JWTZ wavamia kituo cha FFU na kukisambaratisha

Msemaji wa JWTZ sio Luteni Kanali kama mwandishi anavyoelesema ila ni MEJA Eric Komba. mi marekebisho tuu.
 
wapigwe tuu nasema nawapigwe,, tumewachoka sasa kila siku kuwaua raia wasiona hatia? zaid wangeenda kumpa bakora dogo mlongo.
 
29th April 2014

Kundi la wanajeshi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanadaiwa wamevamia kituo cha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) kilichopo Kwa Mrombo na wanadaiwa kutembeza mkong’oto kwa askari kadhaa.

Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kukamatwa, ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotakiwa na NIPASHE kuzungumzia tukio hilo alikanusha.

“Hakuna tukio kama hilo, wewe uliona wapi watu wa serikali wanapigana,” alihoji Kamanda Sabas na kuongeza: “Sisi tulikuwa kwenye vikao vyetu vya kawaida.

Hata hivyo, msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Eric Komba, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana jioni.

Hata hivyo, alisema polisi na JWTZ wanafanya uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zikishawasilishwa makao makuu watatoa taarifa.

Lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tano au sita asubuhi jana, baada ya wanajeshi kuvamia kituo hicho kwa nyakati tofauti.

Inadaiwa wanajeshi hao walikuwa kati ya 50 hadi 60 hivi na haikufahamika mara moja walikuwa wametokea kambi gani ingawa baadhi ya watu walidai walitokea Monduli.

Shuhuda mwingine alisema aliwaona wanajeshi wanne wakiingia kwenye lango kuu la kuingilia kituo hapo na kutembeza kichapo kwa askari aliyekuwapo.

Hata hivyo, habari zingine zinasema hakuna polisi aliyepigwa na hakuna mwanajeshi aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Baadhi ya wakazi jirani na eneo hilo walisema waliwaona kundi la wanajeshi wakiwa katika eneo hilo na wengine wakikimbilia kwenye mashamba.

hahahahaha. pole yao
 
Huyo askari aliyekuwa zamu hapo getini alishindwa kuwachapa Risasi hao Wanajeshi?!

Angemtoa mfaano mmoja wao...alafu inawezekana ni mayanki tu walizinguana sasa dizain kuonyeshana ubabe ndo wakawatimbia wenzao kikosini

Field Force ipo Dar na Mara tu huko kwingine hakuna kitu...ndo maana kikinuka huko wanachukuliwa huku kupelekwa huko...
 
wameanza mazoezi ya kupindua nchi naona, sasa mbona wenyewe kwa wenyewe? tunasubiria tujue sababu ya hili jambo.
 
Ichi ni kisasi baada ya wiki kadhaa nyuma ffu kumpiga risasi mjeda, ilitosababisha kifo chake, Jana wajeda toka monduli walikuja kumchukua mtuhumiwa wao na mpaka saiv hajarudishwa au kuachiwa
 
1. Kituo cha polisi FFU sijawahi kukiona Tanzania hii.

2. Tukio kama hilo lingetokea kama linavyotanabaishwa kwa hakika kusingehitajika kumpigia kamanda simu. Ingekuwa ni vita

3. Askari wa FFU wanaishi kambini...WOTE...or tuseme wanatakiwa wote waishi kambini (hivyo kiuhalisia zaidi ya 80% yao wanaishi kambini)...sasa hao JWTZ wa kwenda kuanzisha vita kambi ya FFU aisee. sijui...labda waende battalion na silaha za nguvu tena si hivi hivi.

4. Sipendi vita kati ya vyombo vya ulinzi na usalama. Natumai hii habari ni rumor tu. au ni ugomvi wa maaskari wawili tu na sio chuki baina ya wengi.

mmmmh point no 2.....ingekuwa vita kati ya polisi na jeshi au??? hahahahaha

viongoz dhaifu n hatari sana kwa taifa......pinda, kikwete na lukuvi hawajui kauli zao zina marefu na mapana kiasi gan
 
acheni uzushi.

Kambi ya ffu gongo la mboto na kambi ya jeshi sio mbali miaka nenda rudi. Leo ndo yatokee huko Arusha.

Hao jamaa kama wanadai kwamba walikuwa kwenye kikao labda ajenda ilikuwa ni namna ya kuwavunja miguu,shingo na kuwatengu viuno, UKAWA.
Sasa wakawa wameshindana kidogo kutokana sumu ya UKAWA kuwa imeenea mpaka kwenye inner cyrcle ya majeshi yetu. Ndio yakatokea hayo mambo ya kutoleana uvivu mpaka kufikia hali ya kupunguziana uchovu na kugawana maumivu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
1. Kituo cha polisi FFU sijawahi kukiona Tanzania hii.

2. Tukio kama hilo lingetokea kama linavyotanabaishwa kwa hakika kusingehitajika kumpigia kamanda simu. Ingekuwa ni vita

3. Askari wa FFU wanaishi kambini...WOTE...or tuseme wanatakiwa wote waishi kambini (hivyo kiuhalisia zaidi ya 80% yao wanaishi kambini)...sasa hao JWTZ wa kwenda kuanzisha vita kambi ya FFU aisee. sijui...labda waende battalion na silaha za nguvu tena si hivi hivi.

4. Sipendi vita kati ya vyombo vya ulinzi na usalama. Natumai hii habari ni rumor tu. au ni ugomvi wa maaskari wawili tu na sio chuki baina ya wengi.

FFU wanakambi na ofisi zao ni hapo hapo kwenye kambi...sasa kama kweli waliingia hapo na kutoka hiyo ni habari nyingine...

Na kama ni kweli basi subiri muda si mrefu utasikia mziki wake
 
FFU wanakambi na ofisi zao ni hapo hapo kwenye kambi...sasa kama kweli waliingia hapo na kutoka hiyo ni habari nyingine...

Na kama ni kweli basi subiri muda si mrefu utasikia mziki wake
mkuu amini tu ni kweli ffu wamefuliwa nimeshudia ilo tukio ni karibu na ofisi mkuu
 
FFU wanakambi na ofisi zao ni hapo hapo kwenye kambi...sasa kama kweli waliingia hapo na kutoka hiyo ni habari nyingine...

Na kama ni kweli basi subiri muda si mrefu utasikia mziki wake

Mkuu wewe ni FFU nini? mbona unawatetea sana hao waonevu. Acha wapigwe tu
 
reporter acha uongo habari iko ivi askari wa jwtz wakiwa watano walipanda daladala kutoka mjini KWA mrombo.askari wa jwtz walikuwa wamevaa kiraia dona wa daladala kudai kwa watu watano akapewa tsh.500 Badala ya 2000. mzozo ukawa mkubwa sana kumbe kulikuwa na askari wa FFU kwenye hiyo daladala huyu askari wa FFU akamwamuru dereva apeleke GARI kambini FFU KWA mrombo baada ya kufika wale askari WA jwtz wakalipishwa nauli.nakuachiwa kesho yake ambayo ni Jana wale askari watano jwtz walirudi kwalengo la kuvamia mwisho wa siku askari wawili wa jwtz walikamatwa na watatu mpaka sasa hawajulikani walipo kambini kwao orijolo hawajaonekana.hii ndio habari acha kupotosha umma
:
 
Kwanza FFU hawana kituo zaidi ya kambi zao....Pili labda hao JWTZ wawe kundi kubwa la askari kuliko FFU au wawe makomandoo lakini kundi DOGO la askari wa kawaida wa JWTZ hawawezi kuwasambaratisha FFU kirahisi na yangezuka mapigano makubwa....Laiti mngejua mafunzo ya askari wa FFU siku hizi tena wengi wakitokea JKT ndio mngetambua hii habari imekaa kiudaku tu...
 
Safi sana Mizengo Pinda. Kauli yako inafanyiwa utekelezaji mzuri. "Watakaoleta Ujeuri wapigwe tu"

Ikulu wakichelewesha mishahara jeshini "Wapigwe tu"
 
Back
Top Bottom