe ndio yaweza kuchagiza shughuli zote za ulinzi na usalama wa nchi.

Natambua idara hii ina uwezo mkubwa tu ina maofisa mahiri tu ambao wamepata mafunzo ndani na nje ya nchi hivyo wana ueledi, umahiri, uerevu na kila aina ya mbinu za kimkakati na kimedani kuhakikisha nchi yetu ipo salama.

Leo hii shirika la ujasusi wa ndani la Russia la FSB limetangaza kumshikilia mwandishi wa jarida la Wall Street Journal kwa madai ya kujihusisha na ujasusi wa ndani yaani kwa kiingereza twasema "Espionage".

Hiyo ni kazi ya majasusi wa ndani ya Russia yaani "Counter Espionage Agents" ambao wapo macho masaa 24 kulinda nchi, mali zake au "Assets" na miundombinu yake na wananchi kwa ujumla.

Sasa ni wakati wa idara yetu ya usalama wa Taifa kujipambanua kumtafuta huyu mwizi wa fedha zetu ambazo zimehifadhiwa kwenye mabenki zikiwa ni akaunti za watu na mitaji pia. Ni wakati wa kushirikiana na vyombo ya ulinzi na usalama vya nchi jirani na pia ni wakati wa kumtambua mtu huyo ambae ni wazi atakuwa alikuwa na pasi ya kusafiria, makabrasha mbalimbali yanoonyesha anuani zake na kadhalika hata kama ni "fake documents".

Kuhusu mabenki yetu nina imani kwa wana taratibu zote kali ambazo ni lazima mkopaji azifuate na kwenye hili ni lazima iwe ni "inside job" wafanyakazi walohusika ni lazima wapatikane kabla ya Jumaa.

Niliwahi kutoa mapendekezo huko nyuma kuhusu kuifanyia mabadiliko idara ya usalama wa taifa Mapendekezo: Serikali ipitie upya Sheria ya Usalama wa Taifa na TISS iundwe upya kwa maslahi ya taifa na nikzaeleza kwa upana wake.

Pia niliwahi kueleza kwamba wapo watu watembea na wallet tu Mtu anaesafiri kwenda nje kila siku lakini anabeba wallet na passport tu, utamfikiriaje? na hawa huenda ni wale ambao huenda sehemu kufanya machafuko kama uporaji fedha katika taasisi za fedha bila kugundulika na hii ni hatari kwa taifa.

Na pia nikawahi kutoa wazo kama nchi yetu ipo tayari kwa vita vya kijasusi wa uchumi katika mada hii Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari ambapo yawezekana kabisa huyu mtu aliefanya wizi huu wa kughushi ni wale akina Carlos Jackal ambae alikuwa na uwezo wa kuingia katika nchi yoyote na kumaliza kazi kisha kujiondokea asijulikane.

Carlos alikuwa ni jasusi ambae alifunzwa kulelewa na kuwa alipwa ujira na idara ya kijasusi ya Russia ya wakati huo KGB na kazi zake hazikuwa na mfano.

Lakini mtu huyu ambae amehusika na wizi wa mabilioni ya shilingi si wa aina ya Carlos Jackal lakini aweza kuwa ni mhalifu wa kimataifa na huenda akarudi tena.

Hivyo Idara yetu ya TISS iamke isijisahau kwani majukumu yake si ya kisiasa bali ni ulinzi madhubuti wa nchi yetu vikiwemo vyombo vyetu vya fedha ambavyo kwa kushirikiana na vyombo vingine kama Uhamaji na hata huko nje Interpol tayari mtu huyu angekuwa yupo kwenye "Wanted List".
 
Jamari Watanzania tusiwe mazuzu hivyo kila kinachosemwa tunameza bila tafakari. Interpol ambayo mwalifu atarudishwa kujibu mashtaka popote alipo!!
Kwani hapa twameza au twajadili?

Kumeza ni kukubali kuwa ndiyo hali halisi kama jamaa hapo juu asema kama kukopa ni kugumu watuwanyaje?
 
Hiyo ni syndicate ya hali ya juu inajulikana vizuri na ma boss wa Bot......ila sisi raia wa kawaida tunaanza kujadili masuala tusio ya jua, kufanya justification ya wizi tu.
Kama ni hivyo kwanini mkuu wa nchi aliongelee ikiwa kila kitu chajulikana?

Atupa faida gani?
 
Back
Top Bottom