Kama mpaka leo hujui shida za wananchi, wewe hufai kuongoza!

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,252
113,645
Tumeshatoka huko. Huko ambako Rais anatenga muda wa kukutana na wananchi wachache na kuzungumza nao juu ya shida zao.

Kwa wakati huo, hizo shida za wananchi zilipata afueni? Jibu ni hapana.

Jana imetangazwa kwamba Bi. Kiguu na Njia [nasikia jana katua Nigeria huko]naye ataanza tena huo utaratibu.

Ukisikia kufilisika kifikra ndo huko sasa!

Wamekaa madarakani zaidi ya miaka 60 na bado tu hawazijui shida za wananchi.

Sasa kama hawazijui shida za wananchi, watawezaje kuleta maendeleo?

Halafu tunashangaa na kulalamika eti umeme shida, maji shida, n.k.

Majibu ya kwa nini tupo kwenye hali tuliyonayo, yapo wazi kabisa.

Jingine, iweje huyu Rais wetu asizijue shida za Watanzania?

Kwani yeye anaishi wapi? Kaishi wapi? Katokea wapi mpaka asizijue shida za watu?

Nchi ina maajabu hii!!!
 
1.) Aibu sana Rais anashindwa kuwa na team ya kumueleza matatizo ya wananchi.

2.) Ni aibu mmno rais kutafuta umaarufu Kwa kujidai anasikiliza shida zamtu mmoja mmoja.

3.) Ni matumizi mabaya ya kodi na muda rais kufatilia tatizo la mmoja-mmoja nakusahau yakitaifa.

4.) Rais kufundishwa/kumuiga makonda katika utendaji nifedheha mbaya sana.

Tutachelewa saaana kufika hii nchi imejaa ujinga na kiki zakilofa
 
Laba pengine hatumfahamu vizuri Raisi wetu,, labda niulize,, mama ni raia wa nchi gani???
 
1.) Aibu sana Rais anashindwa kuwa na team ya kumueleza matatizo ya wananchi.
2.) Ni aibu mmno rais kutafuta umaarufu Kwa kujidai anasikiliza shida zamtu mmoja mmoja.
3.) Ni matumizi mabaya ya kodi na muda rais kufatilia tatizo la mmoja-mmoja nakusahau yakitaifa.
4.) Rais kufundishwa/kumuiga makonda katika utendaji nifedheha mbaya sana.
Tutachelewa saaana kufika hii nchi imejaa ujinga na kiki zakilofa
Hili linaiumiza sana chadema, watakosa la kuwaambia watanzania, ccm inakaba kila angle, salaaaleh!
 
Kwa maana hiyo ni kwamba viongozi wote nchi hii wameshindwa kutatua shida za wananchi, mpaka inabidi RAIS WA NCHI NA AMIRI JESHI MKUU aingilie kati kuja kusikiliza shida za watu kudhulumiana
Kwani Rais hazijui shida za watu? Hajaishi nchi hii kabla hajawa Rais? Sasa hivi haishi nchi hii?
 
Mie nadhani atadeal na watu Wenye ishu kubwa kubwa waloshindwa kupata utatuzi toka kwa wasaidizi wake
Tumpe nafasi ,tuone atakavyofanya na output itakayopatikana
huenda hata kina sie pangu pakavu tukapata nafasi ya kufika ikulu kuongea naye na tukaneemeka🤣🤣
 
Hakuna sababu ingine yoyote ya kimkakati.

Na ni ndiyo, tuna serikali ya watu wapumbavu na wajinga.
Wale wasiofikiwa, wanaodharauliwa, wanaoonewa, sasa wanakwenda kupata suluhisho that means, Nyumbu zinakwenda kupungua, chadema wakitwangwa huruma huipeleka kwa wananchi wajinga, ili wahurumiwe.
 
Tumeshatoka huko. Ambako Rais anatenga muda wa kukutana na wananchi wachache na kuzungumza nao juu ya shida zao.

Kwa wakati huo, hizo shida za wananchi zilipata afueni? Jibu ni hapana.

Jana imetangazwa kwamba Bi. Kiguu na Njia [nasikia jana katua Nigeria huko]naye ataanza tena huo utaratibu.

Ukisikia kufilisika kifikra ndo huko sasa!

Wamekaa madarakani zaidi ya miaka 60 na bado tu hawazijui shida za wananchi.

Sasa kama hawazijui shida za wananchi, watawezaje kuleta maendeleo?

Halafu tunashangaa na kulalamika eti umeme shida, maji shida, n.k.

Majibu ya kwa nini tupo kwenye hali tuliyonayo, yapo wazi kabisa.

Jingine, iweje huyu Rais wetu asizijue shida za Watanzania?

Kwani yeye anaishi wapi? Kaishi wapi? Katokea wapi mpaka asizijue shida za watu?

Nchi ina maajabu hii!!!
Yaani CCM wamekaa "think tank" na kuja na utopolo kama huu!!
Hakika upinzani wamepewa sehemu nzuri sana ya kuanzia kwa wananchi.

Ni kichaa pekee ambaye hajui tatizo lake kuwa ni ukichaa.
 
Mie nadhani atadeal na watu Wenye ishu kubwa kubwa waloshindwa kupata utatuzi toka kwa wasaidizi wake
Tumpe nafasi ,tuone atakavyofanya na output itakayopatikana
huenda hata kina sie pangu pakavu tukapata nafasi ya kufika ikulu kuongea naye na tukaneemeka🤣🤣
Hakuna cha kumpa nafasi wala nini!

CCM wamekuwa na hiyo nafasi kwa zaidi ya miaka 60.

Wapewe nafasi gani tena?
 
Back
Top Bottom