Nashangaa sana viongozi wa JWTZ wanapogoma kujiuzuru kwa madai ya kuwa JESHI SI SIASA. Nishindwa waelewa kwani jeshi lipo chini ya Wizara ya Ulinzi ambayo msingi wa Siasa, na inaongozwa na Waziri ambaye nae ni Mwanasiasa! Hapa wanapaswa kujiuzuru kwa ile tunasema MINISTERIAL RESPONSIBILITY, Wanapaswa jiuzuru coz hili c tukio lao la kwanza, wanatakiwa wawe Accauntable (wawajibike) kwa matendo yao, wajiuzuru kuepuka balaa siku za usoni, wajiuzuru coz siku 3 kabla ya milipuko walifanya ukaguzi ulioshindwa baini tatizo na pengine yaweza kuwa wao ndio chanzo cha hyo milipuko, wajiuzuru kwa sababu wamelitia taifa hasara, kwan siku c nyingi waliingiza silaha mpya ambazo nazo zimeteketea, viongozi wa jeshi wajiuzuru kwa sababu waweshindwa kutulinda, wamesababisha vifo vya raia na kutishia usalama wa taifa. Ni jambo la kushangaza kwa jeshi lililokuwa bega kwa bega na kampeni za uchaguzi kukana leo kuwa sio la siasa. Wote twajua jeshi letu limejawa na wanasiasa wenye kadi za chama fulani, wanaosubilia nafasi fulani serikalini, so WAJIUZURU KWA SABABU ZA KISIASA "ministerial responsibility", wajiuzuru kwa kuwa wemeshindwa tupa ulinzi sisi raia!
Hebu tusaidie kitaalamu haya matukio yamesababishwa na nini hasa?. Naomba majibu yasiwe ya CCM Vs CDM naomba sababu za kitaalamu nadhani wenzetu mnaweza kuwa na fununu kidogo.