- Thread starter
- #21
Hili wazo hawakumshirikisha mtu mwanzoni maana huyu mwanamke aliekubali. Mkataba ilikuwa baada ya mwezi tangu kuzaliwa mtoto achukuliwe na hawa wanandoa. Walishaingia gharama zote kununua kila kitu cha mtoto nyumbani kwao kwa ajili ya kachanga huyo as if huyu mkewe kajifungua. Sasa huyu mama alipoambiwa asaini mkataba kuwa hana haki tena na mtoto huyo kisheria ila atabakia kama mama mzazi na ataruhusiwa kukatembelea hako katoto kwa ridhaa ya wanandoa hawa hapo ndio kasheshe ilipoanzia. Huu mwaka wa tatu anakataa katu katu. Ustawi wa jamii wamesema huyo mama mtoto ndo ana uamuzi wa mwisho. Kuzaa tena nje haitawezekana maana umri umeshawatupa mkono na hawataki kurudia hili kosa. Kuhusu kuchukua mtoto yatima huyu baba kakataa maana alitaka alee damu yake mwenyewe ndo maana akatafuta mwanamke wa kufanya nae hiyo dili. Kweli wabongo nuksi, huyu dada hajui ni matatizo gani anasababisha kwenye nyumba ya watu na hata siku moja hawezi kuwa mke wa huyu baba never. Mtu na mkewe wanapendana sana na kiuchumi wako vizuri. Huyu mtoto angekuwa mrithi hapo baadae na nageweza msaidia mama yake cku za usoni (she is 25 years) ambaye yupo kwenye hali ya umaskini.