Kama huna mchango wowote kwenye jamii inayokuzunguka, unakosa maana ya kuishi

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,595
15,389
Kila mtu ndani yake ameumbwa na kitu ambacho mwenzake hana. Hii ndio sababu pekee kwa nini tumeumbwa tofauti na sio watu wenye ufahamu na akili za kufanana kama bata.

Lazima uwe na kitu cha kuchangia katika jamii. Ukiachia wengine hilo jukumu na ukabaki kuwa mnufaika wa michango ya wengine utakoswa maana na sababu ya kuwa hai.

Kaa kikao na maisha yako. Anza kuona ni nini kinaweza kuwa mchango wako kwa jamii inayokuzunguka au dunia kwa ujumla.

Wazo
Ushauri
Ubunifu
Kipaji

Chochote kile. Hata kuandika uzi wenye kuleta mabadiliko kwa mtu mmoja humu jf ni mchango.

Ni hilo tu kwa leo.
 
Sahihi kabisa na hicho ndio kipimo cha akili,kusolve issue au matatizo yanayokuzunguka au yanayoizunguka jamii yako,yani uyatawale mazingira na sio mazingira ndio yakutawale,badala ya kucomplain kila kitu,weka solution ya jambo hilo,kama kuna tatizo unaweza kulitatua basi litatue kabla hujacomplain.
 
Asante sana.
 
Back
Top Bottom