Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Si tuliambiwa kuwa Kagoda ni ya Rostam mbona tena inakuwa ya Manji? Au lao moja? Basi sitashangaa tukiambiwa kuwa Kagoda ilikuwa ya Kikwete!

Nilivyosikia mimi Rostam hataki kabisa jina lake lihusishwe na Kagoda. Amefanya njama za makubaliano na Manji ionekane kuwa ni ya Manji lakini nijuavyo mimi Kagoda ni ya Rostam. Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini Rostam hataki ahusishwe na Kagoda? Ukishapata jibu la swali hilo umefumbua kitendawili kizima cha EPA
 
Mambo yazidi kufichuliwa

Wednesday, June 11, 2008
Mtandao wa Kikwete wakwapua BoT

Na Saed Kubenea

MSULULU wa makampuni yaliyokwapua mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu (BoT), unadaiwa kunufaisha kampeni za Rais Jakaya Kikwete, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam wiki hii zimeeleza kuwa makampuni hayo, yaliyoanzishwa kwa kasi, yalilenga kujinufaisha, lakini pia kubeba mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jukumu ambalo lilifanikiwa.

Mtoa habari wa ndani aliliambia mwanaHALISI kuwa mpango wa kuotesha makampuni kama uyoga, na kufanikiwa kuchota Sh. 133 bilioni, ulibuniwa na baadhi ya viongozi wa mtandao wa Kikwete baada ya kuona kwamba hawakuwa na fedha za kuendesha kampeni.

Imeelezwa kwamba mpango huo ulipata baraka za aliyekuwa rais, Benjamin Mkapa baada ya kukutana na wanamtandao na kujadiliana nao juu ya mapungufu yao na jinsi ya kupata fedha.

“Baada ya Mkapa kukataa mapendekezo ya baadhi ya viongozi wenzake ndani ya chama na kuamua kuwa Jakaya Kikwete ndiye alikuwa anahitajika kugombea, mzigo wa kupata fedha za kuendesha kampeni ulikuwa umemwangukia,” ameeleza mtoa habari.

Kuna madai kwamba Mkapa alikubaliana na wanamtandao juu ya kupata fedha na kuwaelekeza kwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali ambako uliandaliwa mpango mzima wa kupata fedha kwa njia ya kuuziana madeni katika akaunti ya EPA.

Mfumuko wa taarifa kuhusu jinsi fedha zilivyopatikana unatokana na baadhi ya wanamtandao kutoridhika kwa kuachwa nje ya duara la madaraka na bila kuona uwezekano wa mabadiliko katika miaka miwili na nusu ya utawala wa Kikwete.

Hii ni mara ya kwanza kwa tuhuma nzito namna hii kutolewa dhidi ya mtandao wa Kikwete ingawa baadhi ya wanamtandao mmojammoja wamekuwa wakitajwa kwenye orodha ya “mafisadi” iliyotangazwa na vyama vya upinzani tarehe 15 Septemba mwaka jana.

Kifo cha Ballali ambacho kilitanguliwa na usiri mkubwa wa serikali juu ya mahali alipo, afya yake na iwapo anahitajika kujibu hoja juu ya mabilioni ya shilingi yaliyokwapuliwa, kinachukuliwa kuwa msiba mkubwa kwa waliotaka kujua zaidi mtandao wa wizi ndani ya BoT.

Kwa mujibu wa kalenda ya matukio, uteuzi wa mgombea ndani ya CCM ulifanyika Mei 2005 na kampeni zilianza Agosti mwaka huo. Ingawa mtoa habari hakusema ni lini hasa wanamtandao walikutana na Mkapa, inasadikika kuwa ilikuwa siku chache kabla kampeni kuanza.

Kulingana na taarifa ya maodita wa Delloite & Touche wa Afrika Kusini, waliokagua hesabu za akaunti ya EPA kabla ya kunyang’anywa kazi hiyo, makampuni 12 yaliingia makubaliano kati ya tarehe 10 Oktoba na tarehe 3 Novemba 2005.

Makampuni mengine matano (5) yaliingia makubaliano siku moja, tarehe 19 Oktoba 2005 wakati mengine manne (4) yaliingia makubaliano tarehe 18 Oktoba mwaka huohuo. Mikataba yote ilisainiwa mbele ya kamishena wa kiapo B.M. Sanze.

Ni kasi hii iliyowastua maodita wa Delloite & Touche, kuwafanya watilie mashaka makubaliano hayo kufanyika haraka kiasi hicho; na katika ripoti yao kueleza waziwazi kuwa kulikuwa na chembechembe za udanganyifu.

Kilichowastua zaidi maodita ni kuona makubaliano yote yanasainiwa Dar es Salaam na hata marekebisho yaliyohusu kampuni iliyosemekana kuwa Ulaya, yalifanywa katika siku mbili tu.

Barua ya tarehe 4 Septemba 2006 kwenda kwa Ballali, ikiwa imesainiwa na Samuel Sithole aliyekuwa kiongozi wa maodita, inatilia mashaka kasi ya kutia saini mikataba na kusema ingekuwa vema kuchunguza katika Idara ya Uhamiaji kuona kama kweli wenye makampuni walisafiri kutoka Ulaya hadi Dar es Salaam katika muda mfupi namna hiyo.

Wasiwasi mkubwa ulionyeshwa kwa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo ilionyesha kuwa nchini Ujerumani wanalipa kwa kutumia fedha za Euro lakini BoT ikawasahihisha na kuwaambia waweke Deutshe Marks.

Mshangao wa maodita wa Delloite & Touche unatokana na kuona kuwa sahihisho hilo lililohusu Kagoda na ambalo lilihitaji watu kwenda Ujerumani au kutoka Ujerumani kuja nchini lilifanywa katika saa 48 tu.

Vyama vya upinzani na watu binafsi wamekuwa wakidai kuwa fedha zilizokwapuliwa BoT zilitumika katika uchaguzi mkuu wa 2005 na kwamba Timu ya Rais ya Kufuatilia makampuni yaliyohusika katika wizi huo ni “kiini macho.”

Katika hatua nyingine, taarifa zimemnukuu kiongozi wa juu katika CCM akisema, “Hatuwezi kuendelea kuchota BoT.” Alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na mmoja wa viongozi wa Kamati Kuu (CC) kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) itafute fedha, hata kuomba BoT ili kuendesha kikao cha NEC kilichokuwa kifanyike Dodoma mwezi uliopita.

Kikao cha NEC kinatafuta kujadili hoja zilizowasilishwa na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu kwenye kikao kilichopita ambacho kilifanyika Butiama, mkoani Mara, mwishoni mwa Machi.

CCM ilionyesha nguvu na ufahari wa aina yake wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005 ambapo nchi nzima ilifurika fulana, kapelo, khanga, mabango, vipeperushi, matangazo katika magazeti, redio na televisheni na magari ya chama na mengine binafsi ya kifahari yaliyokuwa yakipishana kama siafu.

“Nakwambia, hakuna awezaye kuthibitisha kuwa fedha hizi zilikuwa za chama. Kwanza hatukuwa na fedha za kufaya kufuru ya aina hii,” ameeleza mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM.

Kiongozi huyo alisema kulikuwa na vurugu ndani ya chama wakati wa uchaguzi. “Kulikuwa na makao makuu mawili – Ofisi ndogo ya Mtaa wa Lumumba na Upanga ambayo yalikuwa makao ya mtandao; kulikuwa na sekretariati mbili na maelekezo kutoka kambi mbili, kabla na baada ya Kikwete kupitishwa kuwa mgombea,” ameeleza mtoa habari.

Hata hivyo MwanaHALISI limeelezwa kuwa siyo viongozi wote ndani ya CCM wanajua mpango wa kukwapua fedha kutoka BoT.

Kiongozi mmoja ameliambia gazeti hili, kwa kutaka ajina lake lisitajwe, kuwa kuna wakati kiasi kilichochukuliwa benki kilimstua hata Mkapa.

“Walipomwambia kuwa Sh. 133 bilioni ndizo zimechukuliwa kutoka BoT, Mkapa alistuka, akashika kichwa kwa mikono miwili na kuuliza, ‘Fedha zote hizo za nini?” ameeleza mtoa habari.
Source: http://saedkubenea.blogspot.com/
Mwisho
 
Inakuwaje kuwaje kila kunapokuwa na Kikao cha Bunge wakati huo huo kuna kuwa na vikao vya CCM,Neki shingo na kadhalika ,hapa si wanapigwa chenga ya mwili wa Tananzia kwa nini jambo hili lisipigwe stop ,kwamba wakati Kikao cha Bunge kikianza ni marufuku kwa kikao chengine chochote cha Chama maana vikao hivi vya kina Chama vinapoteza ushahidi.
Bunge kama mahakama ya Nchi kwa upande wa sera za serikali hivyo kufanya vikao vya chama vinavyowahusisha wabunge wakati wa kikao cha Bunge ni kujikusanya kwa chama husika ili kupoteza malengo na ushahidi Bungeni.
Kikao cha Bunge si kwa ajili ya maslahi ya Chama bali kwa ajili ya maslahi ya Taifa hivyo Chama chochote kinachoitisha kikao katikati ya kika cha Bunge ni udikteta.
 
Haya mambo ya kuuziana kesi inatakiwa waangalie kifungu cha sheria, hili Manji alipe pesa na kifungo jela miaka 20, ili akome kununua kesi za watu.
 
Hakika mimi nafahamu asili ya fedha za Bakhera, Mohamed Enterprise... lakini sijui asili ya fedha za Manji...

Kwa hiyo nikiunganishiwa na EPA.. kidogo kuna kitu kina-click somewhere... anyway tusubiri... Mimi sijui.

Na kama kweli ni Muhusika lakini hakujulikana hadi leo... basi jamaa ni mwanamume
 
Hakika mimi nafahamu asili ya fedha za Bakhera, Mohamed Enterprise... lakini sijui asili ya fedha za Manji...

Kwa hiyo nikiunganishiwa na EPA.. kidogo kuna kitu kina-click somewhere... anyway tusubiri... Mimi sijui.

Na kama kweli ni Muhusika lakini hakujulikana hadi leo... basi jamaa ni mwanamume


Hakujulikana kivipi au ni mambo ya kulindana bro??????
 
Hapa ni ngojera. Yusuph Manji ametwishwa msalaba tu

Kama ametwishwa naye akakubali kujitisha basi huyo huyo aende Segerea si kakubali kwamba yeye ndiyo mwizi? Kama hakubali afumbue mdomo na kusema sasa, sisi hatujui ni mfadhili ya Yanga yetu wala CCM suala ni jinai ya kuiba BOT
 
Awkward,
Mkuu labda humjui Manji vizuri na jinsi anavyofanya kazi zake...
Siku zote huyu jamaa amekuwa akitumiwa na viongozi wetu katika miradi kibao na hivi sasa yuko mbioni kuchukua Cocobeach na kipande kikubwa cha majumba ya msajili yaliyopo Samora..
Vyote hivi ni kitu kama vile Frachise yaani owner wa mali hizi ni kiongozi lakini jina linalokuwa mbele yetu ni Manji..Ndio maana mengi alishindwa kuelewa kiburi cha huyu Manji..
Dotori kasema kweli kabisa kuwa mzigo huu umebebeshwa kwa sababu swala hili lipo Dodoma ktk kikao cha chama yaani siasa ambayo Manji sii mhusika.. Hivyo wajumbe kwa kuona jina la Manji na sio kiongozi watashindwa kuendelea kuhoji Kagoda kwa sababu ipo nje ya maswala yaliyowakutanisha..
Na wakisha toka hapo hata mkianzisha kesi kuhusiana na Manji na hiyo Kigoda sana sana kitaklachotokea ni yeye kurudisha fedha za EPA jambo ambalo linaweza funikwa na kawa kirahisi na wananchi msifahamu kilichoendelea.
Muhimu ktk mkutanbo huuu ni kuwaondoa viongozi wote wa CCM ktk kuhusika na scandal zote waonekane wao ni wasafi.. makosa yalifanyika ama ni lawama za watu wenye wivu...sahau kabisa habari ya uchunguzi wa jambo lolote zaidi tumeshaliwa mkuu..Tumeliwa!
 
Unajua haya mimi niliyasema siku nyingi sana hapa JF, siku niliposema kuwa hata Ze-Comedy wameinunua Manji na Rostam, nilisema kuwa Kagoda na Dowans, Rostam ameamua kumpa Manji, ni dataz ambazo nilizitoa siku nyingi sana hapa, ukweli ni kwamba rostam ameamua "kumpa" Manji kampuni zote zinazomhusu lakini bado ni zake,

Mkuu wangu Bubu, kikako cha bunge hakijaisha hebu naom,ba usikilizie kivumbi betweeen the next few days kama sio kesho!
 
Haahahahaaa

Mwe na amani wakuu,wanakimbia mbio za sakafuni,siku yao yaja na nchi nzima itatiririka damu yao.
 
ipo siku ngumi zitapigwa waziwazi...hivi watu kama selukamba mbona hawana huruma na wanarudisha jitihada nyuma?? Kwa kweli inatia uchungu sana basi tu hakuna jinsi
 
FMES,
Mkuu nakukubali sana na wala sii huyo Rostam peke yake wamo wengi.... viongozi wanatumia sana watu siku hizi kwa janja kama uloisema, kisha huwapa kinga hao watu inapofikia mahakamani ama ktk media. Utaona watakavyo msafisha Manji magazatini hasa hayo anayomiliki mkulu.
Kwa mfano Mama Mkapa ndiye mmliki wa yale maghorofa ya NHC pale Ilala.. lakini ukienda kutaza nani mmliki wa hotel inayoendeshwa ktk moja ya majengo hayo Hotel Lamada utakuta jina la mtu mwingine kabisa hivyo utaondoa dhana ya kuwa mama Mkapa ndiye mwenye majengo na huyo jamaa kapanga tu akilipa kodi kubwa za miaka!...Kumbuka tu upangishaji Tanzania ni lazima utoe kodi ya mwaka mmoja ama miwili kwa mara moja... tayari kisha rudisha fedha alizonunulia majengo hayo toka serikalini.. Na ajabu ni kwamba ikiwa majengo haya ya NHC na Msajili yanalipa hivyo kwa nini serikali yenyewe isipangishe kwa market rate iliyopo badala ya ke yanauzwa wakisingizia serikali inashindwa kulipia gharama za kuyaendesha..
Ndio yale yale ya mashirika ya Umma kilichotembea hapo ni usanii mtupu...yaani maendeleo ya Mtanzania ni sawa na Pialau la Maulidi..
Mkuu hivi sasa naandika kitu safi sana nitakuja kiweka hapa sii muda - nakiita Pilau la Maulidi! lugha nzito na yenye mafumbo na ufunuo mzito mzito utafiki Biblia!...Kazi kwenu.
 
.............kikwete
............manji
.....karamagi
..............lowassa
..............d?..........
.........rostam
 
Watauza na kuyanunua hayo makampuni tena lakini ukweli utabaki palepale. Kikwete ni FISADI mtupu anajaribu kujikosha lakini ni fisadi #1. Huyo Mbunge na mfanyabiashara alipomsakafia Fisadi Mkapa, eti Kikwete anadai huyo jamaa ana busara sana. I don't care Mkapa kaondoka kaacha trilion, jilioni au vilioni Hazina, kama ameiba au kuvunja sheria lazima ashitakiwe kwa mujibu wa sheria. Na si kuanza kupakana mafuta mafisadi kwa mafisadi. Kama kafanya kazi nzuri mbona wananchi ambao ni wengi hawasemi, lakini nyie mafisadi wachache ndo mnaliona hilo.

Fungeni makopo yenu, rudisheni pesa zetu, mjiuzulu kisha mjisalimishe wenyewe tena sio polisi bali Segerea. Kila mtu achague sero gani anapenda apelekwe.
 
kikao cha nec cha sasa ni damage control tu. wanajua kuwa wananchi wamekosa imani na chama na ndo maana wanajaribu kusafishana. kuwa viongozi wa chama hawahusiki na ufisadi.
ukiangalia sequence utaona iko wazi kabisa.
kikwete kuwasafisha lowasa na wnziwe kuhusu richmond
rostam kusema kagoda si yake bali ni ya manji
........................

in conclusion utaweza kugundua kuwa waswahili hawakukosea waliposema simba mwenda kimya ndo mla nyama. muoneni kikwete!
 
Jamani lazima tujiulize hata hawa viongozi serikalini wanajivunia nn???
Kwa kufanya vitendo ndivyo sivyo nn wanajivunia??
Mbona wabunge wa CCM wanapelekeshwa pelekeshwa?Kwa nn wanakuwa waoga tena afadhali ya kunguru wao uwoga wao umepitiliza kabisa.
 
Back
Top Bottom