Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Quote:-

"Tumieni vyombo vya habari kueneza sera za chama na sio kwenda kujitangaza wenyewe na kutaka kuonekana kwenye TV kila siku. Kama ni umwamba wenu si onyesheni kwenye vikao vya CHADEMA? Huko toeni hoja za nguvu na pambaneni kimawazo lakini mkitoka hapo, mnatekeleza lile mlilokubaliana nalo."

Maneno mazito sana mkuu, na yanahitaji kuzingatiwa na wahusika.
 
this is a big joke yaani watu wawili kutokubaliana katika Chama wanatishia chama kusambaratika,chama hakitajengwa na watu wawili au popularity ya watu wachache,wapinzani better be serious sasa kama wanataka kushinda na kuanza kujenga chama as institution based kuliko kutegemea mtu mmoja mmoja...no wander upinzani TZ uko weak sana!
 
Quote:-

"this is a big joke yaani watu wawili kutokubaliana katika Chama wanatishia chama kusambaratika,chama hakitajengwa na watu wawili au popularity ya watu wachache,wapinzani better be serious sasa kama wanataka kushinda na kuanza kujenga chama as institution based kuliko kutegemea mtu mmoja mmoja..."

Mkuu Koba,

Heshima mbele, nimeyasema sana haya kwa muda mrefu kuwa hatuwezi kuwapa madaraka chama cha watu watatu, Chadema iongeze viongozi wakuu, na kina Mwanakijiji wapewe nafasi huko bila hata kugombea, maana this is a very serious national political ishu, misunderstanding ya viongozi wawili tu wanapotishia kusambaratisha chama popular kama Chadema, sasa what is there left kwetu wananchi kuamini?
 
unajua mwisho wa hawa watu 2 utakuwa nini?at the end MKUU WA KAYA WA HULL UNIVERSITY ataamua kuachia ngazi na kuwaachia CW na ZK hapo tena ndio uwanja utakapokuwa hautoshi.
tusubiri tuone.
 
Quote:-

"this is a big joke yaani watu wawili kutokubaliana katika Chama wanatishia chama kusambaratika,chama hakitajengwa na watu wawili au popularity ya watu wachache,wapinzani better be serious sasa kama wanataka kushinda na kuanza kujenga chama as institution based kuliko kutegemea mtu mmoja mmoja..."

Mkuu Koba,

Heshima mbele, nimeyasema sana haya kwa muda mrefu kuwa hatuwezi kuwapa madaraka chama cha watu watatu, Chadema iongeze viongozi wakuu, na kina Mwanakijiji wapewe nafasi huko bila hata kugombea, maana this is a very serious national political ishu, misunderstanding ya viongozi wawili tu wanapotishia kusambaratisha chama popular kama Chadema, sasa what is there left kwetu wananchi kuamini?

mzee ES......

ru serious kweli?yaani wapewe akina mkjj?mhhhhh nina wasi kwa hilo,unajua hizi siasa za TZ ni kuganja njaa tu.tumeshawaona wengi tu walikuwa wasemaji wazuri sana lakini walipopewa madaraka wakafunga midomo,zaidi ya kupeleka watoto wao kwenda S.AFRIKA kusoma na wao wenyewe kila leo semina na safari THATS all.wapi leo SSH(CUF),G55 etc wote kimya.

NAKUTAKIA KHERI YA MWAKA MPYA 2008.
 
Quote:-

"this is a big joke yaani watu wawili kutokubaliana katika Chama wanatishia chama kusambaratika,chama hakitajengwa na watu wawili au popularity ya watu wachache,wapinzani better be serious sasa kama wanataka kushinda na kuanza kujenga chama as institution based kuliko kutegemea mtu mmoja mmoja..."

Mkuu Koba,

Heshima mbele, nimeyasema sana haya kwa muda mrefu kuwa hatuwezi kuwapa madaraka chama cha watu watatu, Chadema iongeze viongozi wakuu, na kina Mwanakijiji wapewe nafasi huko bila hata kugombea, maana this is a very serious national political ishu, misunderstanding ya viongozi wawili tu wanapotishia kusambaratisha chama popular kama Chadema, sasa what is there left kwetu wananchi kuamini?

Mkuu FMES

Hayo maneno in bold ni ya kweli hapo juu?
 
Pendekezo kwa Mwenyekiti wa Chadema,

Huu ni wakati muafaka wa wewe kutumia emergency powers ulizopewa na katiba ya Chadema, kuwateua kwenye kamati kuu kwa muda hawa wana JF wafuatao:-

Kitila mkumbo, Mwanakijiji, Jasusi, Kithuku, Gamba La Nyoka, Nyani Ngabu, Rev Kishoka, Mwafrika Wa Kike, Ogah, Dua, Mtanzania, Masatu, na Mkandara.

JF hatuwezi kunyamza kimya kuona mifarakano isiyokuwa na kichwa wala miguu ndani ya chama chenu, ambacho tunakiheshimu kama chama cha taifa kwa kuhusika haswa katika kuwakosesha usingizi tembo waliolala CCM. Hata ziwekwe political spin za namna gani hapa JF, ukweli unaendelea kujiweka kweupee kuwa huko ndani mambo si salama, sasa JF hatuwezi kukaaa pembeni tu kupiga domo tu, kwa hiyo tuko tayari kuwasaidieni ma-expert hapa kuja kuweka hali sawa, mpaka hali itakapokuwa sawa,

Hawa waingizwe moja kwa moja kamati kuu, na kamati ya ufundi, I have all the trust kuwa watanyooosha yasiyonyoosheka huko ndani, all we care hapa ni taifa tu, na sio majina ya viongozi, maana ninawahusia kuwa mkifanya mchezo you will never recover kutoka kwenye hi stress, maana CCM hawatawapa hiyo nafasi, CCM huenda wanayo matatizo mengi kiutawala, lakini one thing they know better kama history inavyotuonyesha ni kusambaratisha upinzani, if you think what is going on sasa ni a small external political problem, then wait and seee what is coming!

Pokeeeni hawa wakuu mkinusuru chama tuendelee kuwaamsha wananchi, otherwise you are doomed! na ninataka mjue kuwa hatufurahishwi na mnayoyafanya sasa n hasa haya ya kupigiana kelele kwenye media za mjumbe wa kamati kuu ya CCM, Rostam!

Yes, I said it and I am dead serious!
 
FMES,
Naona hunitakii mema ndugu yangu. Sasa nikishateuliwa kwenye kamati kuu ya Chadema si itabidi ujasusi uishe?
 
Wana JF,
Kuna masuala ambayo huwa yanachanganywa mno na ninaona ni bora nifafanue hapa.

Kwanza, Uchumi unapimwa kwa Pato la Taifa, kimombo GDP. Tukisema uchumi unakua maana yake ni kwamba Pato la Taifa limekua. PT ni jumla ya kipato cha kila mtu, au kila factor of production katika taifa husika. Kwa kuwa ni vigumu sana kukokotoa pato la kila mtu, Tanzania na nchi nyingine nyingi changa, hupima Pato la Taifa kwa kuangalia thamani ya uzalishaji kwa kila sekta. Hivyo uchumi hugawiwa kisekta na rekodi ya uzalishaji kuchukuliwa.

Pato la Taifa sio mapato ya TRA au mapato mengine ambayo serikali hukusanya. Hayo huitwa mapato ya serikali na utendaji wa serikali na uwezo wa serikali kujitegemea pia hupimwa na kiasi cha mapato kama asilimia ya Pato la Taifa. Kiwango cha kimataifa ni asilimia 25. Tanzania tumefikia asilimia 16 hivi ya mapato kama asilimia ya Pato la Taifa.

Hivyo, tunaposema uchumi umekua tuna maana kuwa Pato la Taifa limekua, na hatuna maana kuwa Mapato ya Serikali yamekua. Ingawa Uchumi unapokuwa tax base inaongezeka ie wigo wa kukusanya kodi unaongezeka kutokana na kuongezeka shughuli za uzalishaji katika Taifa.

Bwana Zitto,

Nashukuru kuchukua kwako muda kutupa upande wako wa habari hii ambayo kidogo imeleta tafurani na mawazo na maoni elfu kuhusu Uzalendo wako katika Mageuzi.

Langu moja. Pamoja na jitihada zako na za Serikali kutupa Takwimu za kiuchumi (Statistical data) ambazo ni Complex kwa mwananchi wa kawaida, ni vipi kutumia simple terms utamhakikishia Mtanzania kuwa Uchumi unakuwa ilhali yeye msoto ni mkubwa na unaongezeka?

Ajira ni ngumu na mapato ni adimu, gharama za maisha haziendani na vipato, nyongeza ya mishahara haiendani na kipato, huduma za muhimu kama Elimu, Afya, Maji, Nishati na hata Barabara na Chakula ni shida. Jee kukua huku kunawiana vipi na maendeleo na kiu ya Mtanzania aliyeko Isanzu, Kabondo, Ikizu, Chakechake ambaye shida yake ni kuona anaachana na nyumba ya tembe na anaezeka bati?

Ni vipi chama chako cha Chadema kitaachana na Takwimu kubwa na kutumia vitendea rahisi kumpa Mtanzania huyu tumaini kuwa safari ya Ujamaa na Kujitegemea katika kuondoa Umasikini, Ujinga na Maradhi ni kweli inaendelea mbele na MKUKUTA itafikia malengo?

Ni lini Mtanzania ataacha kusikia visingizio vya jua kali, uhaba wa maji na mvua, Umeme shida (IPTL, RDC?) na kuimbiwa kila siku eti ni hali halisi huku anasikia kuwa Mwakilishi wake (ambaye badala ya kumtumikia yeye mwananchi anakitumikia chama) kapewa Shangingi jipya na kuongezewa kipato cha mshahara na marupurupu marudufu?
 
Ukweli ni kwamba jamaa wanahitaji msaada tena wa dharura, na wanauhitaji sasa, haya ya kina Wangwe sio bure, toka kamati ya madini iungwe hakujawa na amani huko ndani, we know better reading between the lines hapa JF, huhitaji kwenda huko ndani kujua kuna problem unahitaji kusoma kwa makini tu maoni ya watu huko ndani hapa JF kujua kuwa hakuna amani huko,

Sasa sisi watu wazima wapenda mendeleo na mabadiliko ya taifa letu, hatuwezi kukaaa tu hapa na kushangilia au kutofanya kitu, ndio maana ninasema tuwape msaada hawa ndugu zetu niliiwaambieni siku nyingi sana kuwa baada ya miaka 45 kwenye madaraka, msitegmee CCM siku moja itawapa power just like that,

Sasa hivi it is very clear what CCM has done and not done, kwanza wametishia kwenda mahakamni, pili wametuma mawaziri wao kuzunguka bongo nzima, tatu wamenyimana vyeo kule Dodoma, it did not work, sasa wameamua kutumia ile gear yao kali kwa kisingizio cha kamati ya madini, kwa mara ya kwanza it is working, guys mmepigwa bao tayari, na wa kuumia na hili bao ni sisi wananchi at large, yaani walalahoi, kubalini sasa mmpewe msaaada,

Ni ushauri wangu wa bure tu kwa Chadema!
 
FMES,

Mimi toka jana nimeshinda kule kwa Wakenya. Naisubiri siku ambayo CCM itaporomoka, mizee kulazimishwa kung'atuka na vijana kuchukua uongozi wa chama.

Ili hayo yafikie lazima CCM wapigwe mweleka kwanza. Tunahitaji kuunganisha nguvu kama ODM ili kuwaondoa hawa majangili na genge lao. Ni makosa makubwa kwa viongozi wa upinzani kuanza kuoneshana mabavu yao. CCM wakigundua tu aina fulani ya udhaifu miongoni mwa upinzani, wataitumia ipasavyo.

Muhimu: Kumwondoa bingwa lazima iwe kwa knockout vinginevyo tutaishia kusema tumejitahidi na kutolewa kwa point, kwa CCM hawajali ni ushindi wa points au knockout, wanachojali ni kubaki madarakani.
 
Hata mimi nimeshinda kule mpaka kilipoeleweka. Ni kweli hatuwezi kufanya chochote bila kuunganisha nguvu zetu. CCM is giant, we need equally or even more giant forces to take it down. Na tunapoongelea nguvu hapa inabidi twende zaidi ya vyama vya siasa. Lazima tuwahusishe vyama vya kiraia, taasisi za dini, activists (hivi tunao kweli hawa?) and everybody who is fed up with CCM. Tatizo moja la TZ ni kwamba taasisi za kiraia na kidini zimejitenga kabisa na mambo ya siasa. Lakini historia inaonyesha kote palipotokea mabdailiko makubwa vyama vya siasa, wasomi, civil society organisations, mashirika ya dini, n.k. walishirikiana.

Bahati nzuri ya Kikwete (I maybe wrong)pamoja na matatizo yake lukuki, anaonekana ni mvumilivu kwa kiasi fulani. Kwa hiyo nahisi kwamba pale patakapotokea kwamba chama chake kikapigwa chini katika uchaguzi halali anaweza asitumie maguvu kung'ang'ania ushindi. Tofauti ni lile lijamaa lilivyokuwa linaing'ang'aniza CCM kushinda hata pale ambapo haiwezekani.
 
Kitila, Kikwete bado hajasukumizwa vya kutosha. Pia naamini tatizo siyo kuungana wala kushirikiana na muungano wenye lengo la kuiondoa CCM madarakani unamsingi mbovu kwani baada ya kuiondoa CCM madarakani what next? Yaliyotokea Kenya ndio haya ya kutaka kuiondoa KANU na baadaye walipopata nchi wapinzani wenyewe wakameguka.

Na anayefikiria kuwa Raila ndiye ataiunganisha Kenya na kuleta yale matumaini naye anaweza kujikuta na matatizo kwani baada ya miaka mitano (assuming ndiye mshindi) wa Kenya watajikuta wana matatizo yale yale na watatamani Kibaki arudi n.k !

Kuungana msingi wake usiwe kuingoa CCM bali matokeo yake yawe ni CCM kuanguka! Tafuteni msingi wa kuungana uwe ni nini?
 
Msingi wa kuungana ni kukusanya nguvu na kuiondoa CCM. Kuiondoa CCM madarakani ni kuondoa mafisadi na wezi waliotapakaa ktk kila kila sehemu ya serikali. Kuiondoa CCM kutaipa fundisho kuwa Watanzania sio wajinga na wamechoshwa na mashenanigans yao na wanataka timu na safu mpya ya uongozi ulio bora na unaojali maslahi ya taifa kwa ujumla na si matumbo yao. Hopefully CCM itakaa chini na kuona wapi walichemsha, kufix kasoro walizonazo, na kukaa mkao wa kula just in case hiyo timu mpya nayo inachemsha.
 
Mwanakijiji: CCM is itself a problem which is in turn a source of so many other problems troubling our country. Kwa hiyo kuitoa CCM tu already ni achievement. Unajua ukiwa unaumwa na umeshambuliwa na wadudu wanaosababisha huo ugonjwa unachotaka kwanza ni hao wadudu wafe/watoke, na unajua kabisa kwamba hao wadudu wakitoka utakuwa umepona, na ukipona maanake utaendelea na shughuli zako kama kawaida. Kwa hiyo tatizo letu la kwanza hapa ni CCM kuwa kikwazo cha sisi kufanya kazi zetu za kawaida za kujiletea maendeleo kwa wao ku-diverge attention yetu-matokeo yake hatuwezi kusoma, kulima, kufanya kazi vizuri maofisini, n.k. kwa sababu tumenyong'onyeshwa na huyu kirusi CCM. Kwa hiyo mzee wangu kumtoa CCM itafungua milango kwa mambo mengine mengi sana.

That said, nimeshasema hapa siku za nyuma kwamba tatizo la nchi yetu/zetu sio kukosa sera au ajenda; ajenda zipo tu sio za kutafuta: kujenga mabarabara,kumaliza njaa, kutokomeza maradhi yanayozuilika (malaria, etc) etc etc. Hata ukamwake mwanafunzi wa drs la 7 kuwa rais wa nchi lazima afanye haya kama ana uwezo na commitment. Ugomvi wetu na CCM ni kwamba wamepoteza uwezo na committment ya kuyafanya mambo ya kijamii. Kazi yao imebaki kupeana zamu ya kuongoza ili wachuna mali kisha waporomoshe majumba milimani kama alivyofanya kakako Mkapa.
 
That said, nimeshasema hapa siku za nyuma kwamba tatizo la nchi yetu/zetu sio kukosa sera au ajenda; ajenda zipo tu sio za ana kutafuta: kujenga mabarabara,kumaliza njaa, kutokomeza maradhi yanayozuilika (malaria, etc) etc etc. Hata ukamwake mwanafunzi wa drs la 7 kuwa rais wa nchi lazima afanye haya kama ana uwezo na commitment. Ugomvi wetu na CCM ni kwamba wamepoteza uwezo na committment ya kuyafanya mambo ya kijamii. Kazi yao imebaki kupeana zamu ya kuongoza ili wachuna mali kisha waporomoshe majumba milimani kama alivyofanya kakako Mkapa.

Mzee Kitila CCM ni tatizo na dawa yake ni kuing'oa. KIlio changu ni vile hata tuliowategemea kwenye upinzani, ambao mlikuwa mwiba kwao, mnawapa sababu ya kukejeli upinzani. Ikiwa chama kimoja kimoja kitakosa nguvu ya kuiondoa upinzani, na kuungana vyama inakuwa ngumu, CCM itakuwa donda ndugu lisilotibika na sisi wote tutakuwa wa kulaumiwa
 
Pendekezo kwa Mwenyekiti wa Chadema,

Huu ni wakati muafaka wa wewe kutumia emergency powers ulizopewa na katiba ya Chadema, kuwateua kwenye kamati kuu kwa muda hawa wana JF wafuatao:-

Kitila mkumbo, Mwanakijiji, Jasusi, Kithuku, Gamba La Nyoka, Nyani Ngabu, Rev Kishoka, Mwafrika Wa Kike, Ogah, Dua, Mtanzania, Masatu, na Mkandara.

JF hatuwezi kunyamza kimya kuona mifarakano isiyokuwa na kichwa wala miguu ndani ya chama chenu, ambacho tunakiheshimu kama chama cha taifa kwa kuhusika haswa katika kuwakosesha usingizi tembo waliolala CCM. Hata ziwekwe political spin za namna gani hapa JF, ukweli unaendelea kujiweka kweupee kuwa huko ndani mambo si salama, sasa JF hatuwezi kukaaa pembeni tu kupiga domo tu, kwa hiyo tuko tayari kuwasaidieni ma-expert hapa kuja kuweka hali sawa, mpaka hali itakapokuwa sawa,

Hawa waingizwe moja kwa moja kamati kuu, na kamati ya ufundi, I have all the trust kuwa watanyooosha yasiyonyoosheka huko ndani, all we care hapa ni taifa tu, na sio majina ya viongozi, maana ninawahusia kuwa mkifanya mchezo you will never recover kutoka kwenye hi stress, maana CCM hawatawapa hiyo nafasi, CCM huenda wanayo matatizo mengi kiutawala, lakini one thing they know better kama history inavyotuonyesha ni kusambaratisha upinzani, if you think what is going on sasa ni a small external political problem, then wait and seee what is coming!

Pokeeeni hawa wakuu mkinusuru chama tuendelee kuwaamsha wananchi, otherwise you are doomed! na ninataka mjue kuwa hatufurahishwi na mnayoyafanya sasa n hasa haya ya kupigiana kelele kwenye media za mjumbe wa kamati kuu ya CCM, Rostam!

Yes, I said it and I am dead serious!

Ha ha haaaa aaaaaaaaaa.............. Naona mkuu hapa umeteleza, kwanza wengine hatuna vyama tuko independent halafu huna habari kwamba Masatu na Mbowe ni paka na panya. Naona kweli umeamua kufurahisha baraza. Tuendelee kumkoma nyani kwa maslahi ya Tanzania then vyama vya siasa.
 
Mkuu Dua,

Heshima mbele, tunawatumeni huko kurekebisha mambo kwa kuweka taifa letu mbele, the big picture ni Tanzania, forget about vyama hapa, wanaotaka vyama zaidi ya taifa, hatuwataki, kwenda chni kwa Chadema, means wananchi wote wapenda mabadiliko na maendeleo kwa taifa letu tutaenda chini,

Mimi ni CCM damu, lakini siwezi kuota kuwa na Tanzania ya bila Chadema, no way! Kwa hiyo mkuu ninakuomba uichukulie hii ishu very serious, sio wakati wa kucheka huu mkuu maana one big mistake on Chadema wote tumepigwa bao, Karamagi Waziri Mkuu Mpya! do you like that? Mambo ya kupigizana kelele kwenye magazeti ya Rostam, what is there to be gained kwa Chadema na sisi wananchi at large kwa ujumla? jawabu ni hakuna, sasa lets talk seriously kuhusu yanayojiri sasa hivi huko ndani ya Chadema, kwa sababu hayawezi kutusaidia sisi wananchi walalahoi kabisaa, haya makelele ya Wangwe na Zitto, yanafanikisha only one thing tena kwa upande wa mafisadi yanampunguza nguvu Mheshimiwa Zitto, na as long as Zitto anaondoa focus ya taifa na kuanza kujibizana na Wangwe kweye media za Rostam, basi mafisadi wanakuwa ndio washindi,

Now do not get me wrong, sijui kabisa chanzo cha makelele haya ya huko Chadema, lakini ninaamini kuwa kuna "something" ambacho viongozi wa Chadema wanakijua lakini hawataki kusema, na hivyo kuficha maradhi kama viongozi wetu wa CCM halafu baadaye ugonjwa na kifo utakuja kuwafichua, na itakuwa too late, ndio maana tunasema sasa kuwa huko chadema, msaada unahitajika tena sana mambo sio sawa huko na guess nani atakayelipia?, ni sisi wananchi walalahoi!

Sasa JF hatuwezi kukaa tu hap kupiga domo tu, lazima tuwajibike kwa kuwasaidia ndugu zetu, hasa kwa mawazo, kumbuka bin-adam huenda chini pale anapofikiri yupo juu na kwamba hahitaji msaada wa mawazo! Uzuri wa mchezo wa mpira huonwa na kusemwa na watazamaji sio wachezaji, kwenye hili la Wangwe watazamaji tumeshaona kuna mdudu kakauona!
 
Mwanakijiji: CCM is itself a problem which is in turn a source of so many other problems troubling our country. Kwa hiyo kuitoa CCM tu already ni achievement. Unajua ukiwa unaumwa na umeshambuliwa na wadudu wanaosababisha huo ugonjwa unachotaka kwanza ni hao wadudu wafe/watoke, na unajua kabisa kwamba hao wadudu wakitoka utakuwa umepona, na ukipona maanake utaendelea na shughuli zako kama kawaida. Kwa hiyo tatizo letu la kwanza hapa ni CCM kuwa kikwazo cha sisi kufanya kazi zetu za kawaida za kujiletea maendeleo kwa wao ku-diverge attention yetu-matokeo yake hatuwezi kusoma, kulima, kufanya kazi vizuri maofisini, n.k. kwa sababu tumenyong'onyeshwa na huyu kirusi CCM. Kwa hiyo mzee wangu kumtoa CCM itafungua milango kwa mambo mengine mengi sana.

That said, nimeshasema hapa siku za nyuma kwamba tatizo la nchi yetu/zetu sio kukosa sera au ajenda; ajenda zipo tu sio za kutafuta: kujenga mabarabara,kumaliza njaa, kutokomeza maradhi yanayozuilika (malaria, etc) etc etc. Hata ukamwake mwanafunzi wa drs la 7 kuwa rais wa nchi lazima afanye haya kama ana uwezo na commitment. Ugomvi wetu na CCM ni kwamba wamepoteza uwezo na committment ya kuyafanya mambo ya kijamii. Kazi yao imebaki kupeana zamu ya kuongoza ili wachuna mali kisha waporomoshe majumba milimani kama alivyofanya kakako Mkapa.

Nyani na Kitila, labda niongeze kidogo hapa.

Tatizo ni CCM, hili halina shaka na halina mjadala. Tatizo la CCM ni zaidi ya watu au chama kilichoko madarakani. Tatizo ni mfumo ambao umekiweka chama hicho madarakani na mfumo ambao unafurahisha wale walioko madarakani (kwa sasa ni CCM). Kuendelea kwa kile kilichopo (Status quo) ndicho kinachopiganiwa na CCM kuendelea kushikilia madarakani.

Hata hivyo huu mfumo ndio uliotengeneza watu walioko madarakani; hivyo tatizo la mfumo ni tatizo la watu walioko madarakani ambao wanaulinda mfumo uliopo na gurudumu linazunguka. Sasa tubadili nini? Kubadili CCM kama chama na watu kuwaondoa madarakani ni kubadili sehemu ya tatizo ambalo kimsingi ni rahisi zaidi.

Kuwaondoa watu madarakani ni jambo rahisi, linalowezekana na linalopaswa kutokea. Hata hivyo kufanya hivyo wapinzani hawahitajiki! Hapa ndipo maneno ya Mwalimu "upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM" una maana. Endapo kwa mfano, CCM watakaa chini na kuona tatizo lao la watu na mfumo (hilo la mfumo niliweke pembeni kwa sasa); wakaamua kubadilisha watu basi wanaweza kuwazidi kete wapinzani.

Endapo kwa mfano vitu viwili vinafanyika (ingawa uwezekano wa hilo ni duchu) basi kuna kila dalili ukuta wa kuzuia wapinzani kuchukua madaraka utainuliwa juu zaidi. Endapo Rais atavunja baraza na kuliunda upya kabisa na kuwatupa nje ya utawala watu kadhaa na kuwaingiza watu ambao wananchi wanawaamini; wapinzani watakosa hoja ya kubadili watu (kwani CCM itakuwa imefanya) na la pili endapo kabla ya 2010 unafanyika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wa kubadili mifumo ndani ya chama kukifanya kiwe cha demokrasia zaidi, wazi zaidi na kinachowajibika zaidi kwa wananchi, wapinzani watanyang'anywa hoja ya mfumo.

Sasa, hapa ndio unaona tatizo la kuweka "kuing'oa CCM" kama lengo lilivyo. CCM inaweza kabisa kucheza kiufundi na kuwanyang'anya hoja wapinzani (political triangulation) na wapinzani wakajikuta wameungana lakini hawana cha kuondoa!

Sasa lengo liwe nini? Kwa vile kubadili watu siyo tatizo kubwa zaidi na ambalo ni rahisi kulishughulikia, basi wapinzani watakapoamua kushirikia wasiweke lengo kuondoa watu bali kubadili mfumo na kuleta mabadiliko katika nchi. Mabadiliko ya muundo na mfumo uliojenga ufisadi ambao kubadilishwa kwake ndiko kutasababisha kuanguka kwa CCM.

Leo hii Kenya wamewaangusha Mawaziri 16 na bila shaka watamuondoa Rais wao lakini watafanya hivyo kama matokeo ya kuamua kuangusha mfumo mbovu uliopo licha ya mafanikio ya kiuchumi chini ya Kibaki.

Sasa tunapoamua kuweka lengo la kuleta mabadiliko katika mfumo na muundo basi ni rahisi zaidi kama Taifa kubadilishana uongozi. Hata hivyo kuna sababu nyingine au msingi mwingine ambao wapinzani wanaweza kuutumia kama msingi wa kuungana kwao. Nitaendelea...
 
Back
Top Bottom