washwa washwa
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 1,613
- 717
Wanafanya mazoezi ya kuchukua nchi km walivyoagizwa na JK na Lukuvi
hao polisi waliopata ZIRO form four hiyo ndo dawa yao
29th April 2014
Kundi la wanajeshi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanadaiwa wamevamia kituo cha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) kilichopo Kwa Mrombo na wanadaiwa kutembeza mkongoto kwa askari kadhaa.
Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kukamatwa, ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotakiwa na NIPASHE kuzungumzia tukio hilo alikanusha.
Hakuna tukio kama hilo, wewe uliona wapi watu wa serikali wanapigana, alihoji Kamanda Sabas na kuongeza: Sisi tulikuwa kwenye vikao vyetu vya kawaida.
Hata hivyo, msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Eric Komba, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana jioni.
Hata hivyo, alisema polisi na JWTZ wanafanya uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zikishawasilishwa makao makuu watatoa taarifa.
Lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tano au sita asubuhi jana, baada ya wanajeshi kuvamia kituo hicho kwa nyakati tofauti.
Inadaiwa wanajeshi hao walikuwa kati ya 50 hadi 60 hivi na haikufahamika mara moja walikuwa wametokea kambi gani ingawa baadhi ya watu walidai walitokea Monduli.
Shuhuda mwingine alisema aliwaona wanajeshi wanne wakiingia kwenye lango kuu la kuingilia kituo hapo na kutembeza kichapo kwa askari aliyekuwapo.
Hata hivyo, habari zingine zinasema hakuna polisi aliyepigwa na hakuna mwanajeshi aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Baadhi ya wakazi jirani na eneo hilo walisema waliwaona kundi la wanajeshi wakiwa katika eneo hilo na wengine wakikimbilia kwenye mashamba.
1. Kituo cha polisi FFU sijawahi kukiona Tanzania hii.
2. Tukio kama hilo lingetokea kama linavyotanabaishwa kwa hakika kusingehitajika kumpigia kamanda simu. Ingekuwa ni vita
3. Askari wa FFU wanaishi kambini...WOTE...or tuseme wanatakiwa wote waishi kambini (hivyo kiuhalisia zaidi ya 80% yao wanaishi kambini)...sasa hao JWTZ wa kwenda kuanzisha vita kambi ya FFU aisee. sijui...labda waende battalion na silaha za nguvu tena si hivi hivi.
4. Sipendi vita kati ya vyombo vya ulinzi na usalama. Natumai hii habari ni rumor tu. au ni ugomvi wa maaskari wawili tu na sio chuki baina ya wengi.

mkuu amini tu ni kweli ffu wamefuliwa nimeshudia ilo tukio ni karibu na ofisi mkuuFFU wanakambi na ofisi zao ni hapo hapo kwenye kambi...sasa kama kweli waliingia hapo na kutoka hiyo ni habari nyingine...
Na kama ni kweli basi subiri muda si mrefu utasikia mziki wake
FFU wanakambi na ofisi zao ni hapo hapo kwenye kambi...sasa kama kweli waliingia hapo na kutoka hiyo ni habari nyingine...
Na kama ni kweli basi subiri muda si mrefu utasikia mziki wake
"Wapigwe tu...na mimi nasema wapigwe tu Tumechoka"!... Long Live Mugabe broda from another mother...