Kama hujawahi tumia hii Kimbo, basi wewe ni kizazi cha akina Lulu

Aafu kuna yale mafuta ya
korie sijui bado yapo, dah. Ulikua ukienda skonga enzi hizo
primary unajipaka mafuta ya korie ugoko wa mguu una meremeta. Usoni ndo
usiseme unawaka kama kioo. Na madaftari yako umechomekea matakoni kama
msela nondo! Dah...

kaaazi kweli kweli.
Tripo9 umenikumbusha mbali!
 
Last edited by a moderator:
bila shaka ww ni mchaga manake mlikuwa mnayapata ya magendo kupitia taveta. ila cowboy umeyasahau pamoja na super ghee. enzi hizo tulivaa na ndala za sonex, na chachacha.wengi tuliviita mwisho saa sita. shule tulikwenda na kidumu na ufagio na begi lilikuwa spoti spoti. vitabu hasa vya kiswahili vilikuwa na hadithi kama "brown ashika tama",na somo la uraia liliitwa siasa, na alikuwa siku nyerere anakuja lazima tujipange barabarani kumpokea huku nyimbo kama "tunaimani na nyerere", alama za chama ca mapinduzi jembe na nyundo" yapo mengi ya kukumbuka sana siku hizi watoto wa umri wa akina lulu hawana hizo.

zikaja kuingia na ndala za umoja kama big-g haikatiki aisee inavaliwa mpaka inatoboka..
 
Kumbe kuna makopo ya plastiki siku hizi! Mimi zamani nilikuwa nafikiri kuwa kopo lazima liwe na asili ya chuma.

labda tuseme wewe bado upo kule zamani haujaja huku siku hizi!sidhani kama kuna mafuta ya kupikia ya mgando kama ya enzi zile ya makopo ya chuma!
 
Aha! Kumbe hii me nilikuwa natumia ndogo yake iko kwenye kikopo kama cha mafuta ya Lay's,ila kalikuwa kanaitwa kibooo.

Mkuu Madame B umenikumbusha mafuta ya Rays ha ha haaa ukipaka shat la shule siku 1 tu limechafuka
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kama unaweza kukumbuka Supa Ghee, lazima ukumbuke, TanBond! Unakumbuka vitu kama Celerac, Millac Cowboy na Cawliflower, Beef nk? Hayo mavituz yametulea kwa afya njema!

Weweeeeeeeeeeeee beef ya Tanganyika parkers, jeshini mpaka tunahonga damnfool...
 
Hivi mafuta ya yolanda nitapata wapi bandugu?Pia natafuta kandambili za skyway.
 
dah nimekumbuka shanti na bodyline mafuta ya kujipaka mwilini baada ya kuoga kwa sabuni ya gardenia.mbeya tulikuwa na sabuni ya kufulia inayoitwa Hisoap bila kusahau matolori ya ZZK!!
 
dah nimekumbuka shanti na bodyline mafuta ya kujipaka mwilini baada ya kuoga kwa sabuni ya gardenia.mbeya tulikuwa na sabuni ya kufulia inayoitwa Hisoap bila kusahau matolori ya ZZK!!

hahahaaaaa Shanti ilikua babu kubwa....vipi chupi za VIP????
 
Back
Top Bottom