kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,317
- 12,617
Nchi zetu za kiafrika ni vigumu watu wake kutembeleana kwa urahisi bila kukutana na vikwazo mipakani/uhamiaji. Hili limetuchelewesha sana kiuchumi.
Sababu kubwa ya kuzuia wageni kuja nyumbani kwako ni ushaghalabagala uliyoko nyumbani kwako. Kama nyumbani kwako ni kuchafu sana, hakujapangiliwa, Kuna watoto wasiokuwa na nidhamu, hakuna chakula wala viti vya kukalia unaweza kusita kukaribisha wageni nyumbani kwako.
Ili Tanzania iweze kukaribisha wageni lazima mifumo yake ya sheria, TRA, kumiliki ardhi, kutambuana, biashara na masoko iwe imara sana, inayosomana na inayotekelezeka.
Bila kufanya hivyo kufungua mipaka litakuwa janga kubwa sana kwa nchi. Unapofungua madirisha upate hewa safi itaingia hewa safi lakini pamoja na vumbi, majani, mbu, panya, papasi na hewa chafu. Hivyo lazima pia uwe na mifumo imara ya kuvitoa ndani visivyohitajika kuingia.
Hatuna sababu za msingi za kuzuia watu kuja kwetu, hasa wale wenye mitaji na ujuzi.