Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Field Marshal Es,

Mkuu wangu shukran tena huwezi amini kuwa nafikiria kufungasha virago vyangu huku kwenda beba gobole langu kwa uchungu mkubwa kwani haikutakiwa kufikia haya, Siasa naziogopa sana!...hao kina Ghandi mfano bora.
lakini pamoja na yote haya nakuomba ukumbuke yale yaliyotukuta kule Bcstimes tukaanza kufikiriwa kuwa ni watu tunaounda chama Chama cha Mapinduzi. wapo jamaa zangu hawaingii tena hapa kutokana na mshikemshike walokutana nao wakati ulee!..

Pia kama bado unakumbuka, kati ya hoja nzito za mwaka huo 2002 ama 2003 ( duh, miaka inayoyoma kweli) kulikuwa na swala la Tanzanite... ambalo serikali yetu ilitupa figure tofauti kitu kama 10% tu ya total production kisha takwimu za kimataifa zilpotoka watu tukakiamsha...Ni wakati huo huo tulifungiwa kwa mara ya kwanza maanake ushahidi ulikuwepo wazi kuonyesha kuwa Tanzanite ilikuwa ikiibiwa vibaya sana.

Madai nyao yalikuwa wezi ni wananchi wachimbaji wenyewe, then why wasiweke mipango na sheria ambazo zitazuia wizi kama huo. Sii ndio kazi ya serikali kuweka policy zinazolinda maslahi ya taifa! - tena basi, walisema hivyo hivyo kuwa uchumi umekua hali figures wanazotupa ni tofauti kabisa na ukweli wenyewe. kwa hiyo mzee wangu, kwa kuelewa hivyo ndio maana niliendelea kushika kamba ya Mheshimiwa Zitto hadi alipofika yeye mwenyewe kuthibitisha kile alichokisema.

Hawa mafisadi wamezoea sana kutudanganya. Maghala yetu yamejaa mali lakini wanaweka tobo zao, mirija na kufyonza toka ktk main reserves kisha wanataka sisi tukubali kuwa hakuna kitu isipokuwa kile tunachokiona... na wamekuwa wajuzi sana wa kutumia neno hili sisi maskini hai wao wakijilipa mishahara mikubwa kuliko hata viongozi wa nchi za magharibi. majumba yao masafari yao yaani huu umaskini wetuinabidi kuutazama upya na kwa mwanga mkubwa zaidi.

Waibe lakini basi wajenge kitu kionekane lakini kuiba mtaji kisha kusingizia umaskini nasi tukakubali kuwa kweli uchumi wetu haukui ktk baadhi ya shemu ni kujifunga wenyewe kwani ni wendawazimu kudai kuwepo kwa Mafisadi. Ni muhimu kwa Zitto kusema alosema ili kuweza kuleta mantiki ktk yale alokuwa akiyasema.

Sasa basi kisera nadhani tofauti kubwa iliyopo kati ya CCM na Chadema ni pale tunapoweka vipaumbele vyetu. Mathlan Chadema wanaweza kuwa waamini kuwa maendeleo yetu yatatokana na kilimo na wakakipa nafasi zaidi ya CCM lakini tunapofikia kulinda maslahi ya viingizio hivi hakuna sera ila ni uzalendo wa kusema na kukubali kinachovunwa kuwa kipo isipokuwa... balaa blaa blaaa.
 
Mwanakijiji, kwa watu walio werevu watajiuliza: nyinyi mlikuwa wapi miaka yote hii na sasa ndio mnaamua kubadili mifumo ya utawala wenu? Ina maana mlikuwa hamjui kuwa mna mfumo mbovu?

Na nini kitakachotufanya tuwaamini sasa hivi kuwa haya mabadiliko yenu ni ya kweli na ya nia njema na si kujichotea kura tu ili muendelee kutawala?

For me, I would tell them, you people have had umpteen chances to do what is right for the country but each time you were given one you blew it. Therefore, I don't believe you.

You need to sit out for a minute and do some soul-searching and hopefully next time around you'll come back better, with a purpose and a clear direction of where you want to take the country.
 
Ha ha haaaa aaaaaaaaaa.............. Naona mkuu hapa umeteleza, kwanza wengine hatuna vyama tuko independent halafu huna habari kwamba Masatu na Mbowe ni paka na panya. Naona kweli umeamua kufurahisha baraza. Tuendelee kumkoma nyani kwa maslahi ya Tanzania then vyama vya siasa.

Whistling.........
 
Mojawapo ya magazeti yanayotoka leo nyumbani lina kichwa cha habari "Wangwe ampinga Zitto" kuhusu kauli yake kuwa uchumi wa nchi unakua. Hii si mara ya kwanza kiongozi huyo wa Chadema kumlenga kiongozi mwenzie aidha kwa uharaka wa kuzungumza na waandishi au kutokana na sababu binafsi. Kwa wale wanaokumbuka sakata la madini kule Tarime Wangwe alikuwa ni mmoja wa watu waliopinga sana kuhamishwa wananchi na kuna wakati aliwekwa lupango. Hata hivyo wananchi wa Tanzania wengi hawakumbuki mchango wake huo na harakati zake pamoja na Lissu kuhusu madini.

Hata hivyo hapa anakuja kijana ambaye hajalipa gharama ya uanaharakati na anaanza kuvuna matunda ya kazi za kina Wangwe kwa kuonekana ndiyo "mtetezi wa wananchi". Kwa Zitto kuendelea kutajwa tajwa haimsaidii sana Wangwe.

Wote wawili bila ya shaka ni watu wanaojiamini sana, wako huru kimawazo, wasio tayari kushauriwa na kusikiliza mashauri hayo. Sitashangaa wote wawili ndani ya Chadema wameanza kuwa "maverick politicians".

Wanasiasa hawa wawili wasipoangalia watakuwa ndio chanzo cha mgogoro ndani ya CHADEMA hasa kama wataendelea kutunishiana misuli kwenye vyombo vya habari. Vinginevyo tunachoanza kushuhudia ni vita ya mafahali wawili kama ya Mrema Vs. Marando, Nyerere Vs. Kambona, n.k

Binafsi nina ushauri ufuatao kwa wote wawili:

a. Stop talking to the press each time they extend their mics to you!

b. Tafuteni wasemaji wenu rasmi siyo kila kitu mkitolee maoni "no comment" nalo ni jibu.

c. Inapobidi mzungumze mjue ninyi mnazungumzia chama chenu hakuna kitu kama "maoni binafsi" kwa kiongozi wa chama!

d. Mitazamo yenu inapogongana zungumzeni kabla hayajafika kwenye vyombo vya habari.

e. Pale mnapotofautiana kimsingi na waandishi wanataka kujua, zungumzeni pamoja na waandishi siyo huyu anasema hili akiwa madongo kuinama na mwingine anasema lile madongo kuinuka! Mnawachanganya watu!

f. Kuna vitu vingine msivitoleee maoni hadi msikilize washauri!

Vinginevyo, mtaendelea kugongana hadharani na kuthibitisha kile ambacho Watanzania wanakifahamu kwa muda mrefu, wapinzani wana migogoro ya ndani!

RIP wangwe, Zitto ungeusikia ushauri huu wa Mzee Mwanakijiji usingetufikisha hapa tulipo leo.
 
Last edited by a moderator:
mara nyingi umaarufu unaotokana na mambo mema huwa hauvumi. Umaarufu unaotokana na uovu ndio unaovuma sana na kwa muda mrefu.
1. Nadhani tuna wanasiasa ambao they are still immature both politically and socially. In principle they are using political parties as a platform for their social development (fame)and personal interest.
2. The politics of personalities are difficult to manage and always results into creating irresponsible society.
3. Zitto is famous, lakini hili sio lililomleta kwenye siasa. Anadai anataka kuwatumikia wananchi. sawa, wananchi wapi hao zitto, uliowazaa ndio unataka kuwaua!

Mimi nadhani kuwe na msemaji mmoja tu wa chama kama ilivyo shauriwa na wengine kabla. Na mtu ambae hawezi kufuata taratibu za usemaji katika chama, basi, sio lazima awe kiongozi wa chama. Akapige kelele huko porini kama wengine! Maana wanaoathirika ni wananchi na sio wao au wake zao!
 
Tunaposema maandishi ya JF hayafi nafikiri watu wataanza kuelewa! ifike mahali tumsifie Mzee Mwanakijiji akiwa hai!

Kila mara anayosema yanatokea!
 
Last edited by a moderator:
Kuwa chama kimoja si sababu ya kufanya watu wasitofautiane. tatizo liko kwetu wenye uelewa mdogo ktk mambo ya siasa. Tutatika 2
Mojawapo ya
magazeti yanayotoka leo nyumbani lina kichwa cha habari "Wangwe ampinga
Zitto" kuhusu kauli yake kuwa uchumi wa nchi unakua. Hii si mara ya
kwanza kiongozi huyo wa Chadema kumlenga kiongozi mwenzie aidha kwa
uharaka wa kuzungumza na waandishi au kutokana na sababu binafsi. Kwa
wale wanaokumbuka sakata la madini kule Tarime Wangwe alikuwa ni mmoja
wa watu waliopinga sana kuhamishwa wananchi na kuna wakati aliwekwa
lupango. Hata hivyo wananchi wa Tanzania wengi hawakumbuki mchango wake
huo na harakati zake pamoja na Lissu kuhusu madini.

Hata hivyo hapa anakuja kijana ambaye hajalipa gharama ya uanaharakati
na anaanza kuvuna matunda ya kazi za kina Wangwe kwa kuonekana ndiyo
"mtetezi wa wananchi". Kwa Zitto kuendelea kutajwa tajwa haimsaidii sana
Wangwe.

Wote wawili bila ya shaka ni watu wanaojiamini sana, wako huru kimawazo,
wasio tayari kushauriwa na kusikiliza mashauri hayo. Sitashangaa wote
wawili ndani ya Chadema wameanza kuwa "maverick politicians".

Wanasiasa hawa wawili wasipoangalia watakuwa ndio chanzo cha mgogoro
ndani ya CHADEMA hasa kama wataendelea kutunishiana misuli kwenye vyombo
vya habari. Vinginevyo tunachoanza kushuhudia ni vita ya mafahali
wawili kama ya Mrema Vs. Marando, Nyerere Vs. Kambona, n.k

Binafsi nina ushauri ufuatao kwa wote wawili:

a. Stop talking to the press each time they extend their mics to you!

b. Tafuteni wasemaji wenu rasmi siyo kila kitu mkitolee maoni "no
comment" nalo ni jibu.

c. Inapobidi mzungumze mjue ninyi mnazungumzia chama chenu hakuna kitu
kama "maoni binafsi" kwa kiongozi wa chama!

d. Mitazamo yenu inapogongana zungumzeni kabla hayajafika kwenye vyombo
vya habari.

e. Pale mnapotofautiana kimsingi na waandishi wanataka kujua, zungumzeni
pamoja na waandishi siyo huyu anasema hili akiwa madongo kuinama na
mwingine anasema lile madongo kuinuka! Mnawachanganya watu!

f. Kuna vitu vingine msivitoleee maoni hadi msikilize washauri!

Vinginevyo, mtaendelea kugongana hadharani na kuthibitisha kile ambacho
Watanzania wanakifahamu kwa muda mrefu, wapinzani wana migogoro ya
ndani!
 
Na Zitto kwa wakati huo aliungwa mkono sana na Kafulila
Akaendelea kulewa sifa mpaka akaanza kutumika,na kuwatumia masalia& co.

hongera Mzee Mwanakijiji kwa kumshtukia Zitto akiwa kinda kabisa
 
Last edited by a moderator:
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom