kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam leo itatoa uamuzi ya sakata la kugombea kuzika mwili wa marehemu Salum Ngindo unaogombewa na mkewe anayetaka uzikwe Kiislamu huku watoto wa marehemu wakitaka azikwe kwa imani ya dini ya Kikristo.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Afumwisye Kibona baada ya mke wa marehemu, Kudra Salum kufungua kesi ya madai dhidi ya watoto watano wa marehemu mumewe aliyefariki Februari 24, mwaka huu katika Hospitali ya Hindu Mandal wakidai kuuzika mwili wa baba yao Kikristo.
Watoto hao ni Matukuta Ngindo, Rose Ngindo, Nono Ngindo, Matukuta Ngindo na Gloria Ngindo.
Wakili wa upande wa Mashitaka, Mussa Roma alidai marehemu aliachana na mke wa kwanza ambaye ni mama wa watoto hao, miaka mingi iliyopita na kufunga ndoa ya Kiislamu na mke wa pili ambaye ni mlalamikaji.
Alidai awali marehemu alifahamika kwa jina la Gerard Ngindo, lakini baada ya kubadili dini alifahamika kwa jina la Salum Ngindo na kufunga ndoa ya Kiislamu na Kudra, Februari 10, 1994 na kuzaa naye watoto.
Alidai kuwa hata baada ya kuishi pamoja, baadaye marehemu aliugua na mlalamikaji ndiye aliyemuuguza kwa kipindi cha miaka sita na baada ya kufa, alitoa taarifa kwa ndugu na watoto wa marehemu kwa ajili ya msibani.
Alidai siku waliyopanga kwa ajili ya maziko, walikwenda katika Hospitali ya Hindu Mandal kuuchukua mwili, lakini baada ya kufika walikuta watoto hao wakiwa na kibali cha kuuchukua mwili kwa ajili ya kuuzika.
Naye Wakili wa utetezi Stephen Tonya alidai marehemu alitumia jina la Salum kama umaarufu, lakini alifahamika kwa jina la Gerard ambalo ni la Kikristo alilozaliwa nalo na hivyo ana wajibu wa kuzikwa Kikristo.
Wakili wa Mashitaka aliwasilisha cheti cha ndoa kati ya marehemu na mlalamikaji ambapo hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapotoa uamuzi wa kuzikwa kwa mwili huo.