Elections 2010 JWTZ kurusha ndege za kivita katika anga la Dar...

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Wakazi wa Dar wametakiwa kutokuwa na hofu pale ndege za kivita zitapokuwa zikipasua anga la Dar kuanzia leo 25.08.2010 hadi 01.09.2010 kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa kuadhimisha siku ya JWTZ mnamo 01.09.2010 sherehe zitakazofanyika katika kambi ya Navy Kigamboni...

Mara ya mwisho kufanya zoezi hili ilikuwa mwaka 2006 katika kuadhimisha miaka 45 ya uhuru wa Tanganyika...

Ninachoona...??

Huu ni mwaka wa uchaguzi wa inawezekana wanataka kuwatisha wengi Wazee,kina Mama na baadhi ya wenye roho ndogo kuwa jeshi lipo na lipo chini ya Amiri jeshi mkuu Mkulu JK

TAFAKARI!...
 
Ni vema na haki, lakini wawe makini na ndege zao za enzi za mwalimu.
 
Kwani ni lazima warushe ndege Dar wanaweza kufanya mazoezi sehemu nyingine zisizokuwa na msongamano ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo ndege za mwaka 47 zitadondoka.
 
Kwani ni lazima warushe ndege Dar wanaweza kufanya mazoezi sehemu nyingine zisizokuwa na msongamano ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo ndege za mwaka 47 zitadondoka.

Naanza kukosa amani. Mapori mengi Tz wakafanyie michezo yao ya kijeshi huko. Dar eneo dogo watu wengi, ajali ndogo italeta mtafaruku mkubwa
 
Ubovu wa ndege hizo na kelele kama milio wa radi kumbuka zinapita 2 hadi 3 kwa mpigo!,Mwaka 2006 zilikatiza juu ya Hospital ya TMJ,nakumbuka SINTONFAHAMU iliyotokea... Mkuu Nyunyu ile ya Kabuku-Manga sio ya kijeshi... Ila ni ya kawaida kabisa...
 
Huu ni mwaka wa uchaguzi wa inawezekana wanataka kuwatisha wengi Wazee,kina Mama na baadhi ya wenye roho ndogo kuwa jeshi lipo na lipo chini ya Amiri jeshi mkuu Mkulu JK

TAFAKARI!...

Je waliokuwepo walijaribu kuuliza cost za zoezi hilo. Maana hata kama wanataka kutisha wazee mbona nguvu unnessary zinatumika? Hio Pesa ya jetfuel si wangenunulia dawa hospitali, kuweka madawati shuleni etc
 
Ni mazoezi au Air show !!! maana kama ni mazoezi hizo Jet zingeelekea maeneo ya porini au maeneo yasio
na wakazi wengi, na sio kama hapa jijini.

Sasa kama mazoezi wanafanyia hapo jijini, then wakati wa kushehereke hio siku ya JWTZ ndio tuseme
wataenda huko porini kufanya hio Air show au !!!
 
Ubovu wa ndege hizo na kelele kama milio wa radi kumbuka zinapita 2 hadi 3 kwa mpigo!,Mwaka 2006 zilikatiza juu ya Hospital ya TMJ,nakumbuka SINTONFAHAMU iliyotokea... Mkuu Nyunyu ile ya Kabuku-Manga sio ya kijeshi... Ila ni ya kawaida kabisa...

hapo kwenye red..... ilikuwa ya JESHI! Sema haikuwa na rangi ya combat!
 
Tayari zimeanza kurushwa kwa MBWEMBWE! Kama nawaona walimu wa Primary wakijaribu kuwatuliza watoto wanaotaka kutoka nje kushuhudia...
 
Wakazi wa Dar wametakiwa kutokuwa na hofu pale ndege za kivita zitapokuwa zikipasua anga la Dar kuanzia leo 25.08.2010 hadi 01.09.2010 kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa kuadhimisha siku ya JWTZ mnamo 01.09.2010 sherehe zitakazofanyika katika kambi ya Navy Kigamboni... Mara ya mwisho kufanya zoezi hili ilikuwa mwaka 2006 katika kuadhimisha miaka 45 ya uhuru wa Tanganyika... Ninachoona...?? Huu ni mwaka wa uchaguzi wa inawezekana wanataka kuwatisha wengi Wazee,kina Mama na baadhi ya wenye roho ndogo kuwa jeshi lipo na lipo chini ya Amiri jeshi mkuu Mkulu JK TAFAKARI!...

Ndege hizi hurushwa mara nyingi wakati wa maadhimisho ya sherehe za muungano, tar 26 Aprili.
Ukiachilia mbali sherehe hizi, mwaka jana pia yalifanyika mazoezi ya kurusha ndege hizi za kivita kwenye anga la Dar. Kwa uhakika inakera kwa sababu ndege hizi zina kelele sana, kwa hiyo naungana kabisa na wale wanaodai kwamba ilibidi zoezi kama hili lifanyikie porini kama ilivyo kwa kambi ya jeshi kule Ngerengere.
Siamini kwamba zoezi hili ni vitisho, tuache speculations zisizo na sababu za msingi.
 
Moja hiyo imepita sasa hivi, fasta! Loud and supersonic!! Imepita kama kupasua tokea BP (labda kigamboni Navy?), imepita uwanja wa mnazi mmoja mitaa ya peacock na starlight hotels, CCM Mkoa na kupotelea kama unaelekea Muhimbili.

Kila mwaka hufanya mazoezi ya ndege hizi kufanya "fly-by" especially siku za uhuru na mashujaa. Sasa iweje leo wafanyie porini, au zianguke tuu hivi hivi? Waacheni porfessionals wafanye kazi zao, bana! Samsing nyuu and eksaiting in ze cite!!!
 
Kwani ni lazima warushe ndege Dar wanaweza kufanya mazoezi sehemu nyingine zisizokuwa na msongamano ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo ndege za mwaka 47 zitadondoka.

hapana tutarusha MIGS 41 latest model, F14 na F16. Bahati mbaya stealth fighter zote tumezipeleka Israel na Marekani kwa ajili ya check3
 
Back
Top Bottom