Kama inasomwa rasilimali usithubutu kuhoji; rasilimali zetu ni mali ya waliozisomea tu

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Sakata la bandari limevuruga chama cha mapinduzi katika maeneo mengi; limevuruga baraza la mawaziri na kulivuruga Bunge.

Mfumo wa bunge umeparaganyika; spika wa Bunge amehamia jukwaani na kuachia majukumu ya uspika kwa katibu wa Bunge. Kwake yeye kurejea bungeni kwa sanduku la kura aoni mwanga; amekataliwa jambo linalomlazimu kutumia propaganda nyingi kuwaandaa wapiga kura. Hakuna mbunge anayetumia nguvu nyingi kama spika katika siasa za majimbo. Hizi ni hasara za kukosa sifa za kisiasa kwenye ulingo wa kisiasa.

Matokeo ya wakataliwa kuongezeka ndani ya chama cha mapinduzi yamechangia baadhi ya wabunge wanaodhani awatapitishwa 2025 kuanza rasmi kujitenga na majimbo na hivyo viongozi wa juu wa chama kuwa na kazi kubwa kushawishi wananchi kuliko wabunge.

Siasa za maendeleo zimeondoka ndani ya chama na badala yake zimebakia siasa za uchawa ambazo hazina tija kwenye mfumo wa maendeleo.

Hali hii imepelekea wazee kushindwa kushawishi na baadhi ya wazee adharani kujitokeza kupinga kinachoitwa uwekezaji. Si mara nyingi sana unaweza kuwasikia wazee kama Warioba, Butibu na wengine wakisema nchi imeuzwa....means wao wenyewe awaelewi. Kama hawa wazee wana wasiwasi ikiwa wana taarifa zote za ndani ya serikali ni nani mwingine atajenga imani kwamba ipo dhamira dhati mbele?

Sikio la kufa halisikii dawa; mwezi septemba tunabadili sheria za rasilimali ili tupate mwanya wakuuza rasilimali za bandari kwa kuzingatia sheria mpya. Haya ni maono ya bunge na maono ya spika ila si maono ya wananchi

Mwisho; kwa wanaouza rasilimali zetu changamoto ya kudai rasilimali zetu kwao wanaita umbumbumbu wa watanzania na kwamba kama inajasomea rasilimali usithubutu kukosoa. Najiuliza wakati mwalimu anaamua kuzilinda hizi rasilimali watanzania aliokuwa anawaongoza walikuwa wamesomea rasilimali?
 
Mtu anaondoka kimya kimya bila tender yoyote wala uwazi anaenda anakabidhi Bandari kwa Waarabu kisa eti ni Rais!
Bunge na Mahakama vyote vimeufyata hawataki ukweli kwamba kuna tatizo!
Mtu mweusi ni mjinga hata angesoma hata akawa Profesa!
Rejea yule Kijana Wakili wa kizungu alivyokuwa akimkebehi Profesa Mruma kwenye ile tribunal.
Anamuuliza, hayo ndo unawafundisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam?! Anamuona zezeta tu!
Viongozi wetu nao ni hivyo hivyo!

Bandari zetu ameshakuwa Mwaraba , Mafuta yao yakikosa soko huko mbeleni kutokana na Matumizi ya magari ya Umeme basi wana Bandari zao walizookota kutoka kwa Viongozi mazuzu wa Tanzania ya leo.
Kifo cha Hayati Magufuli hakikuwa natural death! Kuna kitu na wahusika tumeanza kuwastukia!
 
Tatizo wa tz mengi hatuyajui.
Tz rasilimali nyingi sio za muungano bali ni Tanganyika, Tanganyika naye amekufa, mali zimekuwa wakfu, wabTanzania tunamlaumu m/kiti ambaye ni wa Tz, sio mliliki halali wa rasilimali zisizo za muungano. Amkeni ninyi watu.
 
Back
Top Bottom