Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Kilitime,

Tatizo hapo sio wananchi, tatizo ni hao wanaotoa hizo data ambazo hata hawawezi kutuhakikishia wamezitoa wapi.

Kujua au kuelewa analysis za uchumi sio lazima usomee uchumi. Na kwa taarifa tu siku hizi kwenye nchi nyingi za West, wanaopewa kazi kwenye mashirika ya maana yanayoshughulikia na mambo ya investments sio wale waliosomea uchumi na badala yake ni wasomi wa hesabu. Ukisikia hao watu wa city wanaopata malaki, wengi wao ni universities wamesomea maths.

Kitendawili hapa ni hao wanaojaribu kutulisha data ambazo haziendani na realities huko wilayani.

Mzee ukishajua Hesabu ndio mwisho wa mambo yote!!! Usinikumbushe Analysis za Clansen pale UDSM,,,!!!

Prove that zero devide by any number [0/x; Where x is a real number) is equal to 0 [zero]!!! Ukikosea step moja... swali la marks 18 ndio limepotea hivyo!!! no longolongo...
 
Kwa maoni yangu sioni sababu zozote za kugombana kati ya hawa watu wawili hasa ukitilia maanani mafanikio makubwa katika miezi ya karibuni ya kuitetemsha CCM kuhusiana na mikataba ya madini na kashfa ya BOT.

CCM wameshagundua kwamba wanaweza kabisa kumtumia huyu Wangwe ili kukisambaratisha CHADEMA. Viongozi wa juu wa CHADEMA wanatakiwa walishughulikie sakata hili mapema kwa kumpa onyo kali Wangwe au hata kumsimamisha uanachama kwa miezi sita vinginevyo wanakichimbia kaburi chama chao.

Hapana kaka mtu moja hana uwezo wa kuisambaratisha CHADEMA, hii ni taasisi. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, haya ni malumbano ya kawaida na yatapita kama yalivyopita mengine. Mimi binafsi wasiwasi wangu sio kusambaratika CHADEMA maana najua hilo halipo, ila tu sitaki CCM watake a simple ride through our "backs". Kama akina Ngasongwa hawawezi kumwaga vitu kutokana na kuchoka kwao kiakili, hatutaki Zitto ajichoshe kwa kuwasaidia hasa pale ambapo watu kama Uhuru wanadandia. Tunataka hizo nondo nzito za uchumi alizo nazo Zitto azielekeze kwenye kuibuka na sera mbadala za uchumi through chadema.
 
Unapoona kuna mikwaruzo na personality conflicts ndiyo kwenye demokrasia.

Ukiona kila kitu "ndiyo mzee" basi ujue kuna mtu anapelekwa-pelekwa hapo.

Keep it going guys, tunamung'unya data tu.
 
Chama kinatakiwa kiwe na mshikamano. Katika chama chochote kile kuna kuwa na tofauti mbali mbali za viongozi wa juu wa chama ambazo ni vizuri kama zitamalizwa ndani ya chama badala ya kulumbana katika vyombo vya habari na kuwapa faida vyama vingine. Mafanikio mliyoyapata katika siku za karibuni yanatiwa dosari kubwa sana na malumbano haya ya kwenye vyombo vya habari na ndio sababu Mzee Ndesamburo anawatahadharisha kwamba yanaweza kabisa kusambaratisha chama.

Katika malumbano haya kuna baadhi ya viongozi na hata wanachama watakuwa upande wa Wangwe na wengine upande wa Zitto, hapo mgawanyiko huanza kujitokeza na kuharibu mshikamano uliokuwepo na badala ya kuelekeza nguvu zenu kupambana na ufisadi unaofanywa na CCM mtakuwa mnalumbana wenyewe kwa wenyewe na kuharibu credibility mliyojijengea kwa Watanzania mbali mbali hata wale wasio wanachama wa CHADEMA.
 
Kilitime,

Tatizo hapo sio wananchi, tatizo ni hao wanaotoa hizo data ambazo hata hawawezi kutuhakikishia wamezitoa wapi.

Kujua au kuelewa analysis za uchumi sio lazima usomee uchumi. Na kwa taarifa tu siku hizi kwenye nchi nyingi za West, wanaopewa kazi kwenye mashirika ya maana yanayoshughulikia na mambo ya investments sio wale waliosomea uchumi na badala yake ni wasomi wa hesabu. Ukisikia hao watu wa city wanaopata malaki, wengi wao ni universities wamesomea maths.

Kitendawili hapa ni hao wanaojaribu kutulisha data ambazo haziendani na realities huko wilayani.

Mchumi mzuri ni yule mwenye first degree ya Maths ama Engineering na anapokwenda kufanya MA/MSc anaingia kwenye fani ya uchumi na anaunga mpaka PhD. Wasomi wa zama za akina Ngasongwa (sijui kama ni mchumi) hawa-fit tena kwenye ulimwengu wa wachumi wa zama hizi. Ndiyo maana US wanataka mtu anaekwenda kufanya graduate program ya uchumi lazima awe na very strong background in maths!
 
Kuna tofauti kati ya chama kuwa na mshikamano na kuminya uhuru wa kujieleza.Hatutaki kuendeleza mambo ya CCM katika upinzani.
 
Chama kinatakiwa kiwe na mshikamano. Katika chama chochote kile kuna kuwa na tofauti mbali mbali za viongozi wa juu wa chama ambazo ni vizuri kama zitamalizwa ndani ya chama badala ya kulumbana katika vyombo vya habari na kuwapa faida vyama vingine. Mafanikio mliyoyapata katika siku za karibuni yanatiwa dosari kubwa sana na malumbano haya ya kwenye vyombo vya habari na ndio sababu Mzee Ndesamburo anawatahadharisha kwamba yanaweza kabisa kusambaratisha chama.

Katika malumbano haya kuna baadhi ya viongozi na hata wanachama watakuwa upande wa Wangwe na wengine upande wa Zitto, hapo mgawanyiko huanza kujitokeza na kuharibu mshikamano uliokuwepo na badala ya kuelekeza nguvu zenu kupambana na ufisadi unaofanywa na CCM mtakuwa mnalumbana wenyewe kwa wenyewe na kuharibu credibility mliyojijengea kwa Watanzania mbali mbali hata wale wasio wanachama wa CHADEMA.

Haya ni mazoea tu kaka yaliyojengeka katika mfumo wa CCM. Haiwezekani all the time mkubaliane mambo kwa sababu hata kama sisi sote ni wanachama wa chama kimoja hatufikiri sawa. Cha msingi hapa ni kwamba malumbano hayajengi chuki kiasi cha kushindwa kufanya kazi pamoja na ndivyo sisi chadema tulivyo. Tunalumbana ndani na nje lakini kazi tunaendelea kuchapa na tunaendelea ku-socialise vilevile katika nyama choma na kwingineko. Hatutaki utumwa wa kuvimbia ndani kwa ndani kama ilivyo kwa CCM, watu wanazeeka ovyo kwa sababu ya kumeza mawazo na mahasira badala ya kuyatoa. Ndio maana unaona hata hapa katika JF wanachama na viongozi wengi wa chadema wanaingia hata na majina yao halisi, yote hii ni kwa sababu hiki ni chama cha watu huru, wapende demokrasia na maendeleo. We always extensively brainstorm and debate an issue bofore pressenting it to formal party structures. That is us. Usiwe na wasiwasi, chama chenu kipo makini, hakitawaangusha-kiungeni mkono tujenge demokrasia na nchi.
 
Hilo la kuwaona viongozi wa juu wa CHADEMA wanakuja hapa JF na kujadiliana na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya dunia mimi linanigusa sana na nawapeni hongera za hali ya juu kwa hili. Sijawahi kumuona W. Slaa hapa ukumbini kama hajawahi kufika naomba mumhamasishe ili afanye hivyo, maana inatia moyo kuona viongozi ambao wako tayari kutumia muda wao kujadiliana na Watanzania wengine bila woga kuhusiana na mambo mmbali mbali ndani ya nchi yetu.

Kama unaamini hayo malumbano katika vyombo vya habari kati ya Zitto na Wangwe hayataleta mmomonyoko ndani ya CHADEMA basi na iwe hivyo, na mimi nawatakia kila la heri katika kupambana na mafisadi wanaotumia nyadhifa zao wanazopewa na Watanzania kujitajirisha, kusaini mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa Watanzania na kujinyakulia makampuni ya Tanzania katika mazingira ya kutatanisha.

Mungu ibariki Tanzania
 
Hilo la kuwaona viongozi wa juu wa CHADEMA wanakuja hapa JF na kujadiliana na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya dunia mimi linanigusa sana na nawapeni hongera za hali ya juu kwa hili. Sijawahi kumuona W. Slaa hapa ukumbini kama hajawahi kufika naomba mumhamasishe ili afanye hivyo, maana inatia moyo kuona viongozi ambao wako tayari kutumia muda wao kujadiliana na Watanzania wengine bila woga.

Huyo ni mwachama wa hapa wa siku nyingi, labda kama alijifuta usajiri wake. Niliwahi kumuona miaka ya 2005/6. No wonder huwa anapiga chabo kama guest na kuchukua notes kidogo kidogo na bahati njema alikuwa akitumia jina lake halisi na si hizi fake names za kwetu!
 
I second Bubu,

Inatia matumaini kuona viongozi angalau wanajua nini maana ya kutumia "new media" regardless ya input yao.Hao wengine (Read Kingunge and his tired posse) sina hata hakika kama wanaweza kuelewa what an online forum is, na hata wakielewa wanaweza kuwa na uvumilivu wa ku-weather persistence ya dada kama Asha Abdallah!

Alikuja Kikwete hapa kwenye mkutano wa UN ilikuwa aibu, maana jamaa ana ki-notebook kimechoka choka complete with dog ears.Yaani rais mzima alikosa hata ka PDA ka kiushkaji tu? Aibu.

Teknolojia muhimu.
 
Hilo la kuwaona viongozi wa juu wa CHADEMA wanakuja hapa JF na kujadiliana na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya dunia mimi linanigusa sana na nawapeni hongera za hali ya juu kwa hili. Sijawahi kumuona W. Slaa hapa ukumbini kama hajawahi kufika naomba mumhamasishe ili afanye hivyo, maana inatia moyo kuona viongozi ambao wako tayari kutumia muda wao kujadiliana na Watanzania wengine bila woga kuhusiana na mambo mmbali mbali ndani ya nchi yetu.

Kama unaamini hayo malumbano katika vyombo vya habari kati ya Zitto na Wangwe hayataleta mmomonyoko ndani ya CHADEMA basi na iwe hivyo, na mimi nawatakia kila la heri katika kupambana na mafisadi wanaotumia nyadhifa zao wanazopewa na Watanzania kujitajirisha, kusaini mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa Watanzania na kujinyakulia makampuni ya Tanzania katika mazingira ya kutatanisha.

Mungu ibariki Tanzania

Amina, na maneno yako na wana JF wengine ya kuitakia neema upinzani, demokrasia na Tanzania yetu yadumu!
 
Nakwambia tuna kazi. Sasa huyu kijana Killtime tunayemwania sana hii sijui katoa wapi tena, nimewauliza ni wapi mimi nimesema waseme uongo hawataki kwa sababu hakuna, ila wanapindisha mambo ili kupotosha hoja yangu. Ngoja tukubali kutokubaliana!

Shukrani Kaka,

Nathani Mh. Zitto amechukua muda wa kutosha kukuelewesha sina ya ziada,,, suala la kutaka Mh. Zitto asiseme uchumi unakua halikua jambo jema hata kidogo,,,naomba kwa imani yako,,, umwombe Mungu akusamehe kwa kuwa mbinafsi, hasa likitoka kwa kiongozi wa Chama Makini Mtarajiwa, Mtaaluma, Rais wa DARUSO mstaafu, kwangu mimi niliona kama aiba ya hali ya juu, namshukuru tena Mh.Zitto kuchambua vizuri, kwani ingekuwa ni mimi mwenyewe nimeliona tofauti then I could ask myself a lot of questions!!!

Kutotaka mtu aseme kweli maana yake ni kutaka aseme uongo,,, na ukweli ulichotaka alikisema Wangwe!!! au sio mkuu!!! na sina haja ya kukumbusha kwamba Wangwe amesema nini????

Sasa mbinu za siasa za namna hiyo hazina tofauti na pale Manzeshe University mwenzako akuombe Desa akasome,,, au umuonyeshe how to solve swali fulani wakati wa Prep... umkatalie ati kwa kuwa atakushinda au mko kwenye majadiliano mengine unaficha ili wasikupite wenzako!!! usijue kwamba wewe unamkatia shule mwenzako/wenzako ndiye unayefaidika zaidi...

Serikali ya CCM ikifikisha nchi pazuri, mkachukulia pazuri is far better kuliko kuiombea isifanye chochote alafu nanyi mchukulie uchumi ukikua au ukishuka kwa negative 6%! Kuwa na mtazamo wa mbali nakuhakikishia uta-review post yako...

Mashaka yangu ni kwamba kama taifa litajengwa kwa kutoweka mambo ya msingi wazi, kwa manufaa ya Taifa,,, then hatuhitaji hao wasomi basi!!!

Anyway nimeyakubali yote kwa sababu ya "Wengi Wape" nadhani twaweza funga Mjadala...
 
Mtanzania,

Bila kuchukua mamlaka ya Zitto,,, na kwa kuwa wewe umesoma Hisabati na Statistics,,, Nadhani utanielewa...

(A) Ukitaka kulinganisha kitu chochote kile unatakiwa uwe na reference point...

(B) Uchumi kukua kwa say 2%, 3%, 7% or x% maana yake ni ukilingalisha na mwaka uliopita,,, hii ina maada gani pato la mwaka jana kama ni 100 mwaka huu limekua kwa x% maana yake pato la mwaka huu ni [(100 + (100 *x%)]

(C)Catch 22; Do not compare the percentages!!! kwa sababu hizo percentage ni za pato/mapato tofauti, na hili ndilo linakukuta wewe na wengine... 10% ya 1996 inaweza kuwa ndogo sana kulinganisha 4% ya Mwaka 2008!

kama percentage ndiyo ingekuwa kigezo uchumi wa UK unakua kwa 2-3% kwa hiyo tungesema wao uchumi wao haukui... this is not the case.

(D)Ungeelewa zaidi kama ungekuwa unafuatilia watani wetu, kipindi cha Moi kule Kenya kuna wakati waliregister close to 0% maana yake pato la mwaka ulipita na la mwaka husika... ni hilo hilo... Leo hii kwa nchi kama ya yetu, kwa mfano, tunatakiwa ili tuwakimbilie watani wetu wao uchumi ukikua kwa 5% sisi tunatakiwa ukue kwa 10 au 12%. kwa sababu mapato yetu ni madogo kulinganisha na wao...

Huu ndio uelewa wangu!!! nachangia tu.

Kilitime,
(A) Nakubaliana na wewe ndio maana reference yetu ni historical data kama mwaka jana au sector husika kwa mfano kwenye nchi, reference yetu inaweza kuwa Kenya na Uganda

(B) Hiyo ni complicated zaidi ya ulivyoweka maana 100 ya mwaka jana sio sawa na 100 ya mwaka huu, lakini kuwasaidia ambao hesabu zinawapiga chenga tunaweza ku assume hivyo.

(C)Hapo hauko sahihi, percentages na rations ndio zinatumika muda wote kwenye analysis za uchumi. Ila tu hizo ratio hazina maana yoyote kama hutumii kulinganganisha na miaka ya nyuma au sector performance. Hatuangalii ukubwa wa figure na badala yake tunaangalia ratios. Kama una pesa zako utawekeza kwenye kampuni
kubwa yenye mabilioni ambayo inakua kwa asilimia 3 au utawekeza kwenye kampuni ndogo ambayo inakua kwa asilimia 10? Mimi nitawekeza kwenye kampuni ndogo kama risks za kampuni hizi mbili ni sawa.

Kwenye (c) sasa usipotumia percentage au ratios kulinganisha utatumia nini? Usahihi ni kwamba unatumia hizo percentage ila kinachotakiwa ni hicho cha kwamba hizo percentage inatakiwa ziwe zinapanda na sio kuwa constant au kushuka. hata hizo ratios hazina maana mpaka kama unalinganisha na sector husika au kulinganisha na miaka ya nyuma.

(D) Kama uchumi wa nchi haukui hata kwa asilimia ndogo, hiyo ni hatari maana kama hayo mapato yalikuwa yanakuwezesha kulipia wafanyakazi 1000, ina maana kwa pato hilo hilo huwezi kuwalipa hao wafanyakazi 1000, ndio maana ni muhimu uchumi kukua kila mwaka kwa zaidi ya inflation. Kwa west inflation yao iko chini sana na pia uchumi wao ni mkubwa kwahiyo hata ukikua kwa asilimia 2 ni sawa lakini kwa TZ kiasi kama hicho hakikubaliki maana unaweza kukuta population imeongezeka kwa asilimia 6, uchumi asilimia 2, ina maana nchi ni maskini kuliko mwaka jana.
 
Mchumi mzuri ni yule mwenye first degree ya Maths ama Engineering na anapokwenda kufanya MA/MSc anaingia kwenye fani ya uchumi na anaunga mpaka PhD. Wasomi wa zama za akina Ngasongwa (sijui kama ni mchumi) hawa-fit tena kwenye ulimwengu wa wachumi wa zama hizi. Ndiyo maana US wanataka mtu anaekwenda kufanya graduate program ya uchumi lazima awe na very strong background in maths!

Keil,

Kwahiyo sijachelewa mkuu? Basi nikajiandikishe Ph.D ya online! kwi kwi kwi!!!

Chuo nilikosoma, Watanzania walokuwa wanasoma uchumi walichemka sana miaka ya mwanzoni, walikuwa hawajui maths wakati kwenye programs zao hesabu zilipewa nafasi kubwa miaka ya mwanzoni.

Hivi bado unaweza kuingia BA Economics mlimani hata kama hujui maths?
 
Sidhani; hata hivyo msivi-exaggerate sana umuhimu wa maths, teeh teeh heee!

Kwi kwi kwi!!! Si unajua hapa UK, huwezi kwenda university kama huna at least C ya Maths na English kwenye GCSE?

Nafikiri nyumbani hasa hiyo miaka tulikosa msisitizo wa English kwa watu wa Science na Maths kwa watu wa Arts. Huenda hayo masomo mawili yana faida kwa watu wote.
 
Kuna haja ya kuvijua vigezo vinavyotumika katika kupima ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Mimi naamini kabisa kwamba ama ukusanyaji wake una kasoro kubwa sana au computations zake zina walakini. Haiwezekani uchumi wa nchi ukue kwa 5% au zaidi kwa miaka karibu 10 mfululizo na kusiwe na ongezeko la ajira na kipato.
 
Mimi nadhani tatizo kubwa la siasa za uchumi ni pale tunapofungwa kamba na hili neno lenyewe kuwa uchumi Unakua....
Ebu tutazame kitu kimoja ambacho nakumbuka nilikuwa nikibishana sana na mheshimiwa ndugu Augustine Moshi kule bcstimes wakati wa Mkapa.
Unajua ikiwa mwaka 2000 uchumi ulikuwa ukiongezeka kwa asilimia mathlan 10, kisha 2001 ukashuka kwa asilimia labda 2 hivyo hivyo kwa miaka mitano tukafikia kusema uchumi wetu haukui kabisa ama negative, basi siku utakapo rudi kuanza kupanda juu tutaanza kudai uchumi unakua kama vile mtu alotoka ktk comma kupata nafuu. Hii ni hatari kubwa sana na inahitaji uangalifu mkubwa zaidi na pengine utafiti zaidi kuliko kutangaza ushindi.
Tatizo kubwa la wanasiasa wetu hasa utawala huu ni pale uchumi wa nchi unapokuwa unaanza kupata nafuu, hali inaanza kuonekana kuwa na afueni ktk baadhi ya sekta (viungo) wao hudai tayari maendeleo yameanza na ndege inapaa hali viuongo vingine ndio kwanza vinaanza kushambuliwa na virusi kiasi kwamba nguvu ya kushambulia organs hizo kunampa mtu mshtuko wa hisia za uhai. Huyu mtu hajapona bado na pengine mtasikia kesho yake katutoka kisha mnaanza kuulizana imekuwaje wakati jana tu ndio kwanza aliweza kuinuka akaenda chooni mwenyewe na kula kapata, leo mnatuambia kaondoka!..
Hii ndio hofu yangu kubwa sana ya uchumi wetu hasa Tanzania kwani virusi wanaokula organs za uchumi wetu zinazidi kutapakaa na kama alivyo mgonjwa wa ukimwi, kesho tutakuja shikana Uchawi.
 
Kuna haja ya kuvijua vigezo vinavyotumika katika kupima ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Mimi naamini kabisa kwamba ama ukusanyaji wake una kasoro kubwa sana au computations zake zina walakini. Haiwezekani uchumi wa nchi ukue kwa 5% au zaidi kwa miaka karibu 10 mfululizo na kusiwe na ongezeko la ajira na kipato.

Bubu AK I made the same point earlier, lakini hata kama uchumi unakua kweli katika rate hiyo angalia population growth pia inachangia kuchelewesha a meaningful takeoff in theory for at least 18 years.
 
Pundit,
kweli kabisa mkuu tena kuna factors nyingi sana Tanzania ambazo zinachangia sana ktk kuturudisha nyuma yaani ni sawa na mtu anayepokea millioni 2 lakini ndio ana nyumba kibao akijulikana kama ATM machine ama Buzi.
Sasa hatuwezi kukataa ukweli kuwa ana mshahara mkubwa lakini inapofikia kuangalia nyumba anazolisha kisha matumizi yake huyu Pedejee (President Director General - PDG) ndipo tunapokoma ubishi.
 
Back
Top Bottom