Kama wananchi na viongozi walifundishwa binadamu alikuwa SOKWE na hawajawahi kulaani huu ushetani wataweza kulinda rasilimali zetu Afrika?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Kama viongozi wameshindwa kuondoa somo la Historia linalopotosha ukweli wa asili ya binadamu wanaweza kutetea rasilimali zetu?

Kama viongozi wetu wanaamini Afrika haiwezi kuendelea bila wazungu na kwao mzungu yoyote ni tajiri na mtu mwema; wataweza kulinda rasilimali zetu mbele ya wazungu?

Hadi pale tutakapokuwa na viongozi wanaomini kwamba wao ni binadamu kamili ndipo tutapiga hatua kwenda mbele.

Makanisa mengi yameweza kupiga hatua baada ya kuachana kabisa na misaada....leo makanisa makubwa yanajengwa na waumini wenyewe kwa rasilimali za ndani. Misikiti mingi nchini imeanza kujengwa na waumini wenyewe kwa kuchangishana mabadiliko yanaonekana....

Shule na vyuo vikuu vingi nchini vinajengwa kwa waumini na watu mmoja mmoja kufanya maamuzi. Hali hiyo ipo pia kwenye hospitali na sekta nyingine.

Serikali kwanini isiige mikakati ya waumini? Kwanini tuweze kujenga miundombinu na nyumba za ibada tushindwe kijenga nchi?

Maendeleo yoyote ni imani; tukiamua kuwaaminisha wananchi kwamba
1. Hakuna wizi wa mali zao
2. Kuna uwajibikaji
3. Tuna uongozi safi
Wananchi wataitetea nchi yao iwe njaa au shibe.
 
Back
Top Bottom