kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,331
- 12,647
Watanzania tuna ugoigoi katika kutekeleza na kufanikisha yale tunayoyafikiria, tunayoyapanga na hata yale tuliyoamua kuyatekeleza. Mfano, hata wimbo wa kuhamia dodoma uliimbwa kwa miaka mingi sana kabla ya kutekelezwa'
Siku ambayo gesi yetu itafika Kenya, kesho yake tu asubuhi nishati ya gesi hiyo
1. itasambazwa kwenye viwanda vyote vya uzalishaji kuzalisha bidhaa zenye bei nafuu ambazo zitakuja kuuzwa tanzania kwa bei nafuu kuliko zetu.
2. magari yao yote yatatumia gesi hii nafuu
3, kaya zao nyingi zitapikia gesi wakati sisi tukiendelea kupika na mkaa na kuni.
4. Watajenga kiwanda kikubwa cha mbolea wakayotumia kwenye kilimo chao na nyingine kuja kuuzwa tanzania na kwingine.
5. Vifaa na vipuli rahisi, imara na bora vya vifaa vinavyotumia gesi vitajaa kenya na kuingizwa Tanzania pia kuuzwa.
6. Gesi ya kupikia majumbani itatoka Kenya.
Sisi kwetu pamoja na kuwa na gesi kwa miaka mingi lakini tuna umeme ghali, tunapikia kuni na mkaa, na tunaagiza mbolea kutoka ng'ambo.
Watatuchekaaa saaaana, watatuimbaaa saaaana na watatuona mazombie.
Tukazane sisi kupata matunda ya gesi kabla yao badala ya kuongea sana bila vitendo.